Brightly
JF-Expert Member
- Apr 28, 2022
- 261
- 353
Habari Wanajf nawasalimu kwa jina la jamhuri wa muungano wa Tanzania?.Bila kupoteza muda nimekuja kwenu ndugu zangu najua humu jf nitapata ushaurii utakaonisaidia maake naamini jf ni kisima Cha maarifa na pia inawezekana nikapata msaada. Mimi naitwa John Nina umri wa miaka 26,mhitimu wa stashahada ya uhandisi ujenzii (ordinary diploma in civil engineering) mwaka 2020 kutoka chuo cha ufundi Arusha. Safari yangu ya elimu ilianza mwaka 2006 ambapo nilianza darasa la kwanza licha ya kwamba shule ambayo nilikuwa nasomaa haikuwa ikifanya vizurii lakini nilikuwa nafanya vizurii masomo yangu ambapo tangia nikiwa la kwanza mpaka nahitimu la saba nilikuwa nakuwa wa kwanza. nilichaguliwa kuingiaa kidato Cha kwanza mwaka 2012 kwa kupata grade A. Nilipoingia kidato Cha kwanza moto wangu ulikuwa ni ule ule niliendelea kuongoza Hadi kidato cha Nne ambapo pia nilifaulu vzr mtihani wa kidato Cha nne na kufanikiwa kuchaguliwa kujiunga Diploma ya civil engineering kwa ufadhili wa serikali. Muda wote huo ndoto yangu kubwa ilikuwa siku moja kuwa mtumishi wa serikali ili niweze kulitumikia taifa langu kwa weledi (nikiwa mdogo pale kijijini nilikuaga naona njisii watumishi wa serikalini wanavyoheshimika).ila mpaka nilipofika saivii ndoto zangu zinaendelea kufifia kwanii nilishafanya saili nyingi bila mafanikio na sina mtu yeyote wa kunishika mkono. Mwaka jana nilijaribu kuomba mkopo ila sikupewa asilimia zote na familia haina uwezo wa kunilipia hela inayobakia,kuhusu kujiajili Sina mtajii,kuhusu makampuni binafsii nimeishafanya ila nilichoka kwa sababu ya kukaa hata miezii mitatu,minne mpaka mitano bila kulipwa chchote.Hivyo basi kwa heshima na taadhima naomba mwenye connection au ushaurii wwote ambao utanifanya kupiga hatua kutoka hapa nilipo.