Siendi tena Karume Soko la Mitumba!

Miguu anayo, macho unayo, akili unayo, kwanini mtu akupeleke peleke!? Sasa sijui ni uvivu au nini!?
 
Zama boutique mwana wane kama pale Jamstore Africa sana,Mwenge nk beba kitu cha ukweli,haina chenga kabisa.
 
Kama ni uamuzi wako ni kwanini utuhusishe na sisi?

Wewe jamaa unahamasisha mgomo eeeh
 
Nakushauri,:Ukitaka vitu vizuri wahi a sub uh I na mapema(huwa naamka SAA 10) ukienda baada ya hapo utaumizwa tu na wajanja wa mjini....Io laki 3 uliyotumia ungerudi na belo zima nyumbaani ....Kuanzia viatu hadi juu...!!usije mjini
 
Tatizo ni moja kataa kushikiwa akili mwenye Maamuzi ni wewe. Ata mtu akwambie neno gani ni wajibu wako kukubali Au kukata. Kwanza MI huwa siwaangalii usoni hata aniambe bro Njoo huku uone Au subiri huwa sifuati Naendelea kuangalia nachotaka Kama hamna naondoka. Ilinipa tabu zamani ila saiv Kama wewe lakini saiv huwa nakwenda straight maeneo nayotaka nikikosa sijui aanze story naondoka hata usoni simwangalii zaidi ya kusema Asante
 
Pole sana.
Mi huwa sipendi ninapokwenda kununua kitu halafu mtu ameanza kunisemeshasemesha eti kunielekeza. Huwa nakuwa mkali kama mbogo na kufoka kwamba niache niwe huru.
Naingia na kutoka kila banda kadiri nitakavyo na nionavyo, sitaki unisifie sijuwi unitafutie.
Natafuta mwenye nikikosa naondoka.

Tatizo letu Waswahili ukishaitwa boss basi unajiachia na kuwapa uhuru wahuni.
 
hawana saikolojia ya juu wala nini ni wewe tu na ufala wako kenge we.
 
Uzuri hawakuibii unatoa kwa hiari yako
.. Tatizo nin sasa?
 
Mimi mwenyewe nilishawahi kununua masuruali ya jeans ya hovyo kabisa. Jeans ambazo sio style yangu kabisa hata kuvaa nikashindwa ikabidi niyagawe tu. Hawa jamaa huwa wanasumbua sana kiasi kwamba wanakipamba kitu mpaka kinaonekana kizuri tofauti na uhalisia wake. Mimi nilishaacha zamani sana kununua nguo za mitumbo. Sasa hivi nikitaka nguo ni kuingia kariakoo tu.
 
wale wanaitwa ma winga hawana meza ya biashara ila wanaishi mjini. wanakuja na nauli tu hapo karume usipokuw makini utazunguka soko lote
 
Tabia hiyo ipo pale Big Brother aisee hata kama hutaki kununua kitu kosa upite mle ndani watakufuata wanakuonyesha vitu ambavyo hujapanga kununua watakwambia njoo uone jeans sijui shati daa yaani ni kero tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…