brave one
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 4,879
- 7,393
Habari wadau.
Nina mpenzi wangu tulianza mahusiano tangu tuko O level, chuo mpaka sasa tupo makazini tuna miaka 9 kwenye uhusiano mpaka sasa na wote tuna umri sawa miaka 28. Tatizo kuna vitu viwili tunatofautiana vina hatarisha mahusiano yetu.
Moja, Ndoa mwenzangu anaona muda muafaka wa kufunga ndoa umefika wakati mimi bado sijisikii kuoa na sio kwamba sitaki kumuoa ila ile hamu ya kuoa bado sina yaani utayari wa moyo kuingia kwenye ndoa bado haupo kwenye mawazo yangu najiona nikimuoa 2018 au 2019.
Pili, Mtoto yeye mwenzangu anaona muda wa kuwa na mtoto umefika lakini mimi bado sijapata hamu ya kuwa na mtoto sijapata hamu ya kuwa baba atleast mpaka miaka 3 au 4 mbele.
Kimsingi nina miaka miwili tu kazini yeye ana mwaka mmoja.Tumejitaidi kuzungumza nikampa mawazo yangu hakubaliani nayo na nimemsikiliza yake napata wakati mgumu sijui nifanyaje.
Haya ni maelezo ya jamaa yangu hapa kazini ananiomba ushauri, wadau nisaidie mawazo maana amenipa muda nitafakari nimjibu baadae.
Karibuni sana.