Sifa, shobo na usharobaro vyamtokea puani mwanafunzi wa UCC Mbezi beach mbele ya wajeda leo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,709
109,144
Ilikuwa ni mida ya saa nane kuelekea saa tisa mchana alasiri ya leo ambapo wapiganaji wetu wanajeshi wa jeshi la ulinzi la Tanzania wakiwa katika mazoezi yao ya nyika au safari ndefu na wakati huo wakiwa wanatoka walikotoka na wanarudi zao kambini Lugalo na Makongo kuendelea na ratiba zao zingine ndipo walipokuwa wanapita kimakundi makundi hapa kilipo chuo cha computer ( kilicho chini ya UDSM ) cha UCC campus ya Mbezi beach hapa Makonde ndiyo katika hali ambayo naiita ni ya kutaka sifa za kijinga kijana mmoja ( mwanafunzi ) huku akiwa amekaa na wenzake akawa anawapiga picha huku akiwarekodi wapiganaji wetu huku akifurahi kama vile anawakejeli na kuwachoresha.

Kilichotokea hapo ni kwamba kijana alikula vibao vya uhakika ambavyo vilimfanya akonde ghafla, kuona haitoshi wakamgaragaza katika matope yaliyopo karibu pale na kuamua kupiga simu kwa mkubwa wao Lugalo ambaye alikuja maeneo ya hapo chuoni kisha wakatokomea na kijana na kilichojiri huko mimi sijui na wala sitaki kujua japo nimeshakihisi nini kilimtokea au kimemtokea.

Wito wangu vijana au wadogo zangu hebu jaribuni basi kujifunza japo kidogo kanuni za hawa wapiganaji wetu na tujitahidi kutumia hizi smartphones zetu kwa umakini mkubwa. Labda kitendo hiki cha wajeda kinaweza kuwa onyo na fundisho kwa wale wengine ambao wamekuwa na tabia za kishobo shobo kama huyu dogo na nashindwa kuelewa mbona watu wote tukiwa tupo maeneo ya kuanzia pale njia panda ya Kawe au daraja lile la Mlalakuwa huwa tunakuwa na nidhamu kubwa na iliyotukuka sasa iweje maeneo mengine huwa hatuheshimu taratibu zao hawa wapiganaji wetu?

Hivi mtu katoka Bagamoyo nyika kwa nyika kwa kutembea na anarudi kambini kujipumzisha tena jua letu hili la Dar likiwa linawachoma halafu wewe kibushuti tu unaleta za kuleta kwanini wasikuzingue? Kwa kiasi fulani nawapongeza wapiganaji wetu ili kuleta nidhamu na kuwa funzo kwa wengine ili jambo hili lisije kujirudia tena.
 
Hahaa du mi nawaogopa sana hawa watu cc........najua atapita tu hapa..
 
Hao madogo hawajitambui wacha washikishwe adabu.

wanadhani watu wanafanya masihara na kuanza kuzizihaki kazi zao! yule dogo kama namwona vile jinsi leo atakavyopata taabu kupata usingizi na hata kama akilala basi ugoko wake wote pamoja na miguu itashinda tu ndani ya ndoo au beseni ili kuichua vizuri kwa mazoezi mateso aliyoyapata.
 
Sijaona kosa la huyo dogo na vile vile hao wanajeshi waache ujinga na nyie mnaoshabikia acheni ujinga kitendo kilichofanyika ni kinyume za haki za binadamu.

Jaribu nawewe na haki zako za binadamu uone,siku izi zipn hadi haki za wanyama,kijeshi ni kosa kupiga picha ukiwa na unifomu za jeshi tena mtaani,au hujui ulitaka azipost kwa mtandao halafu ikuwe noma kwao?.
 
Jaribu nawewe na haki zako za binadamu uone,siku izi zipn hadi haki za wanyama,kijeshi ni kosa kupiga picha ukiwa na unifomu za jeshi tena mtaani,au hujui ulitaka azipost kwa mtandao halafu ikuwe noma kwao?.

Nduguyangu sio wanajeshi tu, hata mimi binafsi sipendi mtu simjui alafu anipige picha, aniipeleka wapi nini maelezo yake huko atakako iweka. Labda iwe nimeshindwa kumdhibiti tu, kama yupo ndani ya uwezo wangu kufa hafi ila chamoto atakiona.
 
Kuna mmoja alipiga picha vifaru wakati vinasafirishwa. Kila alipojieleza kua hakua na nia mbaya ndio nao walikua wanazidisha mateso. walimtoa ngozi ya unyayo na kumpeleka kambini kwenye mchanga. kila kidonda kikipona wanakitibia upya. Bahati yake mjeda mmoja aliyemfahamu vizuri aliwaambia wenzake kwamba ni kijana wa mtaani kwao. Hiyo ni baada ya miezi sio wiki
 
Mi naishi karibu nao karibu, nawaogopa kama kifo.
Leo walikuwa wanatembea tembea maeneo ya huku kote
 
Sijaona kosa la huyo dogo na vile vile hao wanajeshi waache ujinga na nyie mnaoshabikia acheni ujinga kitendo kilichofanyika ni kinyume za haki za binadamu.

Uko sawa kweli wewe? Yaani mafunzo ya kijeshi urekodi yaingie kwenye mtandao ya kijamii? Kumkamata nakumpa adhabu nihaki yake kabisa na usishangae huko alikoenda yakaibuka mengine.kwani aliekamatwa gharisa hakua mwanafunzi? Utachukulia simpo lakini kama nipicha za kijasusi utajuaje?
 
Back
Top Bottom