SI KWELI Si salama mwanamke kulala na shahawa baada ya tendo?

SI KWELI Si salama mwanamke kulala na shahawa baada ya tendo?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Nimekutana na video ya jamaa anaelezea kuwa si salama kiafya mwanamke kulala na shahawa baada ya tendo. Uhalisia ni upi?

1778133185357.png
 
Tunachokijua
JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa kulala na shahawa hazina madhara zikibaki mwilini au kwenye ngozi.

Mwanamke kwa asili ukeni mwake una asili ya asidi na shahawa za mwanaume zina asili ya Alkali hivyo haitoleta madhara yoyote iwapo mbegu hizo zitakuwa katika eneo hilo.

Changamoto inaweza kutokea iwapo wahusika wana maambukizi ikiwemo mwanaume na hivyo baada ya kujaamiana kama zitabaki kwa muda mrefu zinzaweza kuongeza nafasi ya kusambaza maambukizi hayo kwenda kwa mwanamke.

Kujisafisha ndani ya Uke ni salama?

Dkt. Hillary Kwizi, Daktari bingwa wa wanawake na Afya ya uzazi anaeleza kuwa zipo nadharia zinazoeleza kuwa kusafisha uke kwa ndani kunaweza kuongeza maambukizi. Tovuti ya women health inaeleza kuwa kusafisha ndani ya uke kunaweza kusababisha matatizo mengine ya kiafya ikiwemo kupata ujauzito, maambukizi ya ukeni na magonjwa ya zinaa.

Inaendelea kueleza pia kuwa kujisafisha ndani ya uke baada ya kushiriki teno haikuzuii kupata magonjwa ya zinaa na badala yake unaweza kuondoa bakteria muhimu wanaoweza kukulinda dhidi ya maambukizi, jambo ambalo linaweza kukupekea kupata magonjwa ya zinaa ikiwe virusi vya UKIMWI.

Je, shahawa zinabeba maambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI)?

Tovuti ya Arkansas Urology inabainisha kuwa Shahawa au Manii hazisababishi maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) moja kwa moja. Kinachotokea ni kwamba Kujamiiana kunaweza kuvuruga bakteria wanaolinda mwili au kuongeza usafiri wa bakteria kuelekea kwenye njia ya mkojo, lakini shahawa zenyewe si chanzo cha maambukizi hayo.

Tunaweza kusema kuwa Shahawa ni alkaline (nyuzi za alkali), wakati uke una asidi. Shahawa zinapobaki ukeni, zinapunguza asidi ya asili. Hii inaharibu mazingira ya bakteria wazuri (Lactobacilli) wanaolinda uke, na kuruhusu bakteria wabaya (wanaosababisha UTI na BV) kukua kwa haraka.

Similar Discussions

Back
Top Bottom