PostGE2025 Mambo muhimu ambayo Tume ya Uchunguzi ya Jaji Chande imeyapuuza

PostGE2025 Mambo muhimu ambayo Tume ya Uchunguzi ya Jaji Chande imeyapuuza

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
26,787
Reaction score
26,761
Wakuu naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Yafuatayo ni mambo nyeti ambayo tume ya uchunguzi wa mauaji ya MO29 imeyaepuka kwa sababu ambazo wanazijua wao wenyewe:

1. Chanzo cha machafuko
Tume haijataja chanzo cha tatizo ni nini kwa kuwa kinagusa mamlaka moja kwa moja. Kila mtu mwenye akili timilifu anafahamu chanzo cha tatizo ni serikali ya CCM kuteka uchaguzi. Na hili tatizo lilianzishwa na Magufuli tangu uchaguzi wa mwaka 2020 na limerithiwa na Samia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024. Kutokuwepo kwa uchaguzi kumesababisha kusiwepo na haki wala amani na kupelekea wananchi kujilipua Oktoba 2025.

2. Wauaji ni akina nani?
Watekelezaji wa mauaji ya halaiki siku ya MO29 hawatatajwa kwenye ripoti hii. Utasubiri sana. Na tulitegemea hilo.

3. Ni wapi ilipo miili ya marehemu?
Maelfu ya miili ya marehemu iliyookotwa mitaani na kunyakuliwa kutoka hospitalini, hadi sasa haijulikani wameipeleka wapi. Tume haijagusia jambo hili hata kidogo.

4. Idadi ya wananchi waliopigwa risasi.
Inakadiriwa maelfu ya watu waliuawa lakini hadi sasa mamlaka haijataja idadi. Wanaogopa kutaja idadi kwa sababu baadhi ya miili waliichukua na kuondoka nayo kusikojulikana.

5. Hatua watakazochukuliwa wauaji
Pamoja na kwamba baadhi ya wauaji walionekana hadharani na mibunduki yao wakiwa wamevaa nguo za kiraia huku wakiwalenga raia na kuwaua kwa risasi kama nyumbu, usitegemee kwamba wangetajwa na hii tume mchongo iliyoandaliwa mahsusi kwa ajili ya kuficha ukweli wa mambo.

6. Mengineyo....
Kama kuna mengine ambayo nimeyasahau, mnaweza kuongezea wakuu.

MAONI YANGU
Kwa ufupi ni kwamba hii tume imesababisha maswali mengi zaidi ya majibu na imetonesha vidonda vya ndugu waliopoteza mali pamoja na wapendwa wao. Dalili zilionekana tangu awali kwa kuwa wahusika wakubwa wa matukio haya....polisi na watawala....hawakufikiwa na tume na wala hawakualikwa kujibu madodoso wala kufanya mikutano ya ana kwa ana na tume hii ya mchongo.

Nawasilisha.
 
Wakuu naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Yafuatayo ni mambo nyeti ambayo tume ya uchunguzi wa mauaji ya MO29 imeyaepuka kwa sababu ambazo wanazijua wao wenyewe:

1. Chanzo cha machafuko
Tume haitasema chanzo cha tatizo ni nini kwa kuwa kinagusa mamlaka moja kwa moja. Kila mtu mwenye akili timilifu anafahamu chanzo cha tatizo ni serikali ya CCM kuteka uchaguzi. Na hili tatizo lilianzishwa na Magufuli tangu uchaguzi wa mwaka 2020 na limerithiwa na Samia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024. Kutokuwepo kwa uchaguzi kumesababisha kusiwepo na haki wala amani na kupelekea wananchi kujilipua Oktoba 2025.

2. Wauaji ni akina nani?
Watekelezaji wa mauaji ya halaiki siku ya MO29 usitegemee kwamba watatajwa kwenye ripoti hii. Utasubiri sana.

3. Ni wapi ilipo miili ya marehemu?
Maelfu ya miili ya marehemu iliyookotwa mitaani na kunyakuliwa kutoka hospitalini, hadi sasa haijulikani wameipeleka wapi. Tume haitagusia jambo hili hata kidogo.

4. Idadi ya wananchi waliopigwa risasi.
Inakadiriwa maelfu ya watu waliuawa lakini hadi sasa mamlaka haijataja idadi. Wanaogopa kutaja idadi kwa sababu baadhi ya miili waliichukua na kuondoka nayo kusikojulikana.

5. Hatua watakazochukuliwa wauaji
Pamoja na kwamba baadhi ya wauaji walionekana hadharani na mibunduki yao wakiwa wamevaa nguo za kiraia huku wakiwalenga raia na kuwaua kwa risasi kama nyumbu, usitegemee kwamba watatajwa na hii tume mchongo iliyoandaliwa mahsusi kwa ajili ya kuficha ukweli wa mambo.

6. Mengineyo....
Kama kuna mengine ambayo nimeyasahau, mnaweza kuongezea wakuu.

MAONI YANGU
Kwa ufupi ni kwamba hii tume itasababisha maswali mengi zaidi ya majibu na itatonesha vidonda vya ndugu waliopoteza mali pamoja na wapendwa wao. Dalili zilionekana tangu awali kwa kuwa wahusika wakubwa wa matukio haya....polisi na watawala....hawakufikiwa na tume na wala hawakualikwa kujibu madodoso wala kufanya mikutano ya ana kwa ana na tume hii ya mchongo.

Nawasilisha.
nonsense
 
Kwa hali hii ndipo wananchi watakapoona umuhimu wa kianzishwa kwa tume huru ya uchunguzi, itakayo ongozwa na watu na maslahi na upande wowote ule wa washukiwa wa hizo vurugu.

Kwa sababu haiwezekani uanzishe tume ya uchinguzi, huku wewe mwenyewe ukiwa ni mtuhumia pia. Kwa namna yoyote ile lazima utawaangushia wengine gunia la lawama, na wewe mtuhumiwa namba moja ukijitoa.
 
Na hili ndilo lengo kuu la kuanzisha tume. Sio kwa sababu nyingine bali imelenga kuficha ukweli na kuwalinda wahusika wa tukio hili.
 
Kama kuna walau jambo moja litatajwa kati ya haya niliyosema hapa, njoo mnikamate mniue.
 
Back
Top Bottom