Sielewi kwanini Maalim Seif ameenda Chato kuonana na Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.
Sikupata jibu na niliwaza sana kilichompeleka Maalim Seif Ikulu kukutana na Magufuli ni nini?..
Anachofanya Maalim Seif ni usaliti machoni mwa mjinga asiyeijua vema katiba ya Zanzibar. Pia ni usaliti machoni mwa nyumbu asiyeikumbuka kauli ya Mbowe mwaka 2015 akibadilisha gia angani kuwa, "siasa haina adui wala rafiki wa kudumu".

Nyumbu buana. Unataka makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar asionane na rais wa nchi! Jinga sana.
 
Sikupata jibu na niliwaza sana kilichompeleka Maalim Seif Ikulu kukutana na Magufuli ni nini?...
Kwenye siasa tumia akiri yako na sio ya mwanasiasa,

Kwa wale waliokufa kwa ujinga basi huko waliko watajutia vifo vyao, ila wale waliokufa kwa kusababishiwa kifo bila sababu basi mungu awalipe uzima wa milele, na wale waliosababisha vifo bila sababu basi adhabu kali waipate hapa duniani na mbinguni pia.

Kwenye siasa mshabiki tumia kichwa na ubongo zaidi kuamua bila kushinikizwa na mhemko.
 
Kwanini aliwasaliti na kuwaingiza watu kwenye vifo wakati akjua ataungana na magu kuliponya Taifa?

Alijua lini na amesaliti watu gani, yuko pale kwa mujibu wa katiba... Wazanzibari timamu wanaitambua!
 
Kuna mambo matatu nataka niweke sawa kumbukumbu ili tuwe pamoja.
  • Kwanza ni msimamo wa CHADEMA na ACT kuwa maridhiano ndio suluhu ya utatuzi wa kisiasa Tanzania. Rejea ujumbe wa Mbowe akiobwa kutoa neno na Magufuli katika shughuli/sherehe za Uhuru 2019. Katika mahojiano ya Lissu na BBC baada ya uchaguzi, aliuzwa - Ukikutana na Magufuli leo unataka kumwambia nini? Alisema, angemshauri kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Hivyo kimsingi vyama vyote viwili vinalengo la maridhiano na serikali iliyopo madarakani. Tatizo ni kuwa wengine wanapata nafasi hiyo na chama kingine bado hakijapata nafasi hiyo.
  • Maalim kwa sasa hivi ni kiongozi wa serikali Zanzibar. Sijui kwanini akatae kukutana na kiongozi yeyote wa serikali iwe ya muungano, bara peke yake au visiwani. Kweli sipati logic katika Thread hii? Kifupi sijaelewa ujumbe unaotaka kuutoa hapa.
  • Unapoingia katika mapambano ya kisiasa ni kwamba kuna idiolojia unayoiamini katika kuleta mabadiliko. Maalim anaweza kupata mkasa wowote (maradhi, uchovu tu wa mapambano au kifo) ule utaomlazimu kuacha siasa, lakini idiolojia iliyokufanya uifuate itabaki pale pale. Hivyo jifunze kufuata idiolojia unayoiamini na si kumuamini mtu vinginevyo hutafika. Maana kama unadhani CCM kamwe haitaweza kuleta mabadiliko ili kuboresha maisha yako, msimamo huo hautabadilika kwa vile Maalim ameacha siasa. Namaliza kusisitiza, amini idiolojia unayoiamini na si mtu/binadabu, utafaulu tu kama upo katika haki.
 
Sikupata jibu na niliwaza sana kilichompeleka Maalim Seif Ikulu kukutana na Magufuli ni nini?

Niliwaza sana, nikamlinganisha kitendo hicho na say, Museveni kukutana na Bobi Wine, his main rival au enzi hizo PW Botha kukutana na Mandela kwa faragha... Watu wasingelielewa..
Alienda hijja chato.
 
Watanzania wengi sasa hivi cannot think logically! Wakati wote tumeona ule uchafuzi wa electuon 2020 unaezaje kusema vyama vya upinzani vinakosea kulaani process nzima unless wewe ni hayawani?

Ila Zanzibar Rais Mwinyi amekuwa na hekima kubwa mno na huwezi kumlaumu Seif kwa kukubali! Ona ccm bara walivyowathreaten wanawake wa Chadema baada ya kuwaibia kuingia tena bungeni kwa kukiuka katiba!! Shame on Ndugai and NECC -ccm
 
Kuna mambo matatu nataka niweke sawa kumbukumbu ili tuwe pamoja.
  • Kwanza ni msimamo wa CHADEMA na ACT kuwa maridhiano ndio suluhu ya utatuzi wa kisiasa Tanzania. Rejea ujumbe wa Mbowe akiobwa kutoa neno na Magufuli katika shughuli/sherehe za Uhuru 2019...
Point: Imani ina maisha marefu kuliko mwanadamu.
 
Hivi ni kwanini mnapenda kusema uongo? 2019 sherehe zilifanyika Mwanza na Mbowe alikuwepo. Acheni tabia ya kuandika uongo uongo.

Aliitwa Mwanza kwenye Sherehe za Uhuru 2019, hakuchomoa


Wanasiasa wa msimamo Bongo washakufa wote…tumebaki na Kaole Group

Bora kumuamini Msanii wa Bongo movie kuliko Mwanasiasa wa Bongo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom