Sijui kwa nini mashirikisho ya soka yanang'an'gania nafasi ya mshindi wa tatu, hii nafasi imepitwa na wakati

HOPEfull

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,730
2,082
Salam wanaspoti.

Jana ilitakiwa iwe fainali ya AFCON 2024 na leo ilikuwa ni sherehe tu ya kushangilia kombe lakini sasa kutokana na kuhangaika na nafasi ya tatu fainali inabidi ichezwe leo.

Timu zimekaa hotelini toka jumatano zinasubiri mechi ya fainali zaidi ya siku tatu hii yote eti kusubiria nafasi ya mshindi was tatu. Kuna haja gani sasa ya kuendelea kuwa na hii nafasi.

Hii nafasi kwanza haina tija wala morali yoyote ya mchezo kwa wachezaji ni mechi ya kupoteza muda na nguvu bure tu.

Timu zilizoingia fainali zimekaa hotelini utafikiri ziko likizo, kwanza hata wachezaji wenyewe watakuwa wamechoka kusubiria.

Mapendekezo yangu ni hivi.

Timu zinazotolewa nusu fainali zipewe zawadi sawa siku hiyohiyo baada ya mechi ya nusu fainali then wawe huru kama wanaweza kutembea au kusubiri fainali.

Dhumuni la mechi ya nusu fainali ni kucheza fainali haya mengine ni kutafuta maokotaokota tu.

Pendekezo la pili ni hili kwamba wachezaji wenye kadi za njano na nyekundu zilizotokana na njano mbili waondolewe makatazo ya kucheza mechi ya fainali. Hii Ni kwa timu zilizoingia fainali.

Yaani kama kuna mchezaji ana makatazo ya kucheza fainali kutokana na kadi za njano au nyekundu iliyotokana na njano basi huyo mchezaji aondolewe hayo makatazo ili aweze kucheza. Kuna wachezaji huwa wanastruggle sana lakini bahati mbaya anafika fainali anakosa mechi ya mwisho kwa adhabu nyepesi. Haya ni mashindano ya kihistoria.

Tunahitaji kuona mechi ya fainali iliyo Bora. Hizo kadi wanazopewa baada ya mashindano huwa zinakufa. Hayo makatazo huwa hayaendelei kwenye mashindano yajayo.

Hapo nimezungumzia adhabu nyepesi za kadi za njano na nyekundu na sio Ile 'straight redi kadi'.

Tusubiri tuone fainali ya leo.😶
 
Jana uwanja ulijaa na vibe lilikuwa kubwa bronze medal Ina maana iendelee kuwepo suala la kadi libaki kama lilivyo ili wachezaji wawe makini haiwezekani umemtendea mwingine kitendo ambacho sio Cha kimichezo halafu final ucheze pay the price of your reckless play
 
Salam wanaspoti.

Jana ilitakiwa iwe fainali ya AFCON 2024 na leo ilikuwa ni sherehe tu ya kushangilia kombe lakini sasa kutokana na kuhangaika na nafasi ya tatu fainali inabidi ichezwe leo.

Timu zimekaa hotelini toka jumatano zinasubiri mechi ya fainali zaidi ya siku tatu hii yote eti kusubiria nafasi ya mshindi was tatu. Kuna haja gani sasa ya kuendelea kuwa na hii nafasi.

Hii nafasi kwanza haina tija wala morali yoyote ya mchezo kwa wachezaji ni mechi ya kupoteza muda na nguvu bure tu.

Timu zilizoingia fainali zimekaa hotelini utafikiri ziko likizo, kwanza hata wachezaji wenyewe watakuwa wamechoka kusubiria.

Mapendekezo yangu ni hivi.

Timu zinazotolewa nusu fainali zipewe zawadi sawa siku hiyohiyo baada ya mechi ya nusu fainali then wawe huru kama wanaweza kutembea au kusubiri fainali.

Dhumuni la mechi ya nusu fainali ni kucheza fainali haya mengine ni kutafuta maokotaokota tu.

Pendekezo la pili ni hili kwamba wachezaji wenye kadi za njano na nyekundu zilizotokana na njano mbili waondolewe makatazo ya kucheza mechi ya fainali. Hii Ni kwa timu zilizoingia fainali.

Yaani kama kuna mchezaji ana makatazo ya kucheza fainali kutokana na kadi za njano au nyekundu iliyotokana na njano basi huyo mchezaji aondolewe hayo makatazo ili aweze kucheza. Kuna wachezaji huwa wanastruggle sana lakini bahati mbaya anafika fainali anakosa mechi ya mwisho kwa adhabu nyepesi. Haya ni mashindano ya kihistoria.

Tunahitaji kuona mechi ya fainali iliyo Bora. Hizo kadi wanazopewa baada ya mashindano huwa zinakufa. Hayo makatazo huwa hayaendelei kwenye mashindano yajayo.

Hapo nimezungumzia adhabu nyepesi za kadi za njano na nyekundu na sio Ile 'straight redi kadi'.

Tusubiri tuone fainali ya leo.😶
Dogo uliishawahi kucheza mpira au unajua mpira wa kubetia tu?
 
Kwaiyo, unataka hayo Mashirika Ya Soka yasiwe na mshindi namba tatu kwenye orodha yao....!

Kifupi Ranking System huitaki...

Basi, hakuna haja ya kuwa na Mashindano kbs...
 
Hebu angalieni kwa makini jamani hi nafasi ipo ipo tu.
 
Kwaiyo, unataka hayo Mashirika Ya Soka yasiwe na mshindi namba tatu kwenye orodha yao....!

Kifupi Ranking System huitaki...

Basi, hakuna haja ya kuwa na Mashindano kbs...
Sio hivo shehe mashindano yawepo ila hi nafasi waiondoe tukitoka kwenye nusu fainali ni moja kwa moja fainali.
 
Back
Top Bottom