Wakuu
Kuna hii dhana kwamba chakula kikidondoka ndani ya sekunde tano bado kinaendelea kuwa salama kwa matumizi na hivyo mtu anaweza kuokota na kukila. Je uhalisia ni upi?
Kuna hii dhana kwamba chakula kikidondoka ndani ya sekunde tano bado kinaendelea kuwa salama kwa matumizi na hivyo mtu anaweza kuokota na kukila. Je uhalisia ni upi?
- Tunachokijua
- Baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kuwa chakula kikidondoka kinaweza kuwa salama tena kama kitaokotwa na kutumiwa tena ndani ya muda mfupi ujao. Dhana ya muda mrefu ni kuwa ni salama kuokota chakula na kukila tena ndani ya sekunde tano.
JamiiCheck imepitia machapisho na tafiti mbalimbali ambazo zinabainisha kuwa dhana hiyo ni potofu kwani chakula kinapoanguka tu hupata bakteria hapo hapo hivyo kinakuwa si salama tena.
Makala iliyoandikwa na Profesa, Daktari Fred Clifton Campbell na kuchapishwa na tovuti ya UT Health anabainisha kuwa kadri chakula kinavyokuwq na unyevu mwingi ndivyo bakteria au vijidudu vingine vinavyoweza kushikamana nacho kwa urahisi.
Watafiti kutokea Chuo Kikuu cha Albama wanaeleza kuwa dhana hii ya "Five-second rule" ni dhana potofu kwani bakteria wanaweza kushikamana na chakula muda mfupi tu baada ya kudondoka. Profesa, Dkt. Jessica Scoffield anafafnua kuwa,
"Bakteria wanaweza kuhamia kwenye chakula mara tu kinapogusa ardhi ama uso wa kitu chochote. Unyevu huongeza kwa kiasi kikubwa uhamishaji huu, na aina ya uso pamoja na aina ya chakula pia huathiri jinsi unavyotokea kwa haraka"
Ingawa kutupa kunaweza kuonekana kama upotevu wa chakula, lakini ni chaguo salama zaidi ili kuepuka hatari inayoweza kutokana na bakteria.