Siasa za Mbeya 2005-2010

Asubuhi nimesikia kwenye uchambuzi Danny Mwakalinga sijui inakuwaje hapo Masa na Sikonge?

Mkuu, soma maelezo ya Engineer hapo juu. Kama anachosema huyo jamaa ni kweli basi ni vema TUSUBIRI hiyo riport maana hapo hakuna atakayesema KASINGIZIWA. Hivyo wote tuache papara na TUSUBIRI.
 

Hapo ndipo tulipo fikishwa na wahandisi wetu wa habari. Wanajua tunameza kila kitu bila kutafakari hivi kweli inaingia akili mtu aende kumdhuru mbunge kwenye mkutano wake akiwa na wafuasi wake kwa kutumia kisu cha mkunjo? IPP wanaji dhalilisha sana kwa kukumbatia ujinga kama huu.

Yana mwisho haya - Rashid kwenye KULI
 
Habari ya leo kwenye Nipashe inasema kuna message nyingi zenye ujumbe mzito kutoka kwa Vigogo Mbeya zinazoashiria kwamba kijana alikua anafanya kazi maalumu. Zaidi, inasema kwamba kuna fedha hupitia mikoa ya kaskazini (ARSHA ?), lakini zikiwa na chanzo chake nje (?). Naamini kwamba mwandishi hawezi kuandika uongo utakao mletea shida baadaye. Hii ni habari ya kipelelezi, inabidi tuifuatilie. Hivi Kyela kuna chama cha upinzani chenye nguvu? Nadhani ni wakati mzuri Bro. Mwakalinga na Dr. Mwakyembe wakapambanishwa kwa vyama tofauti. hapo tutaona nani ni nani. Vinginevyo tuachieni Kyela yetu ya amani........
 
Mpwa check spelling una maana George?

Una matatizo na George Mwakalinga, hilo tunalijua. Huyo kijana ni Daniel Mwakalinga (Dan) na ndiye alikuwa ana record hiyo public meeting baada ya kutumwa na ndugu zake ili kuweka ushahidi kwasababu Dr. Mwakyembe alikuwa anaropoka majungu mengi sana huko vijijini kwamba Mwakalinga kahongwa milioni 400 na katumwa na mafisadi.

Wakaamua kwamba kama anasema ukweli basi afanye hivyo wakati anakuwa recordrd. Huyo kijana wote pale wanamfahamu maana weekends husimamia kuonyesha mipira kwenye big screen kwenye ukumbi wa Mwakalinga na vijana karibu wote wa Kyela huenda kuangalia mipira hapo.

Waliamua aende mtu ambaye anajulikana ili kusiwe na kisingizio cha kwamba walimtuma mtu kwa siri. Walipomwona wakambeba na mambo mengine ndio kama nilivyoandika hapo juu.

Sasa wamezua lingine wanasema kwenye simu kulikuwa na sms za mawasiliano na vigogo. Ni kigogo gani atawasiliana na huyo kijana?

Pia kitu kingine ambacho NIPASHE wamechemsha ni kwamba hiyo simu ilifikishwa polisi ikiwa imesha battery kwahiyo polisi Kyela walishindwa kusoma kilichoandikwa. Baadaye mwenye simu akaambiwa apeleke charger na RCO akaondoka na simu kwenda Mbeya. Kwahiyo hakuna polisi Kyela aliyesoma hizo sms kinyume na Nipashe wanavyodai.

Waliosoma hizo sms ni hao wapambe wa mheshimiwa pamoja na mheshimiwa mwenyewe.

Wacha tusubiri taarifa na ukweli wote utajulikana tu.
 
Mpwa check spelling una maana George?

Daniel Mwakalinga ni huyo kijana inasemekana alitekwa nyara na Wapambe. Huyu ni MPELELEZI anayetumia vifaa vya kisasa kabisa yaani simu ya ERICSSON (OLD SCHOOL) kwa kurekodi picha na sauti.

Kama angelikuwa Mwakalinga George, angelikuwa na vifaa lattest kutoka China ambavyo hata wapelelezi wa Tanzania hawana na huko ni kifaa cha kawaida kabisaaa watoto wanatumia mitaani.

Hebu cheki hii kalamu. Hii ndiyo walitumia kumrekodi Waziri Masha.

 
Mwakyembe siri yafichuka

Na Mwandishi wetu
5th September 2009


Mtuhumiwa akutwa na ujumbe wa kummaliza kisiasa
Wadaiwa uliandaliwa na vigogo mbalimbali nchini





Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe.

Siku tatu baada ya kutiwa mbaroni, Daniel Mwakalinga, anayeshukiwa kuandaa njama za kumdhuru Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, ujumbe uliokutwa kwenye simu yake unadaiwa kuwahusisha vigogo wa Mkoa wa Mbeya katika maandalizi ya kummaliza kisiasa.

Hatua ya ujumbe mfupi uliokutwa kwenye simu ya mtuhumiwa, unadaiwa kuweka hadharani majina ya vigogo hao wanaohusika na njama hizo ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakituhumiwa kumhujumu kisiasa.

Taarifa za polisi zinadai kuwa ujumbe mbalimbali uliokutwa kwenye simu za mtuhumiwa zilizochukuliwa kwa uchunguzi, zinawahusisha moja kwa moja vigogo kadhaa wa CCM na serikali ya Mkoa wa Mbeya kuhusika na njama hizo.

“Sms (ujumbe) hizi zinathibitisha taarifa ambazo tumekuwa nazo kwa siku nyingi...anahusika na vurugu zote za kisiasa zinazotokea Kyela kwa lengo la kumdhoofisha Dk Mwakyembe,” kilidai chanzo chetu kutoka polisi.

Licha ya chanzo hicho kushindwa kutoa undani wa sms hizo, mmoja wa wasaidizi wa Dk Mwakyembe (jina linahifadhiwa), alidai kuwa aliweza kuona baadhi ya ujumbe huo baada ya kumfikisha mtuhumiwa polisi.

Pia zinaonyesha mtiririko wa fedha kutoka nje ya nchi kupitia moja ya mikoa ya Kaskazini kabla ya kuwafikia walengwa mkoani Mbeya.

Mmoja wa wanaotishiwa ni mwandishi wa habari Richard Kilumbu

Ujumbe mwingi unatoa taarifa kutoka kwa mtu wanayemwita 'mzee' na nyingine zinamtaja kigogo mmoja wa mkoa moja kwa moja.
ambaye anadaiwa kumuunga mkono Dk Mwakyembe.

Taarifa za mtandao huo zinadai, mmoja wa wapambe wa kigogo huyo na wapigadebe wa mwanamtandao anayeishi nje ya nchi, tayari anafanya kampeni kuwania ubunge mwenyewe.

“Hawa na kundi lao wanaendesha kampeni kali vijijini za kujinadi sambamba na kundi la ... kwa Kyela hakuna cha muda rasmi kuanza kampeni maana wote hawa wana baraka zote za kigogo wa Serikali mkoa na CCM,” alidai mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya. Majina na sms hizo kwa sasa tunayahifadhi.

Baadhi ya wananchi waliohojiwa walidai kuwa, hali tete ya kisiasa imesababishwa na uamuzi wa makosa au makusudi kuteua mtu ambaye ana uhasama na mbunge.

Hoja hiyo inaungwa mkono na wazee na vijana na kwamba, lawama zote za kudhurika kwa mbunge wao zitabebwa na serikali.

“Mbona haijafanya hivyo kwa majimbo mengine? Kyela tu! Mbunge wetu kakosea nini?” alihoji Mzee Kandambili Malundi, mkazi wa Ikolo.


Taarifa zilizotufikia jana jioni zilidai kuwa mwandishi wa habari, Richard Kilumbo, tayari amefungua jalada la malalamiko polisi kuhusiana na sms anazopata kutoka wanamtandao hao.

Akizungumzia matukio hayo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi alisema jana jioni kuwa vielelezo vya Mwakalinga vimechukuliwa kwa uchunguzi zaidi.

Nipashe ilitaka kujua iwapo simu ya Mwakalinga nayo inashikiliwa, hivyo RPC Nyombi alikuwa na haya ya kujibu: "Nimekueleza kwamba vielelezo vyote ya mtuhumiwa vinashikiliwa nadhani unaelewa maana ya kusema hivyo."

CHANZO: NIPASHE


Hivi kumbe George Mwakalinga katumwa au anaungwa mkono na Mhe. Mwakipesile? huo si ndo mtandao wa mafisadi?
 

Nyumbu,

Hiyo habari ya NIPASHE leo ni uwongo kwa aslimia zaidi ya 90.

Ni kigogo gani mjinga kiasi hicho atakuwa anamtumia sms kijana mdogo na kibarua tu pale Kyela mjini?

Hakuna sms za aina yoyote kama hizo wanazozisema. Kuna kitu Engineer kaandika hapo juu ambacho ni ukweli. Hiyo simu ilizimika ikiwa mikononi mwa wapambe wa Mwakyembe kabla ya kufika polisi Kyela na mpaka RCO anaichukua hakuna polisi wa Kyela aliyekuwa amesoma sms ndani ya simu hiyo. Alisema ataenda kui charge Mbeya na ndipo angesoma hizo sms. Ukiachia mawasiliano ya kawaida ya Mwakalinga na vijana wake wa Kyela hakuna habari za kigogo yeyote.

Wanachofanya NIPASHE ni mwendelezo wa habari za kupika kama jana walivyosema mheshimiwa alitaka kuchomwa kisu.

Kwa habari hii ya leo Mwakalinga ameshawaambia wanasheria wake Dar kuishitaki IPPMEDIA kwa uzushi na kutaka kuleta machafuko Kyela.

Kuweni na subira na ukweli utajulikana muda sio mrefu.
 

Masatu,
Safari hii mtu lazima AFIKISHWE mahakamani kwa huu upuuzi. Mtu huwezi kuandika UPUPU namna hii. Unatunga uongo na mwisho unaanza kuuamini mwenyewe. Hii inanikumbusha ile kesi ya Omar Mahita alipoita waandishi wa habari na kuonyesha USHAHIDi wa visu vya CUF. Visu vyenyewe kama ushahidi eti vimepakwa rangi ya bendera ya CUF - too low. Na ukweli ukawa kwamba yeye ndiyo alikuwa kinara wa kutuma vijana wake. Si ajabu baadaye Zombe akanogewa na akaendeleza hayo mambo.

Mwisho watasema hicho kisu cha mkunjo kimeletwa kutoka nchi za nje. Ngoja tusubiri riport na kama kweli walimteka na kumpeleka kwa Mbunge basi itabidi Mwakalinga atafute MAWAKILI ili hili swala LIISHE. Na hawa jamaa wa IPPMEDIA itabidi na wao wapandishwe kizimbani vilevile kwa kumpakazia. Nina imani mawakili wengi watataka kuishika hii kesi maana ukishinda against IPPMEDIA, basi chart yako ITAPANDA SANA.
 
Hivi kumbe George Mwakalinga katumwa au anaungwa mkono na Mhe. Mwakipesile? huo si ndo mtandao wa mafisadi?

Mkuu,
Mbona husomi habari? Mwenyewe umetutumia na wala hujasoma? Ovyo kabisaa. Unaweka maswali wakati jibu umeweka mwenyewe?

 
Kyela hii ni aibu sana, imekuwaje tumefikia hapa? Kama kweli mbunge anamteka kijana na kumpeleka nyumbani kwake, hilo litakuwa kosa kubwa sana.

Hii habari iliwekwa hapa Jumatano, watu tukaona majungu mpaka walipotoa Nipashe jana.

Mwakyembe mbona anakuwa na watu wa IPPMEDIA kwenye mikutano yake yote Kyela ikiwemo hii anayofanya sasa. Kama hii habari ni kweli alitaka kuuliwa, iweje hao waandishi wasiitoe habari muhimu kama hii siku hiyo hiyo ya Jumatano au hata Alhamisi?

Nafikiri hili jambo litaishia kuwa kama lile la Iringa tu; watu watageuziana vibao mpaka ukweli wote upotee.

Itabidi RPC awe makini sana maana mwanya wowote Dr. Mwakyembe atautumia.

Kwa taarifa nilizo nazo mimi Dr. kule jimboni ana hali ngumu sana, huenda anaamua kutumia hata njia za ajabu ili aonewe huruma kwamba anaandamwa na mafisadi.
 
Natanguliza shukrani ndugu yangu!

Nitakupa story baadaye kuhusiana na Mayasa niliyekuwa naye Jeshini. Mkuu nimechoka na siasa za bongo hasa ukizingatia yaliyotokea week inayoisha hii.

Kila laheri

Masa

Masa,

Huu wimbo nimeupata ONLINE. Unaweza kuupata kwenye PLAYLIST ya George Mwakalinga kama inavyoonyesha kwenye hiyo site. Wimbo wenyewe ni wa 43 kwenye hiyo GeorgeMwakalinga Playlist. Na ili uuvute inabidi uwe na realplayer program ambayo ni free of charge (i hope unayo). Wakati unapiga ukisogeza alama ya mouse, itatokea symbol ya realplayer na ukibonyeza itakuuza wataka kushusha, hapo wee shusha. Ila itaupeleka kwenye mafaili ya Real player. Anyway na jina itaita George Mwakalinga hapo itabidi ukabadili. Ila mwisho kipande kimekatwa, pole sana. Nikipata mwingine ntakutumia ila kwa leo anzia hapa.

http://www.mixpod.com/playlist/18425796 (wimbo wa 43).

Ukishavuta, sema basi asante kwa George Mwakalinga..... hi hiiiii 🙂

NB: Masa, UJUMBE WANGU NIMEU-EDIT. Ila umeni-quate so badili na wako pia ili usije changanya watu hapa nikawa kama vile nakuchonganisha na watu...... Tupo pamoja.
 
Last edited:


Mpwa Sikonge

Thanks a lot, nitaweka thanks kwa Mtanzania si ana mahusiano na George! Nimeutafuta sana huu wimbo....! Jamaa anakipaji cha kutunga RIP Marijan Rajaabu!

Nitamsupport George kama nilivyosema awali naona hamtaki nielewa, aache kuwa pandikizo la mafisadi jamani....simchukii yeye kama yeye...ni ile tabia aliyoonayo ya kutumika. Mwakalinga come up and stand on ur feet....wacha nifaidi Mayasa.......asante Sikonge na napata shida kusema fisadi George Mwakalinga!

Asante napata Mayasa siku nzima
 
Join Date: Mon Aug 2009
Posts: 11
Thanks: 0
Thanked 5 Times in 4 Posts
Rep Power: 0
MLIKUWA MKISOMA KAMA WAGENI SASA MMEJIUNGA
 


He he heee! Ha ha haa! Bwa ha ha haaaaa!
Ndio maana naipenda JF. The home of great thinkers! Surely, there are some great sinkers!
 
Story za wakati ule za Simba na Yangu kurusha njiwa na wachezaji kuruka ukuta ndio sasa zinatumika kwenye siasa za Bongo. ...no wonder, the country is so poor kwa sababu inaongozwa na story za vijiweni...viongozi wetu wanahitaji TBS....
 
Kama kuna mtu asiyempenda Dr basi huyo ni fisadi au ni sehemu ya mafisadi. Kwa nini bambumbile na wenzako mnataka kuwachonganisha wana Kyela kwa Watanzania wachukiao mafisadi? Kwa TAARIFA YENU Dr akitaka kugongea jimbo lolote Mbeya atapeta kwa kura kama alizozipata Mbowe kwenye mkutano wa jana. Acha uzushi na uchonganishi,wakati Dr akisoma ripoti ya RICHMOND mlikuwa wa kwanza kumpongeza leo kwa sababu ya njaa zenu(kuhongwa na mafisadi) mnamgeuka. Mtakufa na njaa zenu kumbukeni WALIOZOEA VYA KUCHINJA VYA KUNYONGA HAWAWEZI.
 

labda nami niulize ni kibarua gani huyu tena kijana mdogo wa kyela anaweza kuwa na mwakili wake dar akawaambia waishtaki IPPMEDIA?au kuna mwakalinga mwingine yupo nyuma ya huyu mwakalinga kibarua?
vinginevyo naaza kuamini mwakyembe amefanya kazi ya ziada kuleta maendeleo mpaka vibarua wa jimbo lake wana wanasheria wao
big up sana mwakyembe kwa hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…