Rais Magufuli: Maalim Seif ni Kiongozi kweli, aliacha 'interest' zake na kutanguliza za Wazanzibari

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,648
2,000
Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amempongeza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuwa miongoni mwa walio katika Serikali inayoongozwa na Rais Hussein Mwinyi, akisema uzoefu wake kama Kiongozi ni mkubwa na unahitajika kwenye Uongozi wa sasa.

Akizungumza kutokea Chato Mkoani Geita, Rais Magufuli amesema, katika Umoja wao (Dkt. Mwinyi na Makamu wa Kwanza na wa Pili wa Rais) mwanga wa Maendeleo ya Zanzibar umeanza kuonekana, akisisitiza pia ni Maendeleo ya Tanzania

Amewataka waendelee kufanya kazi akiwahakikishia ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisema hatowaacha kamwe kwasababu wote wanahubiri Amani.

Rais Mwinyi na Maalim Seif wamewasili Wilayani Chato leo kwa ziara ya siku mbili.

1.jpg
2.jpg
3.jpg
4.jpg
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
14,480
2,000
Magufuli "be like" Maalim Seif wewe sina tatizo na wewe, Tundu Lissu sina tatizo kabisa na wewe, chagua tu nipo tayari kukupa CHEO chochote.

Tatizo langu na ninyi ni moja, "Kwanini mnapita pita mitaani mnawaamsha waliolala usingizi wa pono. Hapo ndio tunakosana.

Njooni tule nchiπŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹

Achaneni na hayo majinga yasiyojielewa.

Kuweni "Wazarendo" πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹
 
Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
4,021
2,000
Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amempongeza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuwa miongoni mwa walio katika Serikali inayoongozwa na Rais Hussein Mwinyi, akisema uzoefu wake kama Kiongozi ni mkubwa na unahitajika kwenye Uongozi wa sasa.

Akizungumza kutokea Chato Mkoani Geita, Rais Magufuli amesema, katika Umoja wao (Dkt. Mwinyi na Makamu wa Kwanza na wa Pili wa Rais) mwanga wa Maendeleo ya Zanzibar umeanza kuonekana, akisisitiza pia ni Maendeleo ya Tanzania

Amewataka waendelee kufanya kazi akiwahakikishia ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisema hatowaacha kamwe kwasababu wote wanahubiri Amani.

Rais Mwinyi na Maalim Seif wamewasili Wilayani Chato leo kwa ziara ya siku mbili.

View attachment 1677425

View attachment 1677408

View attachment 1677410

Swali mmoja je walioiba kura nao ni wazalendo? Mbona interest anazosema ni kwa upinzani tu je wanaoiba kura wana interest za nchi au ni kukundi binafsi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom