Sijalipwa arrears kwa miaka 4 sasa!

mwarain

Member
Feb 12, 2012
56
17
Jamani naomba mawazo yenu. Mimi niliajiriwa 2008 serikalini katika idara ya afya kama mfanyakazi TAMISEMI na nilifanya kazi serikalini kwa muda wa miezi minne ndipo nikaanza kulipwa mshahara. Nilionana na mwajiri wangu ambaye aliniahidi kunilipa malimbikizo yangu (arrears) na nikapewa fomu kuijaza na hadi leo ninapanaoandika hapa sijapewa hiyo hela yangu. Mwajiri wangu anaahidi kuwa mshahara wangu unashughulikiwa na HAZINA hadi leo.
Kwakuwa ni miaka minne sasa sijalipwa haya malimbikizo yangu na wakati huo madai hayo yalikuwa kama shilingi milioni 2 unusu na muda huu ushapita.
Je kuna sheria yeyote inayoniwezesha kudai malimbikizo ya mshahara wangu pamoja na interest?
Nifanyeje niweze kulipwa bila kuzungushwa hivi?
 
Ongeza juhudi za kufanya uuatiliaji kimaandishi na ana kwa ana hasa kwa afisa utumishi...
 
Back
Top Bottom