Wakuu
Kumekuwa na hii dhana ya muda mrefu kwamba mwanamke akinyonyesha bas maziwa yake yatalegea je uhalisia ni upi?
Kumekuwa na hii dhana ya muda mrefu kwamba mwanamke akinyonyesha bas maziwa yake yatalegea je uhalisia ni upi?
- Tunachokijua
- Machapisho na makala mbalimbali ya kiafya yanaeleza kuwa wanawake wengi wamekuwa na dhana kuwa iwapo watanyonyesha basi kuna uwezekano mkubwa maziwa yao yakaelgea. Rejea hapa, hapa na hapa.
Makala ya UPMC Health Beat iliyopitiwa na Daktari Jocelyn Fitzgerald inaeleza kuwa matiti kulegea ama kudondoka ni jambo la kawaida na wala si la kitiba lakini baadhi ya wanawake wanahofia kunyonyesha wakiamini kuwa matit yao yatadondoka.
Sababu za matiti kudondioka
Matiti kudondoka inaweza kusababishwa na mambo mengine kadhaa kama vile;
- Vinasaba, DNA au asili yako ya kifamilia inachangia kwa kiasi kikubwa kuamua ukubwa wa matiti yako, uimara wa ngozi, na jinsi tishu zako zilivyo tangu unazaliwa.
- Kuwa na matiti makubwa, matiti makubwa yana uzito mkubwa zaidi, jambo linalofanya nguvu ya mvutano wa dunia (gravity) kuvuta na kurefusha mishipa inayoshikilia matiti kwa urahisi zaidi kuliko matiti madogo.
- Kutokufanya mazoezi ya kuimarisha misuli ya juu ya mwili mara kwa mara.
- Kushika mimba zaidi ya mara moja, kila unaposhika mimba, mabadiliko ya homoni hufanya matiti kutanuka na ngozi kuvutika. Mimba zinapokuwa nyingi, ngozi inapoteza uwezo wa kurudi katika hali yake ya kawaida baada ya kujifungua.
- Uvutaji wa sigara, kemikali zilizopo kwenye sigara huharibu protini za collagen na elastin, ambazo ndizo zinazofanya ngozi kuwa ngumu na yenye kunyumbulika. Hii inafanya ngozi kulegea haraka.
- Kuongezeka ama kupungua kwa mwili kwa kiasi kikubwa. Kupata na kupoteza uzito mkubwa mara kwa mara kunavuta ngozi ya matiti (wakati wa kunenepa) na kisha kuiacha ikiwa imelegea na tishu za ndani zikiwa zimepungua (wakati wa kukonda).
- Umri
Tafiti na makala za afya zinaeleza kuwa huwezi kuzuia jambo hili moja kwa moja, ingawa yapo baadhi ya mambo ambayo unaweza kuyafanya ili kupunguza kutokea kwa hali hii. Mambo hayo ni pamoja na;
- Zingatia lishe kwa kula zaidi vyakula kama matunda, mboga za majani, nyama na karanga ili kuwa na uzito wenye afya.
- Achana na uvutaji wa sigara.
- Fanya mazoezi ya mara kwa mara yanayohusisha sehemu ya juu ya mwili wako.
- Vaa sidiria zinazokupa uhuru bila kubana sana.
- Epuka lishe kali sana za kupunguza uzito.
Ushauri wa mtaalamu wa afya
Mtaalamu wa lishe kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili, Edna Kenneth anaeleza kuwa wamama wote wasiwe na hofu kuwa wakinyonyesha matiti yao yatalala na badala yake waendelee kuwanyonyesha watoto ili waendelee kupata vitutubisho.