Sifa za CCM pekee ambazo vyama vingine hazina

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,600
CCM ni tofauti sana na nyama vingine vya siasa nchini ambavyo vina usajili kamili na wa kudumu chini ya sheria ya vyama. Sifa pekee za CCM zinjidhihirisha wazi wazi katika masuala mazito ya kitaifa yafuatayo:-
  • CCM ni chama pekee chenye azma ya kuhahakikisha kwamba Muungano wa Tanzania na mapinduzi ya Zanzibar vinaheshimiwa , vinalindwa na vinaendelezwa wakati wote.
  • CCM ni chama pekee chenye azma ya kuhakikisha kwamba ardhi inaendelea kuwa rasilimali kuu ya Taifa na inayoendelezwa kwa maslahi ya wananchi wote.
  • CCM ni chama pekee chenye azma ya kutaka kuona Tanzania ni Taifa lenye umoja, amani, utulivu na mshikamamo madhubuti wa kitaifa wakati wote.
  • CCM ni chama pekee chenye amza ya kuhahakisha kwamba utawala wa sheria na utawala vinalindwa na kuendelezwa wakati wote.
  • CCM ni chama pekee chenye azma ya kuhakikisha kwamba watanzania tunajenga maadili na demokrasia ya vyama vingi katika mazingira ya amani yanayokataa siasa za uchochezi, kashfa, uzandiki,ubaguzi wa rangi, ukabila, umajimbo na udini mambo ambayo ni kinyume na haki za binadamu.
Wananchi kuichagua CCM maana yake ni kujihakikishia wao wenyewe kwamba wataendelea kula hayo matunda ya uhuru kwa ukamilifu. Tanzania ni yote sote.
 
Sifa kuu ya ccm ni matumizi ya vyombo vya dola tu. Ni kweli ccm inachaguliwa na wananchi, lakini haichaguliwi na wananchi wengi kwa ridhaa yao.
 
CCM ni tofauti sana na nyama vingine vya siasa nchini ambavyo vina usajili kamili na wa kudumu chini ya sheria ya vyama. Sifa pekee za CCM zinjidhihirisha wazi wazi katika masuala mazito ya kitaifa yafuatayo:- Kwa haraka haraka nakujibu ifuatavyo:
  • CCM ni chama pekee chenye azma ya kuhahakikisha kwamba Muungano wa Tanzania na mapinduzi ya Zanzibar vinaheshimiwa , vinalindwa na vinaendelezwa wakati wote.
Kiswahili kibovu-muungano unaheshimiwa etc sio vinaheshimiwa (kwani vinini hivyo). Tofauti na wengine CCM wanadai wataulinda kwa "NGUVU ZOTE"
  • CCM ni chama pekee chenye azma ya kuhakikisha kwamba ardhi inaendelea kuwa rasilimali kuu ya Taifa na inayoendelezwa kwa maslahi ya wananchi wote.
Hapa unatulisha matango pori. Nitajie chama kikuu chochote ambacho hakiamini kwamba aridhi ni rasilimali kuu ya Taifa. Huna aridhi huna nchi.
  • CCM ni chama pekee chenye azma ya kutaka kuona Tanzania ni Taifa lenye umoja, amani, utulivu na mshikamamo madhubuti wa kitaifa wakati wote.
Uko sawa kwani CCM wana amini kuwa unaweza kuvipata hivyo bila HAKI. Matokeo yake Inabidi watumie vyombo vya dola kuleta "amani, utulivu, na mshikamano". Hata sijui kama tuna mshikamano-watanzania wanapofurahi ndege "yetu" kushikwa jiulize mshikamano uko wapi.
  • CCM ni chama pekee chenye amza ya kuhahakisha kwamba utawala wa sheria na utawala vinalindwa na kuendelezwa wakati wote.
Hapa ndiyo CCM hasa hii ya fulani inapata zero. Wanavunja sio sheria tu hadi katiba wakiamini kuwa vyombo vya dola vitawalinda. Ustaraabu wote wamepoteza hapa.
  • CCM ni chama pekee chenye azma ya kuhakikisha kwamba watanzania tunajenga maadili na demokrasia ya vyama vingi katika mazingira ya amani yanayokataa siasa za uchochezi, kashfa, uzandiki,ubaguzi wa rangi, ukabila, umajimbo na udini mambo ambayo ni kinyume na haki za binadamu.
  • Huu upupu wako tupia mbali kabisa, inaelekea wewe Tanzania unayoishi ni tofauti na ile tuishiyo sisi wengine. CCM ndiyo wanajitoa mahakama ya Africa ili waendeleee kufanya yao. Demokrasia ndio sahau kabisa kuanzia mwenyekiti wenu hadi Lumumba book 7 humu mtandaoni tunajua kipi kinawaendesha-utashi wa mtu binafsi tena mnadiriki kusema demokrasia inachelewesha maendeleo.
Wananchi kuichagua CCM maana yake ni kujihakikishia wao wenyewe kwamba wataendelea kula hayo matunda ya uhuru kwa ukamilifu. Tanzania ni yote sote.

Kuna taxi dreva alisema wanafurahi CCM kushinda kwa sababu moja tu. CCM haijui kushindwa, CCM hawakubali kushindwa, na CCM ikishindwa patachimbika, kwa sababu ndiyo yenye dola CHAMADOLA basi vurugu yake itapelekea kupotea kwa amani.
 
Niliwahi kumsikia wakili msomi Tindu lissu akiutukana Muungano wetu

Ati huyu anataka kugombea u Rais, ama kweli vituko haviishi

Muungano hauna umuhimu huo kwa sasa, labda kama upo kimatambiko.
 
Sifa kubwa kuliko zote kama aliyewahi kutaka Mwanaharakati Huru Kada Cprian Musiba namnukuu " Kuwa Mwanachama wa CCM lazima uwe na PHD ya UNAFIKI" mwisho wa kumnukuu .
 
Sifa kuu ya ccm ni matumizi ya vyombo vya dola tu. Ni kweli ccm inachaguliwa na wananchi, lakini haichaguliwi na wananchi wengi kwa ridhaa yao.
Ukawa/upinzani haujawahi kuwa uwezo na sifa unazotaka kutuaminisha hapa.
 
Kwa hizo kauli mtaendelea kudharauliwa na Wananchi

Kwa taarifa yako hakuna mwananchi anashida na muungano, muungano una maana kwa viongozi wanaofaidika na uwepo wa huo muungano. Kama upo kimatambiko kama ulivyo mwenge wa uhuru hapo ni sawa. Lakini ni jambo lisilo na maana nje ya matambiko.
 
Ipo siku ukirudia akili zako utajua umuhimu wa Muungano

Taja faida zozote za maana ya Muungano na hasara zitakazopatikana iwapo muungano utakufa. Huo muungano ulikuwa na maana kwa mbali wakati wa vita baridi kati ya USSR na USA kuhusu usalama. Sioni sifa yoyote ya ziada nje ya matambiko, kama tambiko la mwenye wa uhuru. Sana sana wanaoona faida ya huu muungano ni wazanzibari kwani wanaweza kuja kumiliki ardhi huku bara.
 
Kwa mfano mlioonyesha kwenye uchaguzi huu wa chama chenu chadomo wa ngazi mbalimbali ,mkikabidhiwa dola ni zaidi ya janjaweed,bora kife kibudu tu
Sifa kuu ya ccm ni matumizi ya vyombo vya dola tu. Ni kweli ccm inachaguliwa na wananchi, lakini haichaguliwi na wananchi wengi kwa ridhaa yao.
 
Sifa kuu ya CCM ambayo vyama vingine having ni kwamba kinalindwa na vyombo vya dola. Ukikiacha peke take ni chepesi kuliko hewa. Period!
 
CCM ni tofauti sana na nyama vingine vya siasa nchini ambavyo vina usajili kamili na wa kudumu chini ya sheria ya vyama. Sifa pekee za CCM zinjidhihirisha wazi wazi katika masuala mazito ya kitaifa yafuatayo:-
  • CCM ni chama pekee chenye azma ya kuhahakikisha kwamba Muungano wa Tanzania na mapinduzi ya Zanzibar vinaheshimiwa , vinalindwa na vinaendelezwa wakati wote.
  • CCM ni chama pekee chenye azma ya kuhakikisha kwamba ardhi inaendelea kuwa rasilimali kuu ya Taifa na inayoendelezwa kwa maslahi ya wananchi wote.
  • CCM ni chama pekee chenye azma ya kutaka kuona Tanzania ni Taifa lenye umoja, amani, utulivu na mshikamamo madhubuti wa kitaifa wakati wote.
  • CCM ni chama pekee chenye amza ya kuhahakisha kwamba utawala wa sheria na utawala vinalindwa na kuendelezwa wakati wote.
  • CCM ni chama pekee chenye azma ya kuhakikisha kwamba watanzania tunajenga maadili na demokrasia ya vyama vingi katika mazingira ya amani yanayokataa siasa za uchochezi, kashfa, uzandiki,ubaguzi wa rangi, ukabila, umajimbo na udini mambo ambayo ni kinyume na haki za binadamu.
Wananchi kuichagua CCM maana yake ni kujihakikishia wao wenyewe kwamba wataendelea kula hayo matunda ya uhuru kwa ukamilifu. Tanzania ni yote sote.
Vilaza wa CCM mnatia kinyaa.
Muungano wa Tanzania na Zanzibar ndio upi huo!!??
 
Back
Top Bottom