Bawasiri bila upasuaji

Bawasiri bila upasuaji

Joined
May 18, 2026
Posts
24
Reaction score
6

BAWASIRI NI NINI?

Bawasiri ni Ugonjwa unaotokana na kuvimba/kupasuka kwa mishipa ya dawa sehemu ya haja kubwa na kupelekea kuota kwa kinyama/Uvimbe ambao ndio huitwa Bawasiri.

Sababu kubwa ya mtu kupata Bawasiri ni Mgandamizo sehemu ya haja kubwa ambapo mgandamizo huo hupelekea kupasuka/kuvimba kwa mishipa midogo midogo ya damu aina ya veins sehemu ya haja kubwa hivyo hupelekea kuota kwa kinyama, miwasho, maumivu makali na kutoa damu.

Ugonjwa huu umekuwa ni ugonjwa hatari kutokana na tabia za wagonjwa kuficha kutokana na aibu ya tatizo lenyewe lilipo au kuhofia jamii kumtazama tofauti kwa sababu jamii nyingi hasa za Afrika Mashariki zinaamini kuwa ugonjwa huu ni mkosi mkubwa.

DALILI ZA MTU MWENYE BAWASIRI

  1. Kupata muwasho mkali katika eneo la juu la haja kubwa.
  2. Kujitokeza kwa kinyama/vinyama eneo la haja kubwa.
  3. Kutokewa na kiuvimbe katika tundu ya haja kubwa.
  4. Kupata kinyesi chenye damu.
  5. Kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia.
  6. Kupata maumivu ya tumbo/kiuno hasa Bawasiri inapofikia hatua mbaya.

AINA ZA BAWASIRI

Kuna aina 2 za Bawasiri kama ifuatavyo:

1. BAWASIRI YA NJE

Ni kuota kinyama sehemu ya nje ya haja kubwa ambapo kinyama huwa nje hata kama hujaenda kujisaidia haja kubwa.

2. BAWASIRI YA NDANI

Ni kuota kinyama sehemu ya ndani ya haja kubwa mara nyingi huambatana na maumivu makali na damu na kinyama hutoka wakati wa kujisaidia haja kubwa.

Bawasiri ya ndani ina hatua NNE ambazo ni:

HATUA YA KWANZA

Katika hatua hii mtu hujihisi maumivu makali, miwasho pamoja na kutokwa damu wakati wa kujisaidia na kinyama hakionekani wakati wa kujisaidia.

HATUA YA PILI

Hii hutokea wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe punde baada ya kujisaidia.

HATUA YA TATU

Hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenyewe ama inaweza kurudi yenyewe baada ya muda.

HATUA YA NNE

Hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi baada ya kujisaidia.

VISABABISHI/MAMBO YANAYOWEZA KUSABABISHA MTU KUPATA BAWASIRI

  1. Uzito kupita kiasi (Overweight).
  2. Ujauzito.
  3. Unywaji pombe.
  4. Kukaa sana sehemu ngumu.
  5. Kuingiliwa sehemu ya haja kubwa.
  6. Kujisaidia Choo Kigumu.

Sababu za kujisaidia choo Kigumu ni:​

  • Vidonda vya TUMBO.
  • Ngiri/Hernia.
  • Ulaji duni.
  • Kuwa na acid mwingi tumboni.
  1. Kula sana nyama nyekundu.
  2. Presha ya kupanda.
  3. Kula sana pilipili.
  4. Kula udongo (Wajawazito na watoto wadogo).
  5. Kujisaidia kwenye vyoo vya kukaa.
  6. Kuharisha kupita kiasi.
  7. Kufanya kazi ngumu/kunyanyua vitu vizito.

MADHARA/ATHARI ZA BAWASIRI

  1. Upungufu wa damu mwilini.
  2. Kutokwa na kinyesi bila kujitambua.
  3. Kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.
  4. Kupungukiwa nguvu za kiume.
  5. Kupungukiwa na uwezo wa kufanya kazi kutokana na maumivu.
  6. Kupata tatizo la kisaikolojia.
  7. Kutopata ujauzito.
  8. Mimba kuharibika.
  9. Kupata kansa ya utumbo (Colorectal Cancer).
  10. Mwili kudhoofika.

NJIA ZA KUJIKINGA DHIDI YA BAWASIRI

  1. Kula mboga za majani na nafaka zisizo kobolewa kwa wingi.
  2. Kunywa maji mengi lita 2.5 hadi 3 kwa siku.
  3. Acha kufanya mapenzi kwa kutumia tundu la haja kubwa (kulawitiwa).
  4. Punguza kukaa chooni kwa muda mrefu, kunaweza kuongeza shinikizo katika njia ya haja kubwa.
  5. Acha kunywa pombe.
  6. Punguza kula nyama nyekundu.
  7. Punguza matumizi ya pilipili.
  8. Jitibie vidonda vya tumbo.
  9. Jitibie Ngiri.
  10. Dhibiti uzito wako.
  11. Jiepushe/punguza kunyanyua vitu vizito mara kwa mara.

MATIBABU YA UGONJWA WA BAWASIRI

Kuna matibabu aina mbili katika kutibu ugonjwa wa Bawasiri:

1. MATIBABU YA KISASA

Matibabu ya kisasa yanahusisha matibabu ya Hospital ambapo tiba kubwa ya Bawasiri kwa hospital ni kufanyiwa upasuaji mdogo (minor surgery) kwa ajili ya kuondoa kinyama.

Changamoto kubwa ya matibabu haya ni kwamba asilimia kubwa ya wagonjwa wanaofanya upasuaji wa tatizo hili tatizo hujirudia kwa sababu upasuaji huondoa athari ya tatizo na si mzizi wa tatizo yaani ni sawa na kukata mti kisha ukaacha mizizi bila shaka mti huo utachipua na kumea tena.

Lakini pia Upasuaji wa Bawasiri huwa na maumivu makali sana na uponaji wa kidonda hufika mpaka miezi miwili, hali hii ya kukaa na kidonda kwa muda mrefu kunaweza kupelekea kupata Kansa ya utumbo (Colorectal Cancer).

2. MATIBABU KWA NJIA ASILI

Matibabu haya yanahusisha utumiaji wa dawa zinazotokana na mimea dawa.

Dawa hizi Hutibu Bawasiri bila kufanya upasuaji na huweza kuleta matokeo ya haraka kwa mgonjwa endapo atatumia dawa huku akijitahidi kujiepusha na visababishi vyote vinavyopelekea mtu kupata Bawasiri.

Zipo dawa asili nyingi na nzuri sana katika kutibu Bawasiri, mfano wa dawa hizo ni Bawasiri Fluid na Bawasiri Powder, dawa hizi zina ufanisi mkubwa katika kutibu Bawasiri endapo Mgonjwa atazingatia maelekezo.

ZIJUE SABABU ZINAZOWAFANYA WAGONJWA WENGI WA BAWASIRI KUTUMIA DAWA NYINGI BILA MAFANIKIO

Kwanza Mgonjwa wa Bawasiri anatakiwa kufahamu ya kwamba, matibabu si dawa pekee.

Watu wengi wanaamini kwamba matibabu ni dawa pekee na jambo hili limepelekea wengi kuteseka na matatizo kwa muda mrefu sana bila mafanikio na kupelekea kukata tamaa ya kutafuta tiba na badala yake humuona kila mtoa huduma ni tapeli.

Zifuatazo ni sababu zinazowafanya wagonjwa wengi kuteseka na Bawasiri kwa muda mrefu licha ya kutumia dawa mbali mbali:

1. Kutopata dawa sahihi

Si kila dawa inayotangazwa kutibu Bawasiri inaweza kutibu Bawasiri bali dawa yenye ufanisi wa kutibu ndio inaweza kutibu Bawasiri.

2. Kutofuata ushauri wa daktari

Usipofuata yale ambayo daktari anakuelekeza ili kupata suluhisho la Tatizo lako ni ngumu kupona tatizo lako.

3. Kutoziacha sababu zilizopelekea upate Bawasiri

Katika hili wengi wamefeli kwani haiwezekani ukapona Bawasiri ikiwa sababu zilizopelekea upate Bawasiri hutaki kuziacha.

Mfano:

  • Pombe
  • Uzito mkubwa
  • Ulaji mbovu
  • Kuingiliwa kinyume
  • Kula sana pilipili
  • Kukaa sana sehemu ngumu
  • Kunyanyua vitu vizito
  • Kutotibu Magonjwa kama Ngiri na Vidonda vya TUMBO
  • Kutokula vyakula vya kulainisha choo kama vile Mboga za majani & matunda
  • Kula udongo (wajawazito)
  • Kujisaidia kwenye vyoo vya kukaa
  • Kuharisha mara kwa mara
  • Kujisaidia choo Kigumu
Hata utumie dawa zaidi ya 100, usipoziacha ona Tapeli kumbe sababu ni wewe mwenyewe kutofuata miongozo, maelekezo na USHAURI kutoka kwa daktari.

⚫ Ukizingatia hayo utapona Bawasiri kwa muda mfupi sana (week 1 mpaka 3) Biidhnillaah japo wapo wanaopona kwa siku 5 licha ya kukaa na Bawasiri kwa miaka kadhaa.
 
Leo siku ya 3 kuna kipele kigumu na kina maumivu makali kimenitokea,
Nahisi inaweza kua yenyewe,

Hapo kwenye nyama nyekundu nahisi ndio tatizo limeanzia hapo, hizo sababu zingine ni kwa mbaaaaliii😢
 
Leo siku ya 3 kuna kipele kigumu na kina maumivu makali kimenitokea,
Nahisi inaweza kua yenyewe,

Hapo kwenye nyama nyekundu nahisi ndio tatizo limeanzia hapo, hizo sababu zingine ni kwa mbaaaaliii😢
Karib kwa msaada wa matibabu ikiwa bado hujapata suluhisho
0743 549 126
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom