SI KWELI Kifaa cha Artemiss II chasafirishwa kwa msafara

SI KWELI Kifaa cha Artemiss II chasafirishwa kwa msafara

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu nimekutana na hii video inadaiwa kuwa ni kifaa cha Artemiss II kikisindikizwa na msafara baada ya kutua kutoka mwezini. Uhalisia wake ni upi?

===
Witnessing history Artemis II Orion capsule escorted in a powerful convoy—America’s journey back to the Moon

1776230147810.png

 
Tunachokijua
April 1, 2026 shirika la Anga la Marekani (NASA) lilituma wanaanga wanne Reid Wiseman, Victor Glover, Christina Koch na Victor Glover kwenda mwezini kupitia kwa kutumia kifaa maalum. Ilipofika Aprili 6, 2026 walifanikiwa kwenda Maili 248, 655 nje ya dunia, na hivyo kuvunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa Apollo 13 mwaka 1970.

Ilipofika Aprili 10, 2026 wanaanga hao walifanikiwa kurudi tena duniani baada ya kutua kwenye ufukwe wa San Diego hivyo kuhitimisha safari yao ya takribani siku 10 nje ya dunia, wakiwa wamesafiri takribani Maili 252, 756.

Madai

Kupitia mtandao wa X, mtumiaji mmoja alichapisha video akiambatanisha na ujumbe uliokuwa ukieleza kuwa kifaa kilichotumika katika misheni ya Artemiss II kilikuwa kinasafirishwa kwa msafara baada ya kutoka mwezini

Uhalisia wa madai hayo

Baada ya ufuatiliaji wa kina uliofanywa na JamiiCheck, imeridhisha kuwa video hiyo si halisi. Kwa kutumia Nyenzo za kidigitali imebainika kuwa video hiyo imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde.
1776240755814-png.3573008

Mbali na hayo video hiyo imeonekana kuwa na baadhi ya dosari zinazoonekana ikiwemo watu walioshika simu na kuonekana kurekodi, video zao hazioneshi kama zinarekodi kitu. Vile vile kifaa hicho kimeendelea kuonekana na alama ya NASA pamoja na jina la misheni hiyo ambayo nitofauti na kifaa halisi kilichodondoka
Back
Top Bottom