flulanga
JF-Expert Member
- Jul 1, 2016
- 4,861
- 6,343
Nina kawaida kila mshahara ukiingia sitoi pesa bank mpaka tarehe 01 ndio naenda kutoa pesa yoteee yaani haijalishi mshahara umeingia tarehe ngapi, hata ukiwahi tarehe 22 sitoi pesa bank mpaka ikifika tarehe 01 ndio natoa.
Sasa tarehe 01 mwezi huu nikaenda kutoa pesa yoteee nikafanya maemezi yangu ya nyumbani kwangu nikabakiwa na kama laki 3 na 80 hii ndio nikaweka kwenye pochi. Matumizi madogo madogo nikawa nanyogoa kwenye pochi katika hiyo laki 3 na 80 na kwa hesabu zangu labda tokea hiyo tarehe 01 mpaka jana labda ningekuwa nimetumia elfu 80 kwahiyo nikawa najua kwenye pochi nitakuwa na laki 3 au ikipungua sana basi laki 2 na 70.
Lahaula nilichokikuta aiseeee nimejikuta kwenye pochi kuna laki 2 na elfu 2 aiseeee nimeumia sanaaaa
Sasa hii laki imeenda wapi? Yaani tokea tarehe 01 mpaka jana niwe nimetumia laki 1 na elfu 80 kweli jamaaniii? Kwahiyo nahii laki 2 mpaka tarehe 31 siitakuwa nayenyewe imeisha jamani eti maana ndio kwanza tupo katikati yamwezi.
Nitajenga kweli kwa hali hiii au ndio nitaishi nyumba yakupanga mpaka watoto wangu wajue mwenye nyumba ndio bibi yao!!!
Ndugu zangu wenye take home yalaki 5 nakidogo kama yangu mnawezaje kuweka akiba? Hali yakuwa mnaishi nyumba yakupanga kodi haizidi elfu 50 namke namtoto mmoja!!!
Kwanza naishi kwakujibana, nyumba naishi local, nakula kawaida sana, hakuna ndugu anayenitegemea, siombwiombwi pesa nandugu maana wengi wanamaisha yakawaida kama yangu, navaa kawaida mimi namke wangu..... Yaani hatuna makuu wote wawili ila sasa kuweka akiba ndio mtihani mzito......
Nipeni mbinu ndugu zangu ningependa niwe naweza kuweka akiba yalaki 2 kila mwezi.