Sijui lini nitapata mke mwema

Sijui lini nitapata mke mwema

Mungu humpa mume mwema mke mwema. Anza sasa kwa kubadilika na ujiandae kuwa mume mwema then Mungu atakupa mke mwema na ujue mke mwema atoka kwa bwana.

Haijalishi kuwa mume mwema ndio upate mke mwema.kuna mdada namfahamu yupo so innocent maskini ya mungu lakini kaolewa na jamaa mlevi na anamtwanga deile,uzuri wote unapotea...so ni mipango ya Mungu na bahati tu ya mtu...sio lazima wote muendane...
 
bado sijaoa kwa sasa na sijawahi kujihusisha na mahusiano mpaka sasa.sasa hivi nimeshakuwa mtu mzima nataka nianze kutafuta mwenza.lakini nacho ogopa mpaka sasa ni kuanzisha mahusiano halafu baadae kusalitiwa.ndio maana nimeamua kuomba ushauri kwenu ili nisije kukosea katika kuchagua .
mwombe mungu atakupa aliye mwema ,once unaoanzisha uhusiano mshirikishe mungu ili kama kuna lolote upande wa pili ulione kwa haraka. 2. Usikimbilie zinaa kwa utakayempata.3. Pata muda wa nyie kufahamiana. 4.usiogope kuachana na utakayempata ila chunga sana usiwe chanzo cha nyie kuachana.
 
Katika nyakati zetu za sasa ni vigumu sana kumpata mwanamke aliye mwema.

Moyoni mwangu nafikiri sana nionapo marafiki wangu jinsi walivyo salitiwa na wapenzi wao.

Nauliza nyinyi mlio oa na kupata wake wema mlifanyaje mpaka mkawapata hao maana ninampango wa kutafuta mke.

usishangae rafiki zako kusalitiwa,je walikuwa waume wema??unajua wanaume wanasahau kuwa si tu mwanamke anatakiwa kuwa mke mwema,bali hata yeye inabidi awe mume mwema ili mke azidi kumpenda n kumuheshimu ndipo wema wao utazaa matunda mazuri.
 
hamna ujanja kwa kweli ni kupiga magoti kwa imani na kumwomba Mwenyezi Mungu,yeye ndiye mpaji!
 
Hata siku moja! Haiwezekani Mungu akupe Malaika wakati wewe mwenyewe ni Ibilisi.

Mungu alipomuumba mwanaume/mwanamke aliumba pia wa kufanana naye. Ukiona mwenzi wako hamuendani naye ujue huo si ubavu wako tafuta wa kwako ukishindwa mshirikishe Mungu utafanikiwa.

kumpata wa kuendana nae ndo mziki mnene. Try and error zitakufanya umalize wanawake wote dunia hii
 
kwahyo kama biblia haisemi chochote kuhusu wananume wema, kwahyo unadhani wanaume wote ni wema? kwaninm wadada huwa wanapata tabu kutafuta waume wema?? according to you seemz like wanaume wote ni wema.
mwanaume haitaji kuwa mwema.mwanamke akiwa mwema ni advantage kwake. hakuna mtu anayetaka kitu kibaya. sijasema popote kuwa wanaume wote ni wema nilichosema mwanamke ndie anaetakiwa kuwa mwema
 
kumpata wa kuendana nae ndo mziki mnene. Try and error zitakufanya umalize wanawake wote dunia hii
Lisilowezekana kwa mwanadamu kwa Mungu linawezekana...

Ukitumia akili zako unaweza kujikuta kabla ya kumpata wa kuendana naye dunia ya leo unazimwa na Ukimwi.
 
Katika nyakati zetu za sasa ni vigumu sana kumpata mwanamke aliye mwema.

Moyoni mwangu nafikiri sana nionapo marafiki wangu jinsi walivyo salitiwa na wapenzi wao.

Nauliza nyinyi mlio oa na kupata wake wema mlifanyaje mpaka mkawapata hao maana ninampango wa kutafuta mke.

mwanamke umleavyo, ndivyo akuavyo!
 
cha kufanya umwombe Mungu naye atakuonesha hy
mke mwema kwani kwa magoti na maombi yako utampata
kwani Mungu anaweza agiza toka mashariki/magharibi
na akaja kwako cha kufanya kuomba na kuendelea
kusubiri mpaka mwisho wa dahari

Katika nyakati zetu za sasa ni vigumu sana kumpata mwanamke aliye mwema.

Moyoni mwangu nafikiri sana nionapo marafiki wangu jinsi walivyo salitiwa na wapenzi wao.

Nauliza nyinyi mlio oa na kupata wake wema mlifanyaje mpaka mkawapata hao maana ninampango wa kutafuta mke.
 
usisumbuke, sie tushaisha mwaya, usitafute mfanye huyo uliyenaye awe mwema kwako na mbele za Mungu
 
Katika nyakati zetu za sasa ni vigumu sana kumpata mwanamke aliye mwema.

Moyoni mwangu nafikiri sana nionapo marafiki wangu jinsi walivyo salitiwa na wapenzi wao.

Nauliza nyinyi mlio oa na kupata wake wema mlifanyaje mpaka mkawapata hao maana ninampango wa kutafuta mke.

Sasa hivi unaye yule ambaye si mwema au?
 
Ngoja nimsaidie kumjibia swali mtoa mada kasema hivi bado hajaoa kwa sasa .

Kichwa cha habari kinasema "sijui lini nitapata mke mwema". Maana yake ni kwamba hata sasa hivi anaye mke ila si mke mwema.
 
wanadamu tunafanya mengi kwa kutumia juhudi na akili zetu tukidhan kuwa ndo pekee za kutufanikisha lakini katika mambo tukimtanguliza Mungu ili afanye kile ambacho kinatufaa hakika hatuwezi kuhangaika. Sema wakati sie wanadamu tunafanya yetu na inapofika mahali mambo yanagoma ndo tunakumbuka kuwa Mungu yupo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom