Siasa ilivyotumika UDOM

zumbemkuu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
10,832
8,623
WADAU HII NILIIPATA KWENYE FACEBOOK, ILIANDIKWA NA MDAU ANAITWA ALEX MUSHI

''JAMANI HAKUNA SIKU NIMEUMIA KAMA LEO. Uwezi amini mdogo wetu wa mwaka wa kwanza, GETRUDE NDIBALEMA alivyochanganywa katika majina ya waliosimamishwa chuo pamoja na wanachama wengine wa CDM. Tangazo lililopo leo katika website ya chuo limeongeza majina ya ...makamanda wa CHADEMA kama ndiyo vinara wa mgomo. Getrude ni kiongozi wa Baraza la Vijana Chadema yaani BAVICHA tawi la UDOM kama viongozi wengine.

(mfano: Bw. SHILINGI- Mwenyekiti CCM (UDOM); Bw. Saidi Saidi -Mwenykiti UVCCM (UDOM); Bw. HOMERA- katibu mwenezi CCM (UDOM) na wengineo wengi) wa CCM tawi UDOM. Kwa taarifa ambazo nimeziona leo tar. 20 th july 2011 GETRUDE ameongezwa kama ni miongoni mwa Vinara wa mgomo.

Kwa masikitiko makubwa najiuliza maswali yanayonifanya nipate uchungu kiasi cha kutokwa na machozi kuwa; Sisi kuwa CDM tumepoteza sifa ya kuwa watanzania wenye uhuru wa kisiasa kama wenzetu (wanafunzi) wa CCM? Nani mtetezi wetu katikati ya uonevu huu? Kuwa CDM ni uaini au Uasi? Au ndo utekelezaji wa agizo la wakuu wa wilaya kuwa " mkianza kuwarudisha anzeni na CCM ,waacheni CDM kwani hawana shukrani wala fadhila? Wito wangu kwa Serikali ni kuliangalia hili kwa umakini zaidi ili kuhakikisha wananchi wote ndani ya nchi yao wanapata haki zao kwa mujibu wa katiba.

Nauomba uongozi wa wa Chuo ufanye maamuzi kwa mujibu wa kanuni na taratibu zilizopo na si kwa shinikizo lolote kutoka kwa wanasiasa wanaowatumia kwani kwa kufanya hivyo machozi ya wasio na hatia yatakuwa juu yao.( NASEMA HAYA KUTOKANA UKWELI KUWA HAKUKUWA NA VIGEZO VYA MOJA KWA MOJA KUWATAMBUA VINARA KAMA MATANGAZO YALIVYODAI KUWA VINARA WATASIMAMISHWA ; PIA CHUO KINAJUA UKWELI WA NANI ALIYEUSABABISHA ULE MGOMO WA UDOM) Napenda kuwaomba wadau wote watakaoguswa na uonevu wa huu ndani ya chuo kikuu cha DODOMA watoe msaada wao.

NI WAZI ITAMBULIKE KUWA SIKU AMBAYO DUNIA ITAKUWA SI MAHALA SALAMA PA KUISHI, HALI HIYO HAITASABABISHWA NA WALE WAOTENDA MAOVU BALI ITASABABISHWA NA WALE WANAOONA MAOVU YAKIFANYIKA WASICHUKUE HATUA. Kutatuo tatizo la UDOM kwa staili hiyo si utatuzi wa kudumu bali ni kuairisha tatizo linalokuwa siku hadi siku''.

myk take___kama hiki ndo kigezo walichotumia basi kuna hatari amani ikavunjika siku sio nyingi.
 
inaonekana nawewe ni mwanafunzi pale udom au ndio wewe alex mushi

usipende kukurupuka dogo, ungesoma ukanyamaza km huna cha kuchangia.
 
hakika kinachoendelea udom ni hatari kwa taifa,asilimia 90 ya wanafunz waliosimamishwa ni wanaharakati cha kushangaza wengine hawakuwa kabisa siku hiyo lakin kwa kuwa ni mwanachadema bas kasimamishwa,watawala wanatengeneza bom ambalo litakuja kuangamiza umoja na aman ya nchi ye2.damu na machoz ya vijana hawa yatawahukumu.wanaudom musikate tamaa mungu yuko nanyi wala hawawez kupoteza ndoto zenu watawachelewesha tu.
 
Kubali ukatae cdm imechangia kuiyumbisha udom. Huo ndio ukweli na utabaki hivyo.
 
Kubali ukatae cdm imechangia kuiyumbisha udom. Huo ndio ukweli na utabaki hivyo.
Nakubaliana na wewe asilimia 100! CDM itaendelea kuiharibu UDOM kwa migomo na fujo kila mara,lema amekua anaenda Udom siku za migomo usiku na kuhamasisha migomo!
 
Kubali ukatae cdm imechangia kuiyumbisha udom. Huo ndio ukweli na utabaki hivyo.
Ebu fafanua hii kauli yako. Sio unatoa kauli ziko hewani hewani kama akili ya bos wako jk(mgonjwa kutoka kuanguka anguka mpaka kusahau sahau hovyo)....
 
Nakubaliana na wewe asilimia 100! CDM itaendelea kuiharibu UDOM kwa migomo na fujo kila mara,lema amekua anaenda Udom siku za migomo usiku na kuhamasisha migomo!

naam! mzee wa posho, kuna siku hizo posho unazolipwa na nape zitafikia ukomo.
 
ishu ni kwamba kuna watz wanakubali kunyonywa na kuonewa ili mradi yeye anaishi sio mbaya kuna wengi hawapendi kunyanyaswa hata kidogo na hili ndo liposana hapa jf kwa hiyo kuhusiana na hawa wahanga wa mgomo udom wasipoteze muda kudai haki kwa mtoa haki wa dunia hii cha msingi ni kujipanga kwenda vyuo vingine kuna vyuo kama 20+..
na kikubwa zaidi freedom is near future..
 
Suluhisho ni kuondoa matawi ya vyama vyuoni kama ilivyo maofisini. Hivi ni nani alirudisha siasa vyuoni ilihali mwanzoni mwa miaka ya 90 ziliondolewa? Na nyie wanafunzi acheni siasa, fanya kilichowapeleka huko, wenzenu walishasoma, lakini nyie wanawachochea mfanye migomo na kusimamishwa au kufuzwa vyuoni. Take care!!
 
hakika kinachoendelea udom ni hatari kwa taifa,asilimia 90 ya wanafunz waliosimamishwa ni wanaharakati cha kushangaza wengine hawakuwa kabisa siku hiyo lakin kwa kuwa ni mwanachadema bas kasimamishwa,watawala wanatengeneza bom ambalo litakuja kuangamiza umoja na aman ya nchi ye2.damu na machoz ya vijana hawa yatawahukumu.wanaudom musikate tamaa mungu yuko nanyi wala hawawez kupoteza ndoto zenu watawachelewesha tu.

ebu nambie nani amefukuzwa bila haki! Nkupe maelezo ya kutosha ushiriki wake kwenye mgomo
 
ishu ni kwamba kuna watz wanakubali kunyonywa na kuonewa ili mradi yeye anaishi sio mbaya kuna wengi hawapendi kunyanyaswa hata kidogo na hili ndo liposana hapa jf kwa hiyo kuhusiana na hawa wahanga wa mgomo udom wasipoteze muda kudai haki kwa mtoa haki wa dunia hii cha msingi ni kujipanga kwenda vyuo vingine kuna vyuo kama 20+..
na kikubwa zaidi freedom is near future..

wakolini walijaribu kila njia kuhakikisha wafanyakazi na wanafunzi hawajihusishi na hawaipingi serikalli ya kikoloni, kumbe ndo walieneza sumu, linalofanyika vyuoni ni bomu litakalowalipukia watawala.

Tanzania ya leo hata ukilalamika kuhusu "UKOSEFU WA UMEME" unaitwa kuwa mfuasi wa CHADEMA! fu*k!

mkuu ukitaka upendwe na watawala sifia kila kitu, looh!
 
waliofukuzwa wote ni haki yao maana ndio vinara wa migomo kwa maslahi ya binafsi nani asiyejua ili wajijenge kisiasa kama alivyofanya MTATIRO kwa kuwa vinara wa mgomo kama wangekuwa wanafukuza CHADEMA mbona HABIB MCHANGE hawajamfukuza? Kina kafurila na wengne? Mbona pia wamewafukuza makada wa CCM wanaojulikana kama THOBIAS MWESIGA?
 
Kubali ukatae cdm imechangia kuiyumbisha udom. Huo ndio ukweli na utabaki hivyo.
Unaumwa ugonjwa ambao tuba yake si kuvaa tshirt, kofia ama chochote kilicho na rangi ya njano ama kijani. Wanachuo hawa walikuwa wanafuatilia haki na ahadi za viongozi wa serikali hii walizotoa kwao na kwa hali ya kawaida wanachuo lazima waende field. Kudai field na faculty requirement ni CHADEMA? Acha uzezeta wewe kama wala na kuvaa kwa kupitia jengo la udom usamehewe. Hawa vijana wanasoma ktk chuo ambacho viongozi wanasema kimejengwa kwa kutumia fedha za umma. Umma ni ccm au ni watanzania CHADEMA being excluded?
 
Back
Top Bottom