CCM ni tofauti sana na nyama vingine vya siasa nchini ambavyo vina usajili kamili na wa kudumu chini ya sheria ya vyama. Sifa pekee za CCM zinjidhihirisha wazi wazi katika masuala mazito ya kitaifa yafuatayo:-
Kwa haraka haraka nakujibu ifuatavyo:
- CCM ni chama pekee chenye azma ya kuhahakikisha kwamba Muungano wa Tanzania na mapinduzi ya Zanzibar vinaheshimiwa , vinalindwa na vinaendelezwa wakati wote.
Kiswahili kibovu-muungano unaheshimiwa etc sio vinaheshimiwa (kwani vinini hivyo). Tofauti na wengine CCM wanadai wataulinda kwa "NGUVU ZOTE"
- CCM ni chama pekee chenye azma ya kuhakikisha kwamba ardhi inaendelea kuwa rasilimali kuu ya Taifa na inayoendelezwa kwa maslahi ya wananchi wote.
Hapa unatulisha matango pori. Nitajie chama kikuu chochote ambacho hakiamini kwamba aridhi ni rasilimali kuu ya Taifa. Huna aridhi huna nchi.
- CCM ni chama pekee chenye azma ya kutaka kuona Tanzania ni Taifa lenye umoja, amani, utulivu na mshikamamo madhubuti wa kitaifa wakati wote.
Uko sawa kwani CCM wana amini kuwa unaweza kuvipata hivyo bila HAKI. Matokeo yake Inabidi watumie vyombo vya dola kuleta "amani, utulivu, na mshikamano". Hata sijui kama tuna mshikamano-watanzania wanapofurahi ndege "yetu" kushikwa jiulize mshikamano uko wapi.
- CCM ni chama pekee chenye amza ya kuhahakisha kwamba utawala wa sheria na utawala vinalindwa na kuendelezwa wakati wote.
Hapa ndiyo CCM hasa hii ya fulani inapata zero. Wanavunja sio sheria tu hadi katiba wakiamini kuwa vyombo vya dola vitawalinda. Ustaraabu wote wamepoteza hapa.
- CCM ni chama pekee chenye azma ya kuhakikisha kwamba watanzania tunajenga maadili na demokrasia ya vyama vingi katika mazingira ya amani yanayokataa siasa za uchochezi, kashfa, uzandiki,ubaguzi wa rangi, ukabila, umajimbo na udini mambo ambayo ni kinyume na haki za binadamu.
- Huu upupu wako tupia mbali kabisa, inaelekea wewe Tanzania unayoishi ni tofauti na ile tuishiyo sisi wengine. CCM ndiyo wanajitoa mahakama ya Africa ili waendeleee kufanya yao. Demokrasia ndio sahau kabisa kuanzia mwenyekiti wenu hadi Lumumba book 7 humu mtandaoni tunajua kipi kinawaendesha-utashi wa mtu binafsi tena mnadiriki kusema demokrasia inachelewesha maendeleo.
Wananchi kuichagua CCM maana yake ni kujihakikishia wao wenyewe kwamba wataendelea kula hayo matunda ya uhuru kwa ukamilifu. Tanzania ni yote sote.
Kuna taxi dreva alisema wanafurahi CCM kushinda kwa sababu moja tu. CCM haijui kushindwa, CCM hawakubali kushindwa, na CCM ikishindwa patachimbika, kwa sababu ndiyo yenye dola CHAMADOLA basi vurugu yake itapelekea kupotea kwa amani.