Sijasikia mtu kupinga utabiri wa Sheikh Yahya Hussain | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sijasikia mtu kupinga utabiri wa Sheikh Yahya Hussain

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NgomaNgumu, Feb 25, 2011.

 1. N

  NgomaNgumu Senior Member

  #1
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakati fulani kabla ya uchaguzi wa Tanzania Sheikh Yahya Huussain kwa kutumia ujuzi alionao, alitabiri matukio fulani yaliohusu uchaguzi.

  Kilichotokea ni kua watu wengi walilipokea swala hilo kwa hisia tofauti, lakin idadi kubwa ilikanusha na kubeza utabiri huo. Hili lilonyesha kua waTanzania wengi hawakuzoea kuambiwa wasichokipenda, kitu ambacho ni muhimu kua wakweli kama tunataka maendeleo.

  Cha kushangaza zaid ni habari zilizotolewa na gazeti la Mwananchi leo kuhusu utabiri wamunajimu huyo. Inaonekana kua limewafurahisha watu wengi.
   
 2. Tigga Mumba

  Tigga Mumba JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 747
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Ili iweje? Kwani yeye ndiye anatuongoza au kuamua? Katoa uaguzi wake shauri yake,,, asijifanye sasa anakuwa mnajimu wakati anaona upepo unapokwenda
   
 3. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,515
  Likes Received: 1,686
  Trophy Points: 280
  Wamefurahishwa na nini?? Huwezi jua labda wamekosa 500 ya kununua gazeti, labda umeme ulikatika asubuhi hawakuweza kusikiliza habari za magazetini, labda betri za redio zimeisha na uwezo wa kununua nyingine hawana na jana walisahau kuanika juani, labda wameshamdharau maana ni ujinga kutumia maelezo ya mchawi, mshirikina, mfuga majini na maruhani kufanyia maamuzi!

  Achana na Yahya wewe..fanya kazi zako
   
 4. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,555
  Likes Received: 4,683
  Trophy Points: 280
  Sheikh Yahya anabahatisha tu, anaangalia hali halisi ilivyo then anaitolea maoni binafsi, kwa mtu yoyote asiye mshabiki anaweza kubashiri kuwa kama hali ya ugumu wa maisha, ufisadi uliokithiri na kiburi cha watawala, ikiendelea hivi hivi itafika kikomo cha uvumilivu na lolote linaweza kutokea.Utambuzi huu hauhitaji elimu ya unajimu au utaalamu wa kufuga majini.
   
 5. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  mwaka 2005 alisema uchaguzi wa mwaka huo utamwingiza mwanamke katika nafasi ya urais!
  Mwaka 2010 akasema atakayempinga JK atakufa!
  .....changanya na ya kwako
   
 6. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Duhh! Nakubaliana na mtoa mada. Aliposema kuna mgombea urais atakufa basi watu walipinga na kuomba sana nikiwemo mie binafsi. Ila utabiri huu wa sasa naona kama umekaribishwa na wengi na hii inaonesha dhairi kuwa watu wameuchoka utawala wa Kikwete.
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Hivi 'ametabiri' nini tena?
   
 8. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  ..Eti machafuko yatatokea nchini na serikali itasambaratishwa kwa nguvu ya uma.
   
 9. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Huwezi kumpinga kwa kuwa yeye anatumia nguvu za giza na wengi wetu tunatumia nguvu za Mungu kupambanua mambo,hatufanani wala hatuendani,ukitaka kupinga kitu ni sharti uwe unakijua undani wake.
   
 10. cream.b

  cream.b Member

  #10
  Feb 25, 2011
  Joined: Apr 17, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  freud tu huyo anatabiri vitu ambavyo tunaona vinatokea ndio anakuja kutabiri ....let him be like nastrodamus tabiri vitu 5 to 10 years or longer si vya sasa freud tuuuu
   
 11. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #11
  Feb 25, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hakuna utabiri hapo sema tu anasoma mwendo wa upepo kama mtu yeyote. Pia analazimika kuedit tabiri zake ili ziendane na current forces ya nguvu ya umma lasivyo historia itamuabisha
   
 12. Mkubwa ndevu

  Mkubwa ndevu JF-Expert Member

  #12
  Feb 25, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Huyu mzee mwongo coz aliposema anayempinga jk atakufa bt hakufa m2 akajitetea eti kifo cha kocha mziray kimeingilia nyota Peter mziray wa PPT maendeleo
   
 13. N

  NgomaNgumu Senior Member

  #13
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nilichokikusudia wakati ninaanzisha mada hii ni kujaribu kushauri wazalendo kua wanapo jadili mambo kwa maslahi ya taifa, wajaribu kuepuka ushabiki. Kwani ushabiki ni moja ya sababu inayomfanya mtu asiwe na fikira sahihi.

  Kama tunataka maendeleo ya kweli ni lazima tukubali kukosolewa pale ambapo tumekosea. Kinachosikitisha sana ni kumuona mtu anashabikiwa kitu ambacho kikowazi kabisa kua ni makosa kwa sababu tu kinapingana na itikadi za chama anachokishabikia.

  "Chukua elimu hata kama inatoka kwa mwendawazimu"
   
 14. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #14
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tulishakataaa ujadili mambo ya mashetani; hayo ni maoni yake tu kama mchawi sawa na wachawi wengine walio karibu na serikali wala hayana uhusiano na maendeleo ya sasa ya vyama vya upinzani Tanzania; kishaona umaskini umeongezeka akajua cha kusema ni nini
   
 15. a

  abduel paul Senior Member

  #15
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NILIKUA NAFUTATILIA KWA KARIBU KIDOGO SISI WATANZANIA TUNA MTAZAMO GANI KATIKA MAMBO HAYA YA KISHIRIKINA, HIVI KARIBUNI NILIDHANI UTANI LKN NAONA LINA PAMBA MOTO NA SIELEWI SAWASAWA HETI CLOUDS WANATAFUTA MGANGA WA KUTIBU MVUA, TENA SWALA HILI LINAWACHUKULIA MUDA KABISA HEWANI PASIPO HATA KUJUA SASA WANADHOOFISHA HESHIMA YA KIPINDI CHAO KWA KU PROMOTE USHIRIKINA, HAYA WAKIUWAWA ALBINO TUMSHIKE NANI???? HAWA NAO NI WASHIRIKI, MI NASEMAJE, WAMILIKI WA MAGAZETI NI HATARI SOMETIMES, wanaweza kuilewesha jamii ujinga wa hali ya juu sana kwani wakati mwingine wanakusudia tu kufanya biashara ktk magazeti yao pasipo kuangalia impact ya yale wanayo toa magazetini, Embu nitoe mfano....!! hivi unajua kama sheghe Yahya au mchawi yoyote akatabiri jambo nalo likawa na gazeti lika muanika....!! unajua ni kwa kiasi gani gazeti hili litakuwa lime promote ule uchawi...? HII NI HATARI SANA
   
 16. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #16
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Suala la watu kudai haki si utabiri, maana ni matukio yanayotokea duniani kwa takribani miezi kadhaa sasa hususani eneo la Afrika ya kaskazini na mashariki ya kati, sasa huo unakuwaje ni utabiri wakati haya matukio yameshatokea???
  Mwaka jana Sheikh Yahaya alidanganya watu kuwa uchaguzi mkuu usingefanyika kwa kuwa mmoja wa wagombea angekufa, kitu ambacho hakikutimia!!1
  Hakuna lolote hapo Sheikh, wapumbaze haohao uliowashikia akili
   
 17. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #17
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  huyu Sheikh hana lolote, anasubiri kuona upepo unapokwenda ndo anatabiri,kama hivi keshaona machafuko sehemu mbalimbali duniani na kupinduliwa kwa serikali na yeye anajifanya katabiiiiiriii kumbe watu tu tumechoka.Sheikh jaribu tena badae not now
   
 18. a

  abduel paul Senior Member

  #18
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Brother Mallaba!! hivi unajua huyu jamaa ataendeleza vimbwanga vyake kwa muda mrefu kwasababu anapewa airtime, yaani anarushwa hewani, na kwasababu hiyo sidhani kama kuna taasisi unayo fanya tathmini ya watu wangapi wana athirika na tabiri zake, mi nadhani huyu jamaa ni mmoja wa wale walio changia hata idadi ya wapiga kura kupungua kwani wengi wa waTZ ni maskini na ni washirikina kwasababu wanamwamini ndo mana anapewa nafasi magazetini, asiye msirikina ashirikiani naye kama unabisha sema....!! vyombo vya habari navyo kama hilo gazeti na Clouds nao WASHIRIKINA TENA HAWA NI WASHIRIKINA WA MCHANA KWAUPEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!! OHHHHHH MUNGU wa Ibrahim, Isaac na Yakobo tusaidie.
   
 19. a

  abduel paul Senior Member

  #19
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini kiongozi, embu ngoja kwanza............!!!!!!!!!! hivi kweli ulikuwa unategemea kuna mtu atapinga au na wewe ni Mshiriki??? maana kilo chombo kilicho toa habari hizi ni KISHIRIKI, KAMA NAWE UNAUNGANA NAYE NAWE MSHIRIKI, HAKUNA njia bora ya kuepukana na Mshirikina isipokuwa kumuelekea MUNGU pekee, na kutokujihusisha na yale yote ya kishirikina ua mshirikina. kama kupingwa angeanza Rais wako kumpinga kwani huyu mchawi aliwahi kumwambia atamuwekea kinga...!! unless yeye rais wako hakujua kama kuna mtu atamuwekea kinga hapo sawa vinginevyo kama alijua na bado alikubaliana na kinga hiyo basi naye M........................!!!!!!!!!!!!!
   
 20. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #20
  Feb 25, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Huwezi kumpa mtu tahadhari kuwa ukila kupita kiasi, utavimbewa na si ajabu utaharisha, wakati huo mtu huyo tayari anaharisha. Kesho unakuja unaeleza kuwa unatabiri kuwa huyo mtu ataharisha, wakati tayari alishaharisha. Huo si utabiri bali ni uwendawazimu.

  Machafuko yalishatokea Arusha, watu walipoteza maisha yao kwa kiburi cha serikali ya CCM. Juzi tu watu wamepoteza maisha yao Gongo la Mboto kwa sababu ya uzembe wa serikali ya JK na hakuna aliyewajibika. Sasa hayo machafuko yapi tena anayozungumzia? Ningemuelewa kama angesema machafujo yataongezeka kuliko ya sasa.
   
Loading...