Shy-Rose Bhanji awapa makavu CCM

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,833
Shy-Rose Bhanji

Imekuwa ni desturi kwa baadhi ya WanaCCM kwamba kila ninapotoa maoni yangu ya kukikosoa chama changu au serikali wamekuwa wananishambulia kuwa ni sababu ya kukosa ubunge wa Afrika Mashariki. Sina chuki ya kukosa ubunge na hii naisema kutoka moyoni. Siku zote nimekuwa mkweli kwamba pale panapotakiwa kukosoa sijasita kufanya hivo na pale panapotakiwa kupongeza sijasita kufanya hivo.

Kwa vile ninanyanyaswa sana ni vizuri nilitolee ufafanuzi: Huo ubunge siyo kwamba nilikosa lakini ni kutokana na majungu, fitna na roho mbaya ya baadhi ya watu....vita niliyopigwa ni kubwa sana na Mungu tu ndo anajua. Ni kweli kwamba niliumia sana sana kwasababu sikujua nimemkosea nini Rais Magufuli mtu ambaye nilimpenda kwa moyo wangu wote. Isitoshe kazi yangu ya ubunge niliifanya kwa kujituma na kwa moyo wangu wote. Ulikuwa huniambii kitu pale lilipotajwa jina lake...nilifunga safari mpaka mikoani kumfanyia kampeni kwa pesa zangu mfukoni siyo kwamba anipe cheo, hapana ni kwasababu nilimwamini.

Na Naomba niwaulize hivi JK angemkata jina Magufuli baada ya kushinda kura za maoni ndani ya chama angejiskiaje? Hakika angeumia lakini nina imani angemsamehe kama vile mimi nilivomsamehe. Hizi ni nafasi leo zipo na kesho hazipo. Ni sawa na kuja duniani na kesho tunaondoka. Naomba sana sana msininyanyase kwasababu mnaniumiza moyo wangu
 
Ni kweli ameumizwa sana na ataendelea kuumizwa na anawakilisha maoni ya mamilioni ya watanzania vimbelembele waliompigia kampeni na kura Magufuli lakini mwisho wa siku wakaishia kuisoma namba.
Ndugu huyu jamaa tulimchagua kwa utashi wetu kabisa mimi nikiwa miongoni mwao. Yapo mema kafanya na makosa pia, nimekuwa mvumilivu wa makosa yake na nadhani ninge endelea kumpa muda isipo kuwa pale alipo unda kundi la kuuwa na kuteka, kupoteza serekali yake ikalibatiza jina la la wasio julikana! hamu yote iliniishia, imani yangu kwa MAGUFULI haipo kabisa.
 
Huyu Naye sijui anachujaga maneno kabla ya kuongea, kwa hiyo kosa la magu ni kumkata sio? Je aliyepata badala yake anasemaje kuhusu Magu? Hesabu zingine ni Plus na minus so afikirie zaidi. Yeye anamuuliza magu kama angekatwa ingekuweje je ameshawahi kujiuliza je edo alipokatwa bila huruma na rafiki yake kipenzi alijifikiriaje.
Na anaposema alikuwa anafanyakazi nzuri je ni ipi na ninani alimpa hizo credit
 
Huyu alikuwa ni mzigo kwa CCM, hakuwa anaisaidia CCM bali kuichafua kutokana na ulevi wake hadi mahali pa kazi. Aibu aliyoletea taifa kwa kulewa mkutanoni na kufanya vurugu kwenye ndege sababu ya ulevi alitegemea Magu mzee wa vetting za usalama angempitisha.

Na anachofanya saivi anazidi ku prove Magu yupo sahihi, dada Shy Rose hastahili ile kazi, hana akili wala mkakati wowote, kama anategemea kumtisha Magu kwa kutukana na kushinda Ghetto na Halima Mdee huku akiposti ujinga ujinga kwenye mtandao ni wazi basi alikuwa hajaiva. Mwanaume mwenye akili akijerehiwa anafunga mdomo na kufanya mikakata ya chini kwa chini, mbona kina Malima, Mkuchika na RC wa Tabora wamerudishwa kwenye system.

Mwisho na muhimu, dada Shy-Rose chunga sana unavyoshinda shinda Ghetto na Halima Mdee, Ester Bulaya hafurahii kuja kuja kwako, wivu wa mapenzi mbaya, utakuja chomwa kisa bure.
 
Shida si kukatwa na magufuli shida yake ilikuwa ni namna alivyokuwa akiwa kwenye ubunge....alikuwa ni mtu wa skendo za ajabu ajabu tu..hata mimi ningemkata maana alikuwa analiabisha taifa...hata kama alimpigania kwa pesa yake lakini siyo tiketi ya yeye kupewa huo ubunge
 
Huyu alikuwa ni mzigo kwa CCM, hakuwa anaisaidia CCM bali kuichafua kutokana na ulevi wake hadi mahali pa kazi. Aibu aliyoletea taifa kwa kulewa mkutanoni na kufanya vurugu kwenye ndege sababu ya ulevi alitegemea Magu mzee wa vetting za usalama angempitisha.

Na anachofanya saivi anazidi ku prove Magu yupo sahihi, dada Shy Rose hastahili ile kazi, hana akili wala mkakati wowote, kama anategemea kumtisha Magu kwa kutukana na kushinda Ghetto na Halima Mdee huku akiposti ujinga ujinga kwenye mtandao ni wazi basi alikuwa hajaiva. Mwanaume mwenye akili akijerehiwa anafunga mdomo na kufanya mikakata ya chini kwa chini, mbona kina Malima, Mkuchika na RC wa Tabora wamerudishwa kwenye system.

Mwisho na muhimu, dada Shy-Rose chunga sana unavyoshinda shinda Ghetto na Halima Mdee, Ester Bulaya hafurahii kuja kuja kwako, wivu wa mapenzi mbaya, utakuja chomwa kisa bure.
Jinsi yako ni ipi?
 
Shy-Rose Bhanji

Imekuwa ni desturi kwa baadhi ya WanaCCM kwamba kila ninapotoa maoni yangu ya kukikosoa chama changu au serikali wamekuwa wananishambulia kuwa ni sababu ya kukosa ubunge wa Afrika Mashariki. Sina chuki ya kukosa ubunge na hii naisema kutoka moyoni. Siku zote nimekuwa mkweli kwamba pale panapotakiwa kukosoa sijasita kufanya hivo na pale panapotakiwa kupongeza sijasita kufanya hivo. Kwa vile ninanyanyaswa sana ni vizuri nilitolee ufafanuzi: Huo ubunge siyo kwamba nilikosa lakini ni kutokana na majungu, fitna na roho mbaya ya baadhi ya watu....vita niliyopigwa ni kubwa sana na Mungu tu ndo anajua. Ni kweli kwamba niliumia sana sana kwasababu sikujua nimemkosea nini Rais Magufuli mtu ambaye nilimpenda kwa moyo wangu wote. Isitoshe kazi yangu ya ubunge niliifanya kwa kujituma na kwa moyo wangu wote. Ulikuwa huniambii kitu pale lilipotajwa jina lake...nilifunga safari mpaka mikoani kumfanyia kampeni kwa pesa zangu mfukoni siyo kwamba anipe cheo, hapana ni kwasababu nilimwamini. Na Naomba niwaulize hivi JK angemkata jina Magufuli baada ya kushinda kura za maoni ndani ya chama angejiskiaje? Hakika angeumia lakini nina imani angemsamehe kama vile mimi nilivomsamehe. Hizi ni nafasi leo zipo na kesho hazipo. Ni sawa na kuja duniani na kesho tunaondoka. Naomba sana sana msininyanyase kwasababu mnaniumiza moyo wangu
Unajua maana ya neno makavu? Kama upo karibu yake muulize mwaka 2010 alilalamika nini kwa Mzee Makamba! Nyani haoni kundule waswahili walinena
 
Back
Top Bottom