Sijui neno hili lilitoka wapi

Sijui neno hili lilitoka wapi

Translator

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2017
Posts
286
Reaction score
297
Kwenye Kiswahili hakuna neno "kupelekea".
Hili ni moja ya maneno yaliyopata mashiko siku hizi
lakini ukweli ni kuwa hiyo ni "broken language".

Mfano:
1. Tatizo hili limepelekea kila mtu kujihoji.
2. Kuchekelewa kumepelekea tumkose.
3. Ajali imepelekea vifo vya watu wawili.
............
Kimsingi, neno sahihi ni "sababisha".

1. Tatizo hili limesababisha kila mtu kujihoji.
2. Kuchekelewa kumesababisha tumkose.
3. Ajali imesababisha vifo vya watu wawili.
 
Siku hizi lugha za mitaani zimezuka sana ambazo sio rasmi
 
Kwenye Kiswahili hakuna neno "kupelekea".
Hili ni moja ya maneno yaliyopata mashiko siku hizi
lakini ukweli ni kuwa hiyo ni "broken language".

Mfano:
1. Tatizo hili limepelekea kila mtu kujihoji.
2. Kuchekelewa kumepelekea tumkose.
3. Ajali imepelekea vifo vya watu wawili.
Wamelitohoa kutoka kwenye neno la Kiingereza (lead) kwa tafsiri ya moja kwa moja (direct translation)...
 
Bila Shaka Limeletwa Na Kabira Fulani Mashuhuli Sana Kwa Kuvuruga Kiswahili Apa Tz Ususani Utasikia
Umeniletelezea/Umeleteleza.
 
Back
Top Bottom