Mleta mada hii mada ni ubaguzi na ni utoto na ni ajabu kuona africans wanabaguana kwa rangi.
na waliocomment wote inaonyesha wana inferiority complex bila shaka.
Saikolojia ya binadamu mara zote inapoona kitu fulani ambacho kinachukuliwa ni bora na jamii kwa asilimia kubwa lakini yeye kitu hicho hana.
mara zote huishia kuattack hicho kitu ili kionekane au akione kibaya au akichukie ili ajisikie vizuri na kujifariji nafsi yake.
hii ni sign ya mindset changa, utoto, kutojiamini, kutojitambua na inferiority complex ambayo inakuandama hivyo unajaribu kuikataa.
Tabaka la watu wenye asili ya weusi ndio asilimia kubwa wenye hizi tabia na ndio sababu ya matusi na kejeli zote hizi, yote sababu ni inferiority complex na kushindwa kujikubali na kujiamini, kama wewe ni blue au njano basi jikubali ulivyo tu alafu kaa kimya kuliko kutukana wengine na kuwashusha utu ili ujione uko juu. huo ni ujinga uliopitiliza viwango na tabia za kitoto.
mimi naona rangi zote ni sawa na wala sioni rangi nyingine ni bora kuliko nyingine.
Nina asili ya weupe lakini siwezi na sioni sababu ya kumtukana au kumshusha hadhi mtu mwenye asili ya weusi, huo ni utoto kama wa mleta mada.
Kila mtu ajikubali vile alivyo.
kama huwezi kujikubali basi kaa kimya kuliko kutukana wengine ili ujifariji.