Sauti ya umauti masikioni mwangu

Okwaaa

JF-Expert Member
Dec 3, 2020
1,316
2,917
Habari ya usiku wana jf!

Leo ninayofuraha kuweka bando kwenye simu yangu baada ya siku nyingi bila kuweka bando!

Kwanini hiyo heading! Ipo hivi, mm kijana wa miaka 28.6, lakini nipo kama mtu mzima wa miaka 40. Sijaoa wala sina mtoto. Maisha nayoyaishi hiki kipindi sidhani kama Mungu ndiye aliyepanga niyaishi. Naishi maisha ya ovyo sanaa. Nimelelewa na mama tu na ndiye aliyenipambania hadi kupata haka kaelimu ka ovyo ambako hakana msaada na mm kabisa.

Ipo hivi, mwaka huu tangu uanze sina hamu nao tena maana ulikaribishwa kwa majanga ya kuanza kumwuguza mama yangu. Toka mwezi wa 11 hadi huu mwez wa tatu ndo bi mkubwa amerudishwa nyumbani. Nimempambania ili nisije kubaki na uchungu hapa duniani kama mama angefariki. Ningejiona sina maana kabisa ukizingatia mama aliza vitu vyake vyote ili anisomeshe mm akiamini nikipata ajira nitamtunza. Marehemu hasemwi vibaya ila utawala wa mwamba umeniharibia future yangu kwa 100%.

Tuachane huyo marehemu na utawala wake,. Baada ya mama kulazwa ilibidi nitoe hela yangu yote hadi hela iliyokuwa kwenye biashara nikatoa yote. Haikutosha ikabidi nianze kukopa hela kwa wakopeshaji wa mitaani maana walikuwa wananiamin kuwa nitawalipa maana nilikuwa nafanya biashara na wao wanaona. Nimeingiza deni kubwa sana saiz linasoma milion 6. Mimi sina ata mia mbovu, yan ata cha kuuza. Uwanja nilishauza muda. Sasa jana nimeambiwa na mmoja wa watu niliowakopa akaniambia "nitakudai kwa namna nyingine" hii kauli imenitisha sanaa, niliwaza nitakamatwa na police ila nahisi hapana ni uchawi utatumika na jana usiku nimelala vibaya sijui n wenge sijui ndo simu ya kifo yenyewe hiyo nilipigiwa ndotoni!

Mwisho mimi nina amani kuona nimemsaidia bi mkubwa. Lakini pia nina huzuni maana nahisi nakufa muda wowote na nawaza mama atasikiaje habari ya mimi kufa, nawaza mchumba niliyekaa nae miaka mitatu akinisubiri nimuoe atasikiaje habari ya mm kufariki. Kiufupi hicho ndo kinanitisha. Lakini acha iwe hivo tu maana sina uwezo wa kulipa hizo hela mimi.

Makala ni ndefu poleni ila nawaomba tuwapende mama zetu, usimtendee baya mama yeyote huendi ndiye mama yangu ambaye nitamwacha pekee yake hapa duniani bila uwepo wangu. Upendo ni amri kuu ya Mungu!
 
usimtendee baya mama yeyote huendi ndiye mama yangu ambaye nitamwacha pekee yake hapa duniani bila uwepo wangu. Upendo ni amri kuu ya Mungu!
Hapo ndo umefikia changamoto za kiutu uzima na za kiume pia wala usiogope ni za kawaida tu, na wanaume tulio wengi tumepitia changamoto za namna hiyo na tumezishinda tulizana, kaa chini panga mipango mipya ya kuanza kutengeneza uchumi madhubuti
 
Habari ya usiku wana jf!

Leo ninayofuraha kuweka bando kwenye simu yangu baada ya siku nyingi bila kuweka bando!

Kwanini hiyo heading! Ipo hivi, mm kijana wa miaka 28.6, lakini nipo kama mtu mzima wa miaka 40. Sijaoa wala sina mtoto. Maisha nayoyaishi hiki kipindi sidhani kama Mungu ndiye aliyepanga niyaishi. Naishi maisha ya ovyo sana...
Tuanze kukutumia rambirambi kbisa?
 
Habari ya usiku wana jf!

Leo ninayofuraha kuweka bando kwenye simu yangu baada ya siku nyingi bila kuweka bando!

Kwanini hiyo heading! Ipo hivi, mm kijana wa miaka 28.6, lakini nipo kama mtu mzima wa miaka 40. Sijaoa wala sina mtoto. Maisha nayoyaishi hiki kipindi sidhani kama...
Itaendelea?
 
hapo ndo umefikia changamoto za kiutu uzima na za kiume pia
wala usiogope ni za kawaida tu, na wanaume tulio wengi tumepitia changamoto za namna hiyo na tumezishinda.
tulizana, kaa chini panga mipango mipya ya kuanza kutengeneza uchumi madhubuti
Mkuu unahisi nitaanzia wapi? Sina ata thumuni moja. Yani ningekuwa na ndugu ningemuomba ata anitoe kafara ili amtunze mama. Yani sina pa gususa mm. Huenda wengine walibakisha sehemu za kushika
 
Hukujiumba wewe, Mungu anakuona na hatakuacha japo utaona amekuacha. Usikate tamaa na endelea kumuita
FB_IMG_17108777184281008.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom