Pole sana mkuu.Habari samahani naomba kuuliza kwa mtu anae elewa hili swala kama mtu umeahidiwa mkataba na boss na hataki kutoa mwisho wa siku zaidi ya mwaka hujapewa mkataba na unapewa posho tu napo akijisikia hivi swala kama hili wapi naweza toa lalamiko na nikasaidiwa kisheria.
Ushauri mzuriUshauri wangu...kama unaona wanakuzingua acha kazi ondoka kimya kimya...waachie taasisi yao mkuu utapata matatizo bure na kulogwa kupo..waogope sana watu walioshika position... Ninakwambia nikiwa na uzoefu na hayo mambo.
Ushauri mzuri
Sheria inasema ukifanya kazi mahali kwa muda wa zaidi ya miezi 6 wewe unahesabika ni mwajiriwa.Habari samahani naomba kuuliza kwa mtu anae elewa hili swala kama mtu umeahidiwa mkataba na boss na hataki kutoa mwisho wa siku zaidi ya mwaka hujapewa mkataba na unapewa posho tu napo akijisikia hivi swala kama hili wapi naweza toa lalamiko na nikasaidiwa kisheria.
Sheria inasema ukifanya kazi mahali kwa muda wa zaidi ya miezi 6 wewe unahesabika ni mwajiriwa.
Lakini kabla hujaanzisha kesi inabidi ujipange sana,ninachojua watu kama hao huwa wanajipanga sana hawakurupuki na usikute kuna wenzako kama wewe walijaribu kuanzisha kesi kama wewe wakafeli.
Ni jambo linahitaji busara sana.
wahusika wa kusuluhisha hiyo kesi ni CMA/wizara ya kazi.
Lakini hakikisha kabla hujaenda uwe na vithibitisho kwamba kweli wewe ni mfanyakazi wao na umefanya kazi hapo kwa hiyo miezi 12.
Kama hakuna mkataba wowote uliosaini hakikisha uwe na kitambulisho,kama hauna kitambulisho hakikisha makaratasi ya kuonesha malipo yako ya kila mwezi,ukikosa hivyo basi upate hata daftari la attendance/mahudhurio.
Hivyo ndio vitu utaulizwa ukifika mahakamani na kama hauna hivyo vitu utafeli halafu utabaki na uadui tu,utaishi maisha ya wasiwasi bila mpango.
Jitafakari kwa hilo.
Kwani we we na muajiri wako mlikubaliana nn wakati unaanza kazi? Na je kuna mabadikiko yeyote yamejitokeza baada yako ww kuanza hiyo kazi? Kwa sababu unaweza ukalalamika kumbe mlikubaliana hivyo. Angalia kama unaona unafursa nyingine achana na hiyo kazi, kama huna namna vumilia hadi kieleweke.Habari samahani naomba kuuliza kwa mtu anae elewa hili swala kama mtu umeahidiwa mkataba na boss na hataki kutoa mwisho wa siku zaidi ya mwaka hujapewa mkataba na unapewa posho tu napo akijisikia hivi swala kama hili wapi naweza toa lalamiko na nikasaidiwa kisheria.
Nimeshapata utatuzi wa swala langu ahsante Mtoa mada na Wahanga tupo wengi
Sio kweli. Mkataba unaweza kuwa verbal au written na mojawapo kati ya aina hizo inaweza ikawa express au implied. Kwanza ni kosa kosa kisheria kuwa na mfanyakazi wa aina yoyote bila mkataba. Fika ofisi za kazi popote pale ulipo utasikikilizwa na kuelekezwa cha kufanya.Yupo sawa kabisa boss wako wewe ni kama volunteer hapo kwake. Ukiwa na mkataba ndio unaweza kupata msaada kwa kutokulipwa mshahara miezi nane.