Watu hawajui kuwa kitu chochote usipokuwa na nia nacho huwezi kukitengea muda wa kukifanya.
Maelezo ya mkuu
Gobe ukiyasoma katikati ya mistari utaona kuwa kitu anachotaka asaidiwe hakitaki ila anataka kufanya hivyo ili tu kujiridhisha kuwa na yeye ni sawa na vijana wengine.
Kwa umri huo anaona yeye kutokuwa na mpenzi ni habari na kwamba akijulikana atachekwa, kitu ambacho hakina mashiko.
Jiulize kama uliweza kupata ajira ambayo kwa mujibu wako umesema ni nzuri, uliipataje wakati kuna watu wana shahada za uzamili na wanatembea na bahasha kila siku kutafuta kazi ila hawapati?
Nimesema kuwa hicho unachokitaka hukitaki ndio maana hujaamua kukiahangaikia, na ukiona hivyo hakina umuhimu kwako kwa wakati huo. Kwahiyo nakushauri kwa kuwa unajitegemea acha maisha ya kuiga watu, badala ya kutongoza fanya kuchumbia kabisa uoe.
Introvert wengi huwa wagumu kwenye suala la kuanzisha mahusiano yasiyo na future kwa kuhofia kuharibu mipango yao au kukosa sababu ya kuanza kutongozea.
Kutongoza kunahitaji kujitoa ufahamu.