Hii maana yake hasa ni nini? Upinzani Tanzania umekwisha? Chadema walilaumu sana kwanini kipindi kile Maalim alimtafa Magufuli Ikulu na kumsema maalim seif amewasaliti Upinzani, Lakini sasa macho yangu yanashuhudia kile kile kwa Chama cha Demkrasia na Maendeleo - CHADEMA.
Wananchi tupate picha gani kwa viongozi wetu hawa, Je Chadema sasa Wanaitambua Serikali iliyomadarakani Tanzania? Je viongozi wa juu hawa wamefikia bei? tuliambiwa na kuaminishwa Zitto Kabwe ni CCM (B) Je! Chadema wanaenda kuwa CCM (C) ama D? au E? natamani, Hivi kina Halima Mdee na wenzake nao waliwahi mapema zaidi kwenye hili?
Mbowe anatoka jela bila kuona familia yake kwanza anaenda kuonana na Rais Ikulu? Je kuna rushwa ya kisiasa, mbona giza ni nene?
Binafsi niko njia panda., Siioni CCM ikiondoka madarakani naona kama vile nido kwanza wanajichimbia chini zaidi mizizi yao., Tuunge Mkono wapi? Kina James Mbatia na Mrema hao tulijuzwa na kuaminishwa kwamba tayari walishawahi siti za mbele zaidi. Je, Tanzania tunahitaji chama kipya cha Upinzani kukidhi ndoto na dhana ya upinzani?
Naomba majibu wadau wadau wa Ukumbi huu.