TUNTEMEKE
JF-Expert Member
- Jun 15, 2009
- 4,587
- 579
Udom ni janga la taifa,kwa kipindi kirefu tumekuwa tukifuatilia mambo yanavyoendelea chuo kikuu cha Dodoma(udom),kiukweli chuo hiki kimekuwa kikiendesha kibabe,kisiasa na ni chuo pekee Tanzania ambacho hakifuati haki za binadamu wala maazimio ya kimataifa kuhusiana na haki za wanafunzi na wanataaluma.Katika kipindi cha mwaka mmoja chuo kikuu cha dodoma kimewafukuza wanafunzi wasiopungua 800 bila ya kujitetea.Pale college of humanities and social science wanafunzi 511 walisimamishwa masomo tar 13/06/2011 na hadi hii leo vijana hao hawajarudishwa kuendelea na masomo.Tukijaribu kuangalia muda waliokaa vijana hawa nyumbani ni mwingi sana na wengine wamekata tamaa na hawana tena matumaini ya kuendelea kupata haki yao ya kimsingi ya elimu.Wengi wao wamekuwa waangaikaji mitaani na kwa upande wa akina dada wameamua kuolewa au kujiuza.College ya education wanafunzi 89 wametimuliwa,natural science 108 na infomatics ni wanafunz 66.Mzaz usimpeleke mwanao Udom hapafai kabisa.Mateso wanayopata vijana wa Udom muhusika mkuu ni waziri mkuu Pinda,yeye sambamba na mawaziri wake wa elimu bwana shukuru Kawambwa na Waziri wake wa mambo ya ndani kipindi kile Nahodha,walienda pale Udom na kuwadanganya vijana kuhusu tatizo lao la mafunzo kwa vitendo,Kwa pamoja waliahidi course zote zitaenda field na suala hilo lipo ndani ya uwezo wa serikali kwani wao ndio wanyekila kitu.Cha kushangaza suala hili liliwekwa kisiasa zaidi na kiutendaji lilikuwa haliwezekani kwa kile kilichodaiwa kuwa prospectus ya udom 2009-10 ilikuwa haijabainisha jambo hilo.Zikiwa zimebaki siku chache vijana waende field.TCU wanaliwaletea barua wanafunzi wenye matumain makubwa ya kwenda mafunzo kwa vitendo kwa ahadi ya Pinda na mawaziri wake kuwa hakuna atakayeenda field na yeyote anayeona ameonewa basi aende mahakamani.Suala hili lilipokelewa kwa hisia tofauti na kusababisha maandamano na mwisho wa siku Pinda alipokuwa anaitwa kuja kutoa ufafanuzi wa ahadi yake na kauli ya TCU aligoma kufanya hivyo na kuwatoa sadaka watoto wa watu.Hali imekuwa mbaya zaid udom kiasi kwamba kwa hivi sasa mwanafunzi akionekana anatoa mawazo yake kwenye tv au radio hata kama hayahusiani na mambo ya udom basi atatafutwa na kupewa barua ya kusimamishwa chuo.Kuna kijana kasimamishwa kisa alionekana Itv kwenye kipindi cha malumbano ya hoja.Hii ndiyo udom inayoendeshwa kwa itikadi ya siasa na kupoteza future ya vijana.Binafsi mwanangu bora aende diploma ya ualimu kuliko kwenda Udom.Poor Pinda,poor mtoto wa mkulima,poor Udom.Mungu wabariki vijana wa Tanzania.