Sijalipwa mshahara miezi 8 na mkataba sipewi napewa posho tu msaada jamani wapi nipeleke malalamiko?

bennykiba

New Member
Nov 24, 2016
4
45
Habari samahani naomba kuuliza kwa mtu anae elewa hili swala kama mtu umeahidiwa mkataba na boss na hataki kutoa mwisho wa siku zaidi ya mwaka hujapewa mkataba na unapewa posho tu napo akijisikia hivi swala kama hili wapi naweza toa lalamiko na nikasaidiwa kisheria.
 
Cvez

JF-Expert Member
May 19, 2018
1,630
2,000
Yupo sawa kabisa boss wako wewe ni kama volunteer hapo kwake. Ukiwa na mkataba ndio unaweza kupata msaada kwa kutokulipwa mshahara miezi nane.
 
Top leader

Senior Member
Aug 20, 2020
145
250
Ninavyojua hata ukipewa mkataba kuna 12 months probation kama kutestiwa yaani mwaka mzima wanaweza iuvunja mkataba kama hautofanya vizuri ila ikipita hyo miezi 12 ndo wao ndo unaweza washtaki according to my employer's contract maana nimeingia kama nisiyekuwa na experience yaani grade 2
 
Dr. Wansegamila

Verified Member
Feb 3, 2012
2,334
2,000
Habari samahani naomba kuuliza kwa mtu anae elewa hili swala kama mtu umeahidiwa mkataba na boss na hataki kutoa mwisho wa siku zaidi ya mwaka hujapewa mkataba na unapewa posho tu napo akijisikia hivi swala kama hili wapi naweza toa lalamiko na nikasaidiwa kisheria.
Pole sana mkuu.

Peleka malalamiko yako kwa time ya usuluhishi migogoro kazini (CMA). Cheki website yao hii hapa Home | Commission for Mediation and Arbitration wametoa maelezo ya namna ya kuwasilisha malalamiko kwao.

Pia, unaweza kuongea kwa simu na mfanyakazi was CMA akakupa ushauri wa nini cha kufanya. Cheki namba zao kwenye hii link Home | Commission for Mediation and Arbitration chagua namba ya ofisi ambayo IPO karibu na wewe kulingana na ulipo. Atakupa ushauri sahihi was nini cha kufanya.

Pole sana once again.

bennykiba
 
bg_dg_dy

JF-Expert Member
Feb 27, 2009
552
500
Hawa wapo wengi mno, CMA wangekuwa wanaweka dawati la siti ambapo wafanyakazi waathirika wanaweza kupeleka maoni yao na kuwachoma waajiri wa aina hii. Taarifa zitengenezewe usiri na naamini wengi watabadilika
 
mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
5,781
2,000
Habari samahani naomba kuuliza kwa mtu anae elewa hili swala kama mtu umeahidiwa mkataba na boss na hataki kutoa mwisho wa siku zaidi ya mwaka hujapewa mkataba na unapewa posho tu napo akijisikia hivi swala kama hili wapi naweza toa lalamiko na nikasaidiwa kisheria.
Sheria inasema ukifanya kazi mahali kwa muda wa zaidi ya miezi 6 wewe unahesabika ni mwajiriwa.
Lakini kabla hujaanzisha kesi inabidi ujipange sana,ninachojua watu kama hao huwa wanajipanga sana hawakurupuki na usikute kuna wenzako kama wewe walijaribu kuanzisha kesi kama wewe wakafeli.
Ni jambo linahitaji busara sana.
wahusika wa kusuluhisha hiyo kesi ni CMA/wizara ya kazi.
Lakini hakikisha kabla hujaenda uwe na vithibitisho kwamba kweli wewe ni mfanyakazi wao na umefanya kazi hapo kwa hiyo miezi 12.
Kama hakuna mkataba wowote uliosaini hakikisha uwe na kitambulisho,kama hauna kitambulisho hakikisha makaratasi ya kuonesha malipo yako ya kila mwezi,ukikosa hivyo basi upate hata daftari la attendance/mahudhurio.
Hivyo ndio vitu utaulizwa ukifika mahakamani na kama hauna hivyo vitu utafeli halafu utabaki na uadui tu,utaishi maisha ya wasiwasi bila mpango.
Jitafakari kwa hilo.
 
Asante mkuu Mekupa japo vigeZo vyote ninavyo hivyo ila kweli busara inahitajika hapo Asante
 
Ba Bii

JF-Expert Member
Jan 22, 2018
203
250
Habari samahani naomba kuuliza kwa mtu anae elewa hili swala kama mtu umeahidiwa mkataba na boss na hataki kutoa mwisho wa siku zaidi ya mwaka hujapewa mkataba na unapewa posho tu napo akijisikia hivi swala kama hili wapi naweza toa lalamiko na nikasaidiwa kisheria.
Kwani we we na muajiri wako mlikubaliana nn wakati unaanza kazi? Na je kuna mabadikiko yeyote yamejitokeza baada yako ww kuanza hiyo kazi? Kwa sababu unaweza ukalalamika kumbe mlikubaliana hivyo. Angalia kama unaona unafursa nyingine achana na hiyo kazi, kama huna namna vumilia hadi kieleweke.

Otherwise pole sana kwa hali unayopitia.
 
rolla

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
2,182
2,000
Yupo sawa kabisa boss wako wewe ni kama volunteer hapo kwake. Ukiwa na mkataba ndio unaweza kupata msaada kwa kutokulipwa mshahara miezi nane.
Sio kweli. Mkataba unaweza kuwa verbal au written na mojawapo kati ya aina hizo inaweza ikawa express au implied. Kwanza ni kosa kosa kisheria kuwa na mfanyakazi wa aina yoyote bila mkataba. Fika ofisi za kazi popote pale ulipo utasikikilizwa na kuelekezwa cha kufanya.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom