Siasa ya Ujamaa na kujitegemea bado ni Itikadi ya CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa ya Ujamaa na kujitegemea bado ni Itikadi ya CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgeni wenu, Jan 16, 2012.

 1. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Napenda saana kujua kuhusu siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ni Sera ya CCM au Serikali(hasa katika kipindi hiki cha vyama vingi)na pia naomba kujua kama siasa hii Inatekelezeka,au imebaki kama Kauli mbiu?..
  Nimejaribu kuwauliza wengi(hasa Wazee wastaafu) na wanasema haikuwa Sera ya Chama ila ni Fikra za Mwenyekiti(mwl Nyerere)na C C M yake enzi hizo, na pia Nimepata Jibu la Ajabu kutoka kwa Mzee mmoja hapa Morogoro kuwa Ujamaa ulizaliwa kwa Nyerere ukakulia kwa Mwinyi,ukaugulia kwa Mkapa na Ukafia kwa Kikwete ila Utazikwa na Vyama Vingi..
  Sasa napenda Kujua ni sawa Kuuzika au ifanyike mbinu ya kuufufua?..
  MY take: ni Bora kuacha mabaya ya Serikali zilizopita na Kuchukuwa yaliyoa Mazuri tu kwa Afya ya Taifa,JE ujamaa na kujitegemea ni Kuuchukuwa au Kuuacha? Nategemea mengi toka kwenu...
  Ni mimi Mgeni wenu
   
 2. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Dada angu soma thread halafu rudi tena,pole kwa kuelewa todfauti
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Ujamaa na Kujitegemea ni contradiction.

  Ujamaa maana yake ni kutegemeana. Kujitegemea maana yake ni kutokuwa mjamaa.

  Ukiwa mjamaa huwezi kujitegemea. Ukijitegemea huwezi kuwa mjamaa.

  "Ujamaa na Kujitegemea" ni contradiction, moja ya sababu ulishindwa.
   
 4. T

  TUMY JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli ujamaa uli fail kipindi cha Hayati Baba wa Taifa Mwalimu J.K Nyerere ila kama ni mfuatilia mzuri wa hotuba zake aliwahi kuulizwa swali hilo na Waandishi wa habari na alijibu kwamba " Ujamaa uli fail kwasababu ya baadhi ya washiriki wake kumgeuka, watu ambao alitegemea wangemsapoti walimgeuka, lakini pia Mwalimu alikuwa muwazi alisema kama ujamaa ulikuwa mbaya basi ndani kulikuwa na mazuri pia kwanini yale mazuri yasichukuliwe yakafanyiwa kazi kwa manufaa ya watanzania. Binafsi namuunga mkono kulikuwa na mambo mengi sana mazuri ndani ya mpango huo tatizo ni kwamba watu hawakumuelewa pamoja na tamaa za baadhi ya watu.
   
 5. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Napenda saana kujua kuhusu siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ni Sera ya CCM au Serikali(hasa katika kipindi hiki cha vyama vingi)

  Ipo kwenye katiba ya nchi hivyo basi ni ya serikali sio ya chama japo inaweza kuhusianishwa na chama kwa sababu katiba ilitungwa wakati wa chama kimoja

  na pia naomba kujua kama siasa hii Inatekelezeka,au imebaki kama Kauli mbiu?..

  Inatekelezeka kama kutakuwa na uongozi thabiti/imara ila kwa sasa sio hata kauli mbiu kwasababu imebaki kwenye makaratasi tu

  Nimejaribu kuwauliza wengi(hasa Wazee wastaafu) na wanasema haikuwa Sera ya Chama ila ni Fikra za Mwenyekiti(mwl Nyerere)na C C M yake enzi hizo, na pia Nimepata Jibu la Ajabu kutoka kwa Mzee mmoja hapa Morogoro kuwa Ujamaa ulizaliwa kwa Nyerere ukakulia kwa Mwinyi,ukaugulia kwa Mkapa na Ukafia kwa Kikwete ila Utazikwa na Vyama Vingi..sina maelezo kuhusu hii kauli ya mzee. Sasa napenda Kujua ni sawa Kuuzika au ifanyike mbinu ya kuufufua?..

  sio sawa kinachotakiwa ni kuiboresha mbonaa China wajamaa lakini wanaendelea kwa hiyo commitment ya viongozi katika kutekeleza majukumu inatakiwa

  MY take: ni Bora kuacha mabaya ya Serikali zilizopita na Kuchukuwa yaliyoa Mazuri tu kwa Afya ya Taifa,JE ujamaa na kujitegemea ni Kuuchukuwa au Kuuacha? Nategemea mengi toka kwenu...

  Nikweli ulilolisema tuige mazuri
   
 6. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Nashukuru kwa Majibu ambayo kwa kisi fulani yananifanya nifikirie tena upya
   
 7. mooduke

  mooduke JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Swadakta nafikiri hapo kwenye RED ndipo Mwl N6yerere alikwama, Ujamaa ndio Siasa ya Kweli ya Uchumi inyoweza kuwakomboa Watanzania

  Ahsante Kiranga.


   
 8. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,340
  Trophy Points: 280

  Mkuu Kiranga nimesoma hii post yako zaidi ya mara kumi nikijaribu ku-prove kama hii kitu uliyoandika ni logical "Truth" ama ni "Fallacy"

  Jibu limeniambia ulichoandika ni logical "Truth" kama wazee wetu wangeweza ku-work out hii kitu tangu miaka ile ya 70 tungekuwa mbali!
   
 9. M

  MtuKwao Senior Member

  #9
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 7, 2006
  Messages: 190
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Naomba ni-define Ujamaa upya; kwamba ni: Kujenga uchumi wa nchi kwa kuangalia maslahi ya watu, kwa maana ya maendeleo yanayomlenga mtu. Aina hizi za siasa ni maarufu sana kule Kaskazini mwa Ulaya (Scandia). Kama ni madini basi tuyasimamie kwa manufaa ya wote (nchi) n.k.
  Kujitegemea maanake (maana yangu) NCHI iwe na uwezo wa kujipangia mambo yake na kuyafanikisha kizalendo.

  Kama hayo yanakubalika, basi tunahitaji kuyarudia kwa kasi mpya??
   
 10. F

  FUSO JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,859
  Likes Received: 2,336
  Trophy Points: 280
  sasa mbona hawajatutangazia ili tujue kwamba sasa hivi kila mtu ni kula kwa urefu wa kamba yake na bila mtaji wa akili na pesa basi wafwaaa......ukiwa umesimama wima.
   
 11. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Ujamaa na kujitegemea was out tanzanians choice after independencebut selfishfism policy of nyerere. Ukiangalia sana katika miaka yote ya utawala wa nyerere, utaona alifanyaaa juu chini ili aabudiwe kama mungu na umma wa kitanzania waati anajenga uchumi mbaya sana Tanznaia. alikuwa anaimbiwa kwaya na TOT kuwa yeyey ni mwenye busara, mzuri kifikira, fikira zake zidumu na sahihi, bababmlezi wa umma, kipaji chake kazaliwa nacho, babab mlezi wa taifa na mambo mengi wakati watu mikoani na vijijini wanatembea uchi wa nyama na kero ya kurudia dalasa la saba inawakumba vijana kila kukicha.

  Huyu Nyerere alikuwa katili sana, siasa ya ujamaa na kujitegemea haikuwa kwa ajili ya kujenga uchumi bali ni kujenga jina takatifu la nyrere tuu ingawa alikuwa hastahili. jiulize, kwa nini alitunyima uhuru wa kuona TV na kufaidi mafunzo ya tokanayo na TV kwa miaka 27 ya utawala wake wa kujinjijenga kama mungu mtu? kwa nini alikuwa hataki kujenga shule za secondari mpaka ngazi ya kata kama anavyofanya mkapa na kikwete?

  Mashabiki wake wanamsfifu kuwa kagomboa africa, huo ni upuuzi, alistahili kumgomboa mtanzania kwanza yule aliyekuwa anarudia dalasa la saba mara kumi ili kutafuta elimu ya secondari na wengine kuja mjini kutafuta kazi. Kwa nini aliwaita watu unemployed, eti, wazururulaji badala ya kuwatafutia kazi? Mbona kikwete kawajengea machina comlex badala ya kuwapeleka keko rumande? unaona jinsi julius alivyokuwa katili ili mradi tuu afanywe mungu mtu na baraza la maaskaofu wakatoliki Tanzania?

  Ujamaa na kujitegemea, kwa taarifa yako, ulikuwa ni utumwa ndani ya serikali huru. ona alivyofanya operation vijiji vya ujamaa! , nyerere,halafu aliwarudisha kenya , wale watu waliotaka kumpndua moi mwaka 1982, moi akawauwa wote, kweli hili ni jambo la kumpendeza mungu mpaka aitwe mtakatifu jamani? Mbona hakuwasamehe akina macghee na wenzake , akina member lee, mpaka wakafia Gerezani?

  Ujamaa ulivyomfyanya Nyerere mungu mtu, leo hii, ukitaja mabaya ya nyerere hadharani, utasikia mtu anakutukania baba yako kama vile umekashifu dini yake? wewe soma africa now gazete la mwaka 1985, ambalo nyerere alijifanya kulaani Mkataba wa Mkomato accord, kati ya wakati ulke sauth africa vs msumbiji. Ona jinsi mataifa ya africa yalivyomtukana Nyerere ndipo utajua kuwa huyu mtu hakuwa na jina kama tulivyodanganywa na wapambe wake katika africa. halau anagalia. tulipopigana na Iddi Ammin, nchi zote za OAU, hazikutuunga mkono na vita yetu na Uganda, ingawa Iddi Ammini alituchokoza!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  You too, are a great thinker!
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Jan 17, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Ujamaa na kujitegemea hauna contradiction yoyote.
   
 14. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Haya sasa ni makusudi ya kupotosha!
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Contradict contradiction iliyoonyeshwa hapo juu ili kuonyesha kwamba hamna contradiction.
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Jan 17, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  We've gone through this before. Haven't we?

  Or else itakuwa kama zile ligi za dini zisizo na mwisho!
   
 17. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #17
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Onyesha kupotosha kuko wapi, ama sivyo wewe ndiye utakuwa mpotoshaji.
   
 18. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #18
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Who knows labda this time tunaweza kukubaliana, nikumbushe objection yako ilikuwa nini?
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Jan 17, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kwamba the kujitegemea half of it was about building a nation that is not foreign aid dependent (as it is now) and ujamaa being about living together peacefully despite the differences in our religious convictions, ethnic backgrounds, etc.
   
 20. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #20
  Jan 17, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hii ni Thread nzuri sana hasa kwa wakati huu. Wakati tunapata uhuru 50 years ego ilibidi tuanzishe utamaduni wetu ambao haukufanana na ule wa kikoloni. Kwa hiyo Mw. Nyerere alianzisha mfumo wa ujamaa 1968. Wakati huo walikuwa wasomi wachche sana Tanganyika. Ili kujenga taifa linalo jitegemea Ujamaa ulikuwa ni mwelekeo mzuri kwa wakati ule. Ingawaje nchi ilikuwa maskini hasa baada ya kushuka bei za katani na kahawa ambayo ndiyo mazao mawili ya biashara tuliorithi baada ya uhuru lakini Elimu ilikuwa bure na hata tiba bure. Palikuwa hamna mafisadi. Najuwa wapo msiopenda ujamaa kwa hiyo I am sorry but the truth has to come out.

  Ajili ya muelekeo huu wa kiujamaa, nchi yetu iliwekewa vikwazo vingi vya uchumi na ndiyo vilivyo rudisha nyuma maedeleo. Hivi leo wasomi ni wengi na rasilimali nyingi tunazo lakini hali ya uchumi na maedeleo ni mbaya zaidi kuliko wakati wa ujamaa. Na hii ni kwa sababu wananchi wanahangaika na ukata na hawapati muda wa kutafakari maendeleo ya nchi yao kwa hiyo wanaridhika na repoti wanazopewa na serkali yao. Uki tafakari demogrphicaly uchumi wa nchi na population utaona how much tumerudi nyuma. We will not be able to progress in this condition of apathy.
   
Loading...