Sijui nifanyaje naomba ushauri

Sijui nifanyaje naomba ushauri

Na inakuaje ukajisikia kabla hujajiandaa?
Usipomaliza kujiandaa inakuaje; kujisikia kutakoma au hakutakuja kabisa?
Kwani hisia za kuoa zinaletwaga na nini?
Usipojiandaa kwa wakati inakuaje wakati Binti wa watu umemuweka pending anasubiri tu hapo?
Ina maana walioko tayari ila hawajaoa wanasubiri wajisikie?
Vipi wale waliooa ila hawajisikii kuoa imetokea nini? Huko ''kujisikia'' kuna beba uzito gani kwenye maisha ya mume na mke? Mbona anajisikia kwenda kunywa maziwa tu bwerereeeeeeeee??

NB: Lengo langu sio kupata majibu, ila uone/ufikiri zaidi ya unachokisoma.

vyote vinafanya kazi sambamba ndo maana ukioa lazima uwe umejiandaa na ni muhimu kufanya kitu unachojisikia ukiona ujapata hamu ya kuoa ujue may be muda wako bado
 
nyooo miaka Tisa nabembeleza ndoa bado MTU anasema bado ...keshokutwa anakuja kukuletea kadi ya harusi anaoa...wakati Mie nshaanza kupata makunyanzi...
utazirudisha siku nyuma au?


Aisee Huyo binti atakua ana mdudu kichwani.

mbona unaongea as if ni kitu cha upande mmoja sijakupata point yako
 
Hujisikii kuoa,na vilevile bado mda wa kuoa labda miaka3 au 4 lkn mapenzi unajisikia kufanya jishangae
 
Huyo jamaa analeta utani na maisha ya mwenzie, kama hayuko tayari bora amwache tuu
 
kama humtaki mwache akaolewe, maana mwanamke kuchelewa kuzaa kuna athari. wewe unaweza zalisha muda wowote utakao. hata ukiwa kama Vladimir Putney utazalisha. lakini mwenzako akiwa 30 and above anaanza kufikiria mikasi ya upasuaji
 
mwanamke anasema umri wake wa kuwa na mtoto umefika anataka azae akiwa kijana mwenyewe nguvu hataki kuja kuzaa wajukuu kimsingi jamaa anamuona mdada bado muda anao wa kutosha anaisi labda kuna external force ndo maana mdada kachachamaa
changamoto hii...kumpoteza mtu mliyekuwa na mahusiano ya muda mrefu hivyo si vizuri,halikadhalika kuingia kwenye ndoa pasipo maridhiano ya pamoja si jambo jema...nadhani mmojawao ajishushe na kuangalia mazuri ya hitaji la mwenzie,,kupitia hayo yanaweza mjengea mtazamo wa kukubaliana...yaweza kufunga ndoa isiwe sasa,lakini pia si kufika muda wa miaka minne...
 
sidhani kama hilo neno "hamu" umelitumia kwa usahihi maana kama unasubiri hadi upate hamu ya kuoa au ya kuwa na mtoto basi kuna tatizo, je hio hamu isipokuja kabisa ndio ndoa hamna?? Sio justication nzuri kwa mtu mwenye upeo mwema, ujana una mwisho, kesho inakuja, kama unataka kumuoa heri muaone saa hizi.
 
Hahahaaaaa very interesting

Jamaa kanogewa na uhuru wa kifedha na kimaisha Kwa ujumla. Anaona ndoa itamfunga kitanzi ashindwe kula bata angali bado ana Miaka miwili tu kazini. Ndio shida ya kuchelewa kushika hela

Mwambie kuwa ndoa haito mzuia kula ujana, ni makubaliano tu ya namna mtakavyo ishi kwahiyo aache kumtesa mdada wa watu. Akizubaa anaolewa huyo na ataanza kuhangaika kujenga mahusiano mapya na mwanamke mwingine
 
mbona unaongea as if ni kitu cha upande mmoja sijakupata point yako

Huyo binti ana mdudu anapofushwa na mtu asiyekuw na hamu ya kummiliki...
put yourself in her shoes ...
 
Hahahaaaaa very interesting

Jamaa kanogewa na uhuru wa kifedha na kimaisha Kwa ujumla. Anaona ndoa itamfunga kitanzi ashindwe kula bata angali bado ana Miaka miwili tu kazini. Ndio shida ya kuchelewa kushika hela

Mwambie kuwa ndoa haito mzuia kula ujana, ni makubaliano tu ya namna mtakavyo ishi kwahiyo aache kumtesa mdada wa watu. Akizubaa anaolewa huyo na ataanza kuhangaika kujenga mahusiano mapya na mwanamke mwingine

Asante mkuu hata mimi nahisi kijana unaisi uhuru wake utapungua sana au bado anaisi yeye ni mdogo
 
sidhani kama hilo neno "hamu" umelitumia kwa usahihi maana kama unasubiri hadi upate hamu ya kuoa au ya kuwa na mtoto basi kuna tatizo, je hio hamu isipokuja kabisa ndio ndoa hamna?? Sio justication nzuri kwa mtu mwenye upeo mwema, ujana una mwisho, kesho inakuja, kama unataka kumuoa heri muaone saa hizi.

Nadhani watu mmeelewa vibaya neno hamu alichozungumzia ni ile willingness yake kuingia kwenye maisha ya ndoa kutake ile step ndo anaona wakati bado
 
changamoto hii...kumpoteza mtu mliyekuwa na mahusiano ya muda mrefu hivyo si vizuri,halikadhalika kuingia kwenye ndoa pasipo maridhiano ya pamoja si jambo jema...nadhani mmojawao ajishushe na kuangalia mazuri ya hitaji la mwenzie,,kupitia hayo yanaweza mjengea mtazamo wa kukubaliana...yaweza kufunga ndoa isiwe sasa,lakini pia si kufika muda wa miaka minne...

Asante mkuu
 
Na inakuaje ukajisikia kabla hujajiandaa?
Usipomaliza kujiandaa inakuaje; kujisikia kutakoma au hakutakuja kabisa?
Kwani hisia za kuoa zinaletwaga na nini?
Usipojiandaa kwa wakati inakuaje wakati Binti wa watu umemuweka pending anasubiri tu hapo?
Ina maana walioko tayari ila hawajaoa wanasubiri wajisikie?
Vipi wale waliooa ila hawajisikii kuoa imetokea nini? Huko ''kujisikia'' kuna beba uzito gani kwenye maisha ya mume na mke? Mbona anajisikia kwenda kunywa maziwa tu bwerereeeeeeeee??

NB: Lengo langu sio kupata majibu, ila uone/ufikiri zaidi ya unachokisoma.

mkuu nikupata ila kuna tofauti kubwa sana kuoa na kunywa mazima ,kunywa mazima hata watoto wa secondary wanaweza ila step ya kuoa unatakiwa kujipima vya kutosa kuanzia mind yako hadi saikolojia
 
Umeongea point ya msingi.

Nafikiri kitu ambacho huwa kinasumbua sana ni hiki ''NITAMWOA NANI'' ukishajiridhisha ni fulani, huwa haisubiri kujiskia tena mkuu.. huenda kuna kitu huyu ndugu hasemi au hana hakika bado ila umri wa mahusiano yao ndio unasimamam mbele yeke uso wake kila anavyotaka kufikiri vinginvyo.

Tafakuru yakinifu na inahitajika hapa ili aweze kujing'amua. Vinginevyo lolote laweza kutokea ambalo sasa hulioni.

mkuu nikupata ila kuna tofauti kubwa sana kuoa na kunywa mazima ,kunywa mazima hata watoto wa secondary wanaweza ila step ya kuoa unatakiwa kujipima vya kutosa kuanzia mind yako hadi saikolojia
 
Ikiwa nitasoma mawazo yako sawa, this applies to...why buy a cow when you can a get a milk for free? Huyo dada ni muda umefika, kama unampenda kweli toa nia ya kuoa. Hiyo miaka 3 ni mirefu....lakini kusema hujisikii sio sababu.......
 
Back
Top Bottom