Sijavutiwa na muonekano wake ila anataka kunioa

Mkataa pema pabaya panamuita

Ingekuwa ametafutiwa na mtu au anashinikizwa na ndugu zake ningemwambia usikubali kuolewa lakini katongozwa akakubali kwa sababu mkaka ana pesa basi hana budi kuliendeleza libeneke aolewe laana zingine tunazitafutaga wenyewe

Akijishaua ulomwbia hapo juu atayaona na atalia maisha yake yote
Kabisa mydear atalia sana
 
Habari zenu wapendwa,

Nimekutana na mkaka ambaye tunafahamiana kitambo kidogo kiukweli amejaaliwa mali na ana upendo na mimi na yupo tayari kunioa tatizo sasa linakuja mimi ninachompendea anatabia nzuri ila kama mnavyojua Mungu ametuumba tofauti kila mtu na sura yake na kila mtu macho yake anavyoona hivyo kwenye swala la muonekano kiukweli hajanivutia kabisa yaani daah.

Ila tabia ni njema sana sasa nawaza nikimkubali anioe hivi inawezekana kweli kuja kumpenda huyu mtu baadae nikiwa kwenye ndoa maana wengine wananiambia nitampenda mbele kwa mbele uwezekano huu upo kweli?
Pole sana.
Unanikumbusha kisa cha dada mmoja hivi kinaelekea kufanana na chako. Yy alimpata bwana wa kumuoa ana mali na ni mstaarabu kwa vile yule bwana hakuwa handsome huyo mwanamke alimkataa akidai siyo level yake. Akamfanyia visa vingi sana yule bwana akavumilia baadaye mambo yakamshinda ikibidi yule bwana amuache yule mwanamke.
Siku zikaenda, yule bwana akawa amepata mwanamke mwingine akamuoa na maisha ya ndoa yao ni mazuri na wana watoto 4.
Yule mwanamke katika kutafuta akakutana na ma-handsome, mwanaume wa chaguo lake lkn hakuwa na upendo, hapo hawajaoana wanamegana kisera, usaliti ukazidi ikabidi aachane na huyo handsome wake, akapata mwanaume mwingine wa chaguo lake naye wakawa wanamegana, yule mwanamke kila akigusia suala ndoa jamaa anaruka futi 6, hataki hata kusikia. mwanamke akapata mimba yule handsome akaukataa ujauzito, mwanamke akahangaika kuulea mpaka mtoto akakua, akajaribu bahati yake tena, lkn akaambulia mimba nyingine na tunavyoongea sasa huyu mwanamke ana watoto wa 3 wa baba tofauti na baba zao hawatoi matumizi na wameshaoa na wana watoto na huyu mwanamke hajaolewa mpaka wa leo na umri wa miaka 36.
Je, huyu mwanamke alipata alichokuwa anakitafuta? Leo hii ukimgusia habari za wanaume unamuudhi, anawachukia sana wanaume.
Mdogo wangu usije ukawa km huyu mwanamke mwenye watoto wa 3. Mapenzi ni kamari, ukila usifikiri utakula tena.
Kila lakheri
 
Habari zenu wapendwa,

Nimekutana na mkaka ambaye tunafahamiana kitambo kidogo kiukweli amejaaliwa mali na ana upendo na mimi na yupo tayari kunioa tatizo sasa linakuja mimi ninachompendea anatabia nzuri ila kama mnavyojua Mungu ametuumba tofauti kila mtu na sura yake na kila mtu macho yake anavyoona hivyo kwenye swala la muonekano kiukweli hajanivutia kabisa yaani daah.

Ila tabia ni njema sana sasa nawaza nikimkubali anioe hivi inawezekana kweli kuja kumpenda huyu mtu baadae nikiwa kwenye ndoa maana wengine wananiambia nitampenda mbele kwa mbele uwezekano huu upo kweli?
Si huwa mnasema kikubwa pesa, sura mtavumiliana??
 
Mwanamume ambaye hujampenda na hajakuvutia nae utawezaje kwenda kumtii?

Na usipokuwa tayari kwenda kumtii ni janga umelitafuta kwa ndoa yako.

Usikubali dada haya maisha ni mafupi sana kukubali kuishi hadi kifo na mtu asiyekuvutia kimapenzi.

Tafakari chukua hatua....
 
Hyu dada ananikumbusha wanaume wanaoa mwanamke mwenye makalio au sura, kimoja kikipungua au kupotea mapenzi Yanapungua au kwisha kbs. dada ukipenda ua penda na boga lake.
 
Doooooooh Nenda dada kapate stara yako ukipendwa shikamana ooooohoo.Atakupenda huyo na utasahau hata hao wazuri tena hao ndo wanaume sasa

Mungu hakupi vyote hivyo huyo kapewa mali na upendo kanyimwa vingine nendaaaa tu
Muumbaji ni mmoja

unatufanya wenye mienekano mibou tuhisi ipo siku
 
Habari zenu wapendwa,

Nimekutana na mkaka ambaye tunafahamiana kitambo kidogo kiukweli amejaaliwa mali na ana upendo na mimi na yupo tayari kunioa tatizo sasa linakuja mimi ninachompendea anatabia nzuri ila kama mnavyojua Mungu ametuumba tofauti kila mtu na sura yake na kila mtu macho yake anavyoona hivyo kwenye swala la muonekano kiukweli hajanivutia kabisa yaani daah.

Ila tabia ni njema sana sasa nawaza nikimkubali anioe hivi inawezekana kweli kuja kumpenda huyu mtu baadae nikiwa kwenye ndoa maana wengine wananiambia nitampenda mbele kwa mbele uwezekano huu upo kweli?
Weka picha take tuonee
 
Kwa jins ulivyomuelezea kijana huyo... ni wazi kabisa kuwa hastaili kuwa na mwanamke wa aina yako... na hyo hali ya kusitasita uliyonayo... ni kwa sababu MUNGU ana nia njema ya kumuepusha kijana na balaa litakalomgharimu maisha yake yote.....

Ushauri kwako, achana na huyo jamaa... usubiri ile special order ya kijana wako wa kuchonga kutoka pale veta.
 
Sibora ungeniambia mwenyewe sasa nini kuja kunitangaza uku
 
Habari zenu wapendwa,

Nimekutana na mkaka ambaye tunafahamiana kitambo kidogo kiukweli amejaaliwa mali na ana upendo na mimi na yupo tayari kunioa tatizo sasa linakuja mimi ninachompendea anatabia nzuri ila kama mnavyojua Mungu ametuumba tofauti kila mtu na sura yake na kila mtu macho yake anavyoona hivyo kwenye swala la muonekano kiukweli hajanivutia kabisa yaani daah.

Ila tabia ni njema sana sasa nawaza nikimkubali anioe hivi inawezekana kweli kuja kumpenda huyu mtu baadae nikiwa kwenye ndoa maana wengine wananiambia nitampenda mbele kwa mbele uwezekano huu upo kweli?

ukifata maandiko sawa olewa na mtu ulie mridhia na kumkubali ,ila kwa sasa ivi ilivo dunia sura si roho-ukitaka pesa tafuta yako,ukitaka mtu wa kuishi nae tafuta alie kuridhi na mnae elewana-
 
Ebu elezea muonekane wako kidogo kwamba upoje ili tujifunze,samahani lakini
 
Mhh. Hili ndio tatizo letu baadhi ya wanawake. Ila kabla ya kufanya unayoyataka kuyafanya angalia kwanza umri unaruhusu kuwa na hayo maringo uliyo nayo sababu usije jikuta wakati unafika wa kutaka ndoa na hata wa kukupa habari gani asipatikane.

Pia angalia vile moyo wako unataka.

Na uwache dharau sababu hakuna aliyejiumba.
mfundishe asiact kama viantelope
 
Kwa jins ulivyomuelezea kijana huyo... ni wazi kabisa kuwa hastaili kuwa na mwanamke wa aina yako... na hyo hali ya kusitasita uliyonayo... ni kwa sababu MUNGU ana nia njema ya kumuepusha kijana na balaa litakalomgharimu maisha yake yote.....

Ushauri kwako, achana na huyo jamaa... usubiri ile special order ya kijana wako wa kuchonga kutoka pale veta.
hahahaha kuna watu mnamajibu daaaah...nachekaga sana nkiingia jamii forum
 
Back
Top Bottom