Uchunjuba Punjubi
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 799
- 624
Hiyo nimeisemea kibinaadamu lazima uwaze hivyo, maana wanahustle sana, ila akili yako inakuwa haiko sawa kwa muda hivi.Kumbe sababu ushaijua tayar "mpaka unaanza kuwaonea huruma kwa jinsi walivyokuhangaikia hivyo usiponunua hata kimoja si itakuwa shida sana? "
HaaahaaaHiyo nimeisemea kibinaadamu lazima uwaze hivyo, maana wanahustle sana, ila akili yako inakuwa haiko sawa kwa muda hivi.
Na kwa taarifa yako katika vitu vyote ulivyonunua kuna "Cha Juu" umewekewa na hao jamaa. Haiwezekani mtu akawa eti anamiliki au yuko share kwenye hayo maduka yote.Wakuu, habari zenu! Huu ni uamuzi wangu ambao nimeamua kuuchukua baada ya kuona napata hasara kila ninapoenda soko la mitumba pale karume, opposite na makao makuu ya TFF pale. Kitu cha kwanza ni ile system yao ukiulizia kitu basi watahakikisha wanakuzungusha karibia soko zima, yaani wanakuweka kwenye chain flan ambayo hutoki( sijui wana dawa wale) utasikia twende huku ukaangalie, kaa hapa tukuletee, vitu usipovipenda utaambiwa subiri tukuangalizie, twende huku, ukiwaambia nimeahirisha hawakuelewi kabisa, ni kama akili yako wanakuwa wameiteka hivi mpaka unaanza kuwaonea huruma kwa jinsi walivyokuhangaikia hivyo usiponunua hata kimoja si itakuwa shida sana? Kingine ni bei zao, wanasaikolojia ya juu sana wale watu, wanakujua kabisa huyu bei zake ni hizi, huyu zile. Kuna siku nimeenda pale nimechoma laki tatu hivi hivi nimekuja kutafakari vitu nilivyonunua hata havieleweki kabisa, mpaka nikawaza hawa jamaa walinipa nini, hivi nilikuwa na akili yangu timamu kweli? Kwa sasa nilichoamua ni kutokwenda kabisa karume, ntakuwa naingia madukani tu au Tandika na sehemu zingine zenye mitumba.
Duh kweli! Nimekumbuka siku moja niliwahi kuulizia kitu, hali ilikuwa hivoNi kweli mkuu karume ukiuliza kitu utazungushwa soko zima na mtu anakuwa na juhufi hachoki mwishowe unaweza kununua hata kitu usicho kikusudia
Hao jamaa japo sijawahi kutana nao ila kwa sifa hizo tunapaswa kuwapongeza mkuu.Shughuli za biashara wanaweza maana wana uwezo wa kumshawishi mteja awaamini na kupenda bidhaa bila kuweka mashaka.Wakuu, habari zenu! Huu ni uamuzi wangu ambao nimeamua kuuchukua baada ya kuona napata hasara kila ninapoenda soko la mitumba pale karume, opposite na makao makuu ya TFF pale. Kitu cha kwanza ni ile system yao ukiulizia kitu basi watahakikisha wanakuzungusha karibia soko zima, yaani wanakuweka kwenye chain flan ambayo hutoki( sijui wana dawa wale) utasikia twende huku ukaangalie, kaa hapa tukuletee, vitu usipovipenda utaambiwa subiri tukuangalizie, twende huku, ukiwaambia nimeahirisha hawakuelewi kabisa, ni kama akili yako wanakuwa wameiteka hivi mpaka unaanza kuwaonea huruma kwa jinsi walivyokuhangaikia hivyo usiponunua hata kimoja si itakuwa shida sana? Kingine ni bei zao, wanasaikolojia ya juu sana wale watu, wanakujua kabisa huyu bei zake ni hizi, huyu zile. Kuna siku nimeenda pale nimechoma laki tatu hivi hivi nimekuja kutafakari vitu nilivyonunua hata havieleweki kabisa, mpaka nikawaza hawa jamaa walinipa nini, hivi nilikuwa na akili yangu timamu kweli? Kwa sasa nilichoamua ni kutokwenda kabisa karume, ntakuwa naingia madukani tu au Tandika na sehemu zingine zenye mitumba.