neema pita
Member
- Apr 26, 2012
- 30
- 6
Nina miezi 3 tangu nimejifungua.
Mzazi mwenzangu tulipanga kuona baada ya ujauzito akaniambia nitoe nikakataa basi tukarumbana tukawa tumekosana.
Nimekaa nyumbani na ujauzito nyumbani nikaambiwa niende kwa alienipa huo ujauzito nikaenda kwa nguvu japo jamaa hakutaka alinipikea tumekaa.
Simu yake na yangu zinafanana zote ni tecno m3
Kuna siku nikashika yake kwa kutokujua nikadhani yangu.
Alinitukana sana na kuniambia hanipendi ana mtu anaempenda sio mimi nisimng'ang'anie hanitaki kabisa basi nikaamua kuondoka nikamweleza mama ukweli basi akasema huwezi mlazimisha mtu kama hakutaki.
Nilipokaribia kujifungua nikamuomba hela akaninyima.
Sikuchoka nilipojifungua nikamtaarifu nikamtumia na picha ya mtoto hata hongera hakunipa aliulizia jinsia tu nilivyomwambia kakaa kimya.
Sasa kilichonifanya nije kwenu.
Mtoto anamiezi 3 kipindi chote hatukua na mawasiliano cha ajabu wiki sasa ananiambia niende kwake nikamsalimie kaniuliza na mpenda nikajibu ndio.
Anataka niende sijui nia yake nini mama kasema kama anakutaka aje hapa nyumbani sababu alikutelekeza bila msaada wowote umezaa hajaja hata kumuoba mtoto iweje leo akuite uende? nimemwambia aje kakataa siwezi kuja huko kwenu wewe njoo.
Sielewi lengo lake nini je kwa nini akatae kuja nyumbani au anataka kuniumiza tena kwani nilishaanza kuzoea japo nampenda sana sijui nifanye nini? sijui nia yake nini juu yangu