Nilikuwa siamini mapenzi yanauma, leo nimeamini

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
6,805
12,669
Katika maisha yangu, nimewahi penda kwa dhati mara moja tu, mitihani ya maisha na mikosi kwa miaka 3 ikaniandama, kwa kiasi fulani kuna sehemu ilibidi nitumie uongo kuweka mambo sawa. Leo umenigharimu.

Tarehe 01/01/2023 nilikabwa nikaibiwa viatu, pesa na simu ndogo.

Tarehe 02/01/2023 napoteza vyeti vyangu vyote vya taaluma.

Tarehe 03/01/2023 napigiwa simu kuitwa nimepata kazi (faraja inarejea).

Tarehe 05/01/2023 anakuja ndugu yangu japo sio wa damu yeye ndiye aliyenisomesha anaomba nimkope laki 3 sikuwa na hiyo hela wakati huo anaomba nimpeleke hata kwa mtu nimchukulie dhamana, kwakuwa namuamini tunaenda kwa mtu namuwekea dhamana anapewa laki 3 kwa ahadi alipe tarehe 09 siku zimekata hapatikani na amehama nyumba na mji bila kusema nalazimika kulipa Deni.

Tarehe 14/01/2023 Mpenzi ameniblock.

Tarehe 16/01/2023 Naanza kazi kwa Mara ya kwanza Ila napokea ujumbe kuwa mimi na yeye basi na hataki kuniona na kuanzia siku yangu vibaya.

Nakiri wazi nimeachwa na mwanamke wa ndoto zangu, nimeachwa na mpenzi wangu wa kwanza(mwanamke ninayempenda) kwa uzembe wangu mwenyewe.

Sina wa kumlaumu, presha ilishuka nikajisikia kufa kufa (vibaya hakuna maelezo) nimewekewa drip 2 now angalau nimekaa sawa nimepewa ruhusa ya kwenda nyumbani.

Najua una akaunti yako humu, najua utasoma huu ujumbe kwa namna yoyote nimeumiza moyo wako nimekuangusha uliniamini ila sijatimiza wajibu wangu naomba unisamehe "Masai" wewe ni mwanamke wa thamani sana najua pengine haitawezekana hata chembe kurudi kwangu ila naomba tusiwe maadui, nipo kwenye trauma naumia.
 
Tafuta pesa wewe acha kuzubaa...! Pata pesa wewe. Pesa sabuni ya roho, pesa ina amisha mlima... pesa ndio kila kitu hacha kulialia kijana ona una patwa na magonjwa ya watu wazima (ya wastaafu wakati ndio kwanza umeanza kazi)
 
Kuna kanuni moja muhimu hukuwa unaijua, kuwa kwenye mahusiano na usitegemee kuumizwa ni sawa na kuogelea halafu usitegemee kulowa... tunajifunza kutokana na makosa, mshukuru Mungu kwa kukupatia kazi na ufocus na maisha yako kwanza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom