Matokeo hasi ya timu za kariakoo kwenye michuano ya kimataifa ikawe Fundisho kwa viongozi wa klabu, wasiendekeze maneno dhidi vitendo.

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,305
12,802
Malengo ya Simba sc kimataifa ni kufika nusu fainali na malengo Yanga Sc kimataifa ni kuingia makundi.

Yanga wametimiza malengo Yao lakini siyo malengo ya kushangilia sana kwa maana Yanga Sc ni timu kongwe, nimetizama mechi za Yanga Sc kimataifa haswa Belouzidad, Al ahly na Medeama, kiukweli timu zetu zinapaswa kukaza misuli ya kichumi na kusajili wachezaji wenye high Quality.

Simba sc bado wanajitafuta kutimiza lengo lao la kufika nusu fainali kimataifa, kiuhalisia ukitazama timu inavyocheza unaona kabisa viongozi wa Simba sc walitumia siasa "maneno dhidi ya vitendo" hata mtu asiyejua mpira hawezi kukubali kuwa kikosi Cha Simba sc ni Cha kufika nusu fainali hakuna/haiwezekani.

Malengo ya kufika nusu fainali/Fainali huambatana na usajili ulio Bora kwa timu kama Mamelodi/Al ahly hawa walisema malengo Yao ni kufika Fainali huwezi kupinga kwa sababu ya usajili wao na maandalizi yanaonekana.

Timu zetu za kariakoo ziache maneno Sasa (maneno dhidi ya vitendo) zijikite katika maandalizi yaliyothabiti huwezi kusema kuwa una malengo ya kucheza Nusu fainali wakati timu yako inaingia kwenye makundi kwa bahati bahati na Tia maji tia maji.

MAONI YANGU: Mpira ni mchezo wa wazi na hauchezwi chumbani Viongozi wa timu za kariakoo huu Ni muda Sasa wa kuacha kudanganya mashabiki Ni muda wa vitendo dhidi ya maneno.

Nawasilisha hoja.
 
Back
Top Bottom