Sijui huyu Mwanamke ni wa aina gani?

Sijui huyu Mwanamke ni wa aina gani?

Mancobra

Member
Joined
May 31, 2021
Posts
54
Reaction score
97
Sijui huyu ni demu wa aina gani? Ipo hivi; one day usiku ilinitafuta namba ngeni kwa sms(ilinitext Mambo), sikutaka kuchelewa nikapiga, najua wanangu wa halotel mnajua wingi wa dakika za halotel kwenda halotel. Basi bana, sauti iliyosikika upande wa pili ilikua ya kike.

Mazungumzo yalikua hivi;
Me: Hlw nani mwenzang
Her: Mim Joan(sio jina lake halisi, natumia kwa mazngira haya ya JF).
Her: Nilitegemea kuongea na rafiki yang wa kike Ila naona Kama nimekosea namba!!?
Me: Ok, haina noma kama umekosea namba, usiku mwema.
Her: Poa.

Nilikata simu nakuendelea na issue zangu. Baadae kidogo Kama dakika tano, demu katuma sms, " samahani kaka unaweza kuwa unamfahamu rafiki yangu(akataja jina ) yupo Arusha?". Nikamjibu mimi sipo Arusha nipo Dar so ntakua simfahamu.

Akaendelea, "ok haina shida ila hii namba yako kuna dada angu yupo Dar alikua anatumia kuwasiliana na mm" nikamjibu, kiukweli hii namba ni yangu toka kitambo, nikaendelea Kwan dada ako anafanya kazi Gani?

Akajibu anafanya kazi bank. Nkamwambia ntakua simfahamu coz kazi zangu hazihusiani na Mambo ya bank. Demu akasema poa nimekuelewa , tukaagana.

Ee bwana ee, kesho asubuhi mida ya saa nne kanitumia sms;

Her: habar za asubuhi bro, jana usiku nilipenda ukarimu wako.
Me: poa, kawaida tu.
Her: yani kutokana na ukarimu wako natamani nikujue, unaitwa nani?
Me: Mancobra(not real name)
Her: naomba tuwe marafiki.
Me: poa.

Baadae demu akaanza kuniuliza maswali Kama askari kanzu, una miaka mingapi, unafanya kazi Gani, wew ni mzaliwa wa Dar?, Kati ya mvua na jua unapenda kipi?, Yani alikua Ana maswali kibao. Ila wadau maswali yake yote nilimpa majibu yanayostahili.

Basi bana, baadae nilivopata muda nkampigia simu, Cha ajabu alionekana kunifahamu kimtindo, nkajua atakua Ni demu anayenifahamu, ckumzingatia saanaa coz kipnd hicho nilikua bize na harakat zangu.

Ilivofika kesho yake, demu kanitafuta kaanza kuniuliza maswali Kama kawaida yake;

Her: Mancobra, una mchumba?
Me: Sina mchumba.
Her: upo kwenye mahusiano ya kimapenzi?
Me: hapana.
Her: ok, naomba tuwe wapenzi

Ee bwana ee, wadau Kama mnavojua vijana wa kiume hatunaga no demu akijileta Ni kama mbuzi kafia kwa muuza supu. Lakni kabla ya kumjibu nkakumbuka cjawahi kumuona huyu demu, kiufupi nilikua cjawahi kukutana nae wala kuona picha yake WhatsApp na isitoshe kwa kipindi chote nilipokua nachat nae alinambia anatumia simu ndogo.

Man cobra baada ya kuwaza hii pisi zjawahi kuiona na isitoshe inaonekana kama inanifahamu hata kabla ya kujifanyisha imekosea namba, nikaona nisiipe jibu la moja kwa moja kwamba nipo tayari kuwa nayo kimahusiano badala yake nikwamwambia, "Joan siwezi kukwambia kwamba nipo tayari au sipo tayari kuwa na wewe kimahusiano coz mpaka saiv cjapata kukufahamu vizuri, yani mimi cjawahi kukuona face to face even picha yako cjawah kuiona, na inaonekana wew unanifahamu kabla, hivyo inakua ngumu mm kukuamin, naomba kabla ya yote tufanye wepesi wa kukutana au nitumie namba yako ya WhatsApp niweze kukufahamu"

Baada ya kumuambia hvyo demu akajibu the best Ni kutuma namba ya WhatsApp halaf kukutana Ni baadae. Nkasema poa, baada ya kutuma namba, demu akanambia kwa sasa Hana bando hvyo kuona picha zake nisubiri baadae kidogo (alinambia picha atatuma jion), nkamkubalia.

Lakini Kama ilivyo kawaida yake alinikomalia nimpe jibu kam nipo tayar kua nae kweny mahusiano ya kimapenzi?

Mtoto wa kiume nkaona isiwe shida nkamkubalia. Baada ya kumkubalia alionesha kufurahi Sana alisema " nafurahi Sana kuwa na mtu Kama wew kwny mahusiano mancobra, mm ntakupenda kwa dhati, naomba unipe uhakika kwa upande wako utanipenda kwa dhati?".

Kiukweli wadau, mimi nkamute kwanza, maswali mengi kichwani huyu demu mbona anaingia mzima mzima kwenye mahusiano na wakati huo hataki mimi nimfahamu?

Nkaanza kuwaza, Ni mtego nmewekewa na demu wangu au? Au huyu demu Anatest sexuality yangu? Nkasema anyway, jioni ikifika atakapotuma picha ndo ntajua Kama nimpende au nisimpende.

Mara paaap, jion ikafika, nkamtafuta whatsapp, akawa yupo online nkamtext akaitika, baada ya salamu nkaomba picha.

Sasa hapo ndo yakaanza mapicha picha yenyewe.

Ngoja kwanza ninywe maji baadae ntakuja kumalizia.

(Itaendelea)

Kuendelea kusoma bonyeza link

Sehemu ya pili
 
Umeanza mapicha picha na wewe, tusome kisa hiki kwa week mbili sio?
 
Chai
images%20(10).jpg
 
Wew dogo umefua nguo za kuvaa kesho shule?
 
Back
Top Bottom