Katika kuishi kwa amani mimi na wake zangu,maana mie nina wake 2 ilibidi kila mmoja nikae nae kutunga kanuni ambazo zinatusaidia sana kuishi kwa amani.Kwa kuwa wake zangu na mimi tunatoka kwenye tamaduni tofauti basi kila mke ana kanuni zake.Mfano kwa mke
wangu mmoja,kuna kanuni hii:
1.Chumbani ni sehemu ya utulivu hivyo wakati wa kulala,kelele haitakiwi,hakuna kuwasha redio,wala tv.Iwapo mmoja wetu anataka kusikiliza redio au kutazama tv basi aende sebuleni.Pia kwa kila mke kuna chumba spea ambacho hutumiwa ama na mimi au mke wangu,ambapo ikitokea tumehitilafiana sana basi ili kuepusha kukuza mgogoro mmoja wetu anahamia kwenye hicho chumba.
Pia tuna kanuni moja ambayo inakataza kugombana mbele ya watoto au wageni.Nikipata nafasi siku moja nitaziandika hapa hizo kanuni.Muhimu ni kwamba tunahitilafiana sana tu lakini hatuzitumii hitilafu hizo kuzua fuji baina yetu