Si kila aliyekolea mapenzini kakolea kwa hiyari

Logistics

Member
Joined
May 16, 2014
Posts
56
Reaction score
18
Wakuu, kuna hii kitu nimeiona kwenye mahusiano ya watu wengi sana, unakuta mwanaume kampenda mwanamke kiasi kwamba hata aambiwe pumba yeye anafuata tu, hata aambiwe mfukuze mama yako nyumbani tubaki wenyewe, basi yeye kweli anatimua kuanzia mama, baba, dada, kaka na wadogo zake wote.

Sasa najaiuliza, huko ndio kukolea katika mapenzi ama vipi? ifike mahala tutambue kuwa, hawa wanawake wetu wanatulisha vitu vya ajabu sana kupitia chakula wanachotuandalia kila siku.

Wanawake hawa hawa tunaojidai tunawapenda sana, wanatutengea maji ya kuoga yenye kila aina ya mitishamba, ili mradi tu tuwe watii, yani kila kitu kwao iwe mteremko.

Bado najiuliza sana, the power of decision making kutoka kwa mwanaume inakuwa wapi mpaka mwanamke awe anafuatwa kwa kila jambo analosema.

Wanaume tuweni makini, and by the way sijui njia itakayo kunasua na hizi limbwata.
 
Kama unaota tabu oa mwanamme, msharuhusiwa na Ing'land.

Kuogopa limbwata ni sawa na kupigwa risasi ya maji kwa bunduki toy afu ukafa. Kilichokuua si hiyo risasi maji, siku zako zilikuwa zishafika tu.

Mbona pilau linaandaliwa kwa mitishamba? Mchicha wenyewe tu ni mitishamba. Mtaanza kupewa vyakula vya plastic ili isiwe mitishamba.
 
MMMMMMh ni kweli kabisa, hasa wanawake wa sasa hivi hawajiamini kabisa katika suala la mapenzi, unakuta mwanamume anapechuka na huko kwenye mchepuko ndiko anakoenda kulishwa hayo malimbwata, anageuka mbogo kwenye familia yake, mwanamume anafukuza mke na watoto ambao alikuwa anawapenda kupita upeo. Ila ninachoamini ni kuwa kila jambo lina mwisho wake, na mwisho waweza kuwa mbaya au mzuri, wanaume nawashauri sana ukiwa karibu na Mungu haya mambo ya malimbwata hayatakukuta asilani.
 
Mi natamani nipewe limbwata kabisa nimpende na kumsikiliza zaidi. hahahahaaaaa......!!!. mia
 
umenikumbusha songi 1 la kikenya kiitikio kipo hv.
amenipa juju oooh oooh oooh!,
amenipa juju,
nimeshachiziiii!!!.....x2
 
Usioe mwayego kaa tu kwa maza, wanawake sio watu wazuri
afu limbwata yenyewe wanaidumbukiza huku hivi, kaa nao mbali....

kwan kulidumbukiza huko chini kazi? Mbona watu wanazama chumvin na hawaoni kinyaa? Usimfanye mwenzako akajichelewesha bure
 
Hili tatizo litaisha iwapo Hair Salon za wanawake zote zikifungwa mjini. Huko ndo kinapatikana kirusi cha ushauri mbaya kwa wakezetu.
 
Wakuu, kuna hii kitu nimeiona kwenye mahusiano ya watu wengi sana, unakuta mwanaume kampenda mwanamke kiasi kwamba hata aambiwe pumba yeye anafuata tu, hata aambiwe mfukuze mama yako nyumbani tubaki wenyewe, basi yeye kweli anatimua kuanzia mama, baba, dada, kaka na wadogo zake wote.

Sasa najaiuliza, huko ndio kukolea katika mapenzi ama vipi? ifike mahala tutambue kuwa, hawa wanawake wetu wanatulisha vitu vya ajabu sana kupitia chakula wanachotuandalia kila siku.

Wanawake hawa hawa tunaojidai tunawapenda sana, wanatutengea maji ya kuoga yenye kila aina ya mitishamba, ili mradi tu tuwe watii, yani kila kitu kwao iwe mteremko.

Bado najiuliza sana, the power of decision making kutoka kwa mwanaume inakuwa wapi mpaka mwanamke awe anafuatwa kwa kila jambo analosema.

Wanaume tuweni makini, and by the way sijui njia itakayo kunasua na hizi limbwata.

Au wewe mzee nn maana nashindwa kupata picha uchunguzi wako uliufanyaje???
 
MMMMMMh ni kweli kabisa, hasa wanawake wa sasa hivi hawajiamini kabisa katika suala la mapenzi, unakuta mwanamume anapechuka na huko kwenye mchepuko ndiko anakoenda kulishwa hayo malimbwata, anageuka mbogo kwenye familia yake, mwanamume anafukuza mke na watoto ambao alikuwa anawapenda kupita upeo. Ila ninachoamini ni kuwa kila jambo lina mwisho wake, na mwisho waweza kuwa mbaya au mzuri, wanaume nawashauri sana ukiwa karibu na Mungu haya mambo ya malimbwata hayatakukuta asilani.

Kumbe limbwata linatolewa kwenye Michepuko?? Aagh!! Basi wanajitakia wenyewe, mi nilianza kufurahi nikijua linatolewa kwenye njia kuu!! Michepuko sasa baasi nielekezeni linavyoandaliwa ili nami nikampe njia kuu wangu nimpende zaidi na zaidi na zaidi hata nisipate kuchepuka tena
 
Dawa ya hizo takataka ni kukaza kwenye ibada tu
 
Wanaume wengine,wanakera,mishenzi,haijali ndoa,hakuthamini,michepuko kibao na vipigo juu!ndo mnapowahiwa hapo.
 
mimi natafuta limbwata kali mwenye dondoo anipe bahshishi itatolewa iliyonona
 
Back
Top Bottom