Shy-Rose Bhanji awapa makavu CCM

Shy-Rose Bhanji awapa makavu CCM

Huyu alikuwa ni mzigo kwa CCM, hakuwa anaisaidia CCM bali kuichafua kutokana na ulevi wake hadi mahali pa kazi. Aibu aliyoletea taifa kwa kulewa mkutanoni na kufanya vurugu kwenye ndege sababu ya ulevi alitegemea Magu mzee wa vetting za usalama angempitisha.

Na anachofanya saivi anazidi ku prove Magu yupo sahihi, dada Shy Rose hastahili ile kazi, hana akili wala mkakati wowote, kama anategemea kumtisha Magu kwa kutukana na kushinda Ghetto na Halima Mdee huku akiposti ujinga ujinga kwenye mtandao ni wazi basi alikuwa hajaiva. Mwanaume mwenye akili akijerehiwa anafunga mdomo na kufanya mikakata ya chini kwa chini, mbona kina Malima, Mkuchika na RC wa Tabora wamerudishwa kwenye system.

Mwisho na muhimu, dada Shy-Rose chunga sana unavyoshinda shinda Ghetto na Halima Mdee, Ester Bulaya hafurahii kuja kuja kwako, wivu wa mapenzi mbaya, utakuja chomwa kisa bure.
huko ghetto kwa halima inaoenakana mnashinda wote na hao wanawake wenzio maana unavyoandika ni kama unajua kila kitu.
 
Ndio mkomage kujipendekeza! Mbona ilikuwa dhahiri kuwa Jiwe hafiti kwenye nafasi aliyopo! Na bado wapo wengine wanauguza vidonda kimya kimya! Ulidhani namba wataisoma wapinzani peke yao?
 
Wacha waisome namba eeeeh ,waisome nambaa ccm mbele kwa mbele.

Walidhani wanamwimbia Mbowe na Tundu Lissu.

Mbowe ni bilionare hana njaa ktk siasa, ukimkomoa unakomoka.mwenyewe same applies kwa wapinzani wengine.

Maneno kama

.....nilimpenda sana

.....nilimwamini sana.

ebaki historia, Chatu mdogo mnaemfuaga akikua si atawala??
Shy-Rose Bhanji

Imekuwa ni desturi kwa baadhi ya WanaCCM kwamba kila ninapotoa maoni yangu ya kukikosoa chama changu au serikali wamekuwa wananishambulia kuwa ni sababu ya kukosa ubunge wa Afrika Mashariki. Sina chuki ya kukosa ubunge na hii naisema kutoka moyoni. Siku zote nimekuwa mkweli kwamba pale panapotakiwa kukosoa sijasita kufanya hivo na pale panapotakiwa kupongeza sijasita kufanya hivo. Kwa vile ninanyanyaswa sana ni vizuri nilitolee ufafanuzi: Huo ubunge siyo kwamba nilikosa lakini ni kutokana na majungu, fitna na roho mbaya ya baadhi ya watu....vita niliyopigwa ni kubwa sana na Mungu tu ndo anajua. Ni kweli kwamba niliumia sana sana kwasababu sikujua nimemkosea nini Rais Magufuli mtu ambaye nilimpenda kwa moyo wangu wote. Isitoshe kazi yangu ya ubunge niliifanya kwa kujituma na kwa moyo wangu wote. Ulikuwa huniambii kitu pale lilipotajwa jina lake...nilifunga safari mpaka mikoani kumfanyia kampeni kwa pesa zangu mfukoni siyo kwamba anipe cheo, hapana ni kwasababu nilimwamini. Na Naomba niwaulize hivi JK angemkata jina Magufuli baada ya kushinda kura za maoni ndani ya chama angejiskiaje? Hakika angeumia lakini nina imani angemsamehe kama vile mimi nilivomsamehe. Hizi ni nafasi leo zipo na kesho hazipo. Ni sawa na kuja duniani na kesho tunaondoka. Naomba sana sana msininyanyase kwasababu mnaniumiza moyo wangu
 
Ndugu huyu jamaa tulimchagua kwa utashi wetu kabisa mimi nikiwa miongoni mwao. Yapo mema kafanya na makosa pia, nimekuwa mvumilivu wa makosa yake na nadhani ninge endelea kumpa muda isipo kuwa pale alipo unda kundi la kuuwa na kuteka, kupoteza serekali yake ikalibatiza jina la la wasio julikana! hamu yote iliniishia, imani yangu kwa MAGUFULI haipo kabisa.
Kweli mkuu makosa yote yanavumilika lakini hili la wasiojulikana linakatisha tamaa kabisa.

Unaumda kundi la kuua binadamu wenzako??
 
Shy-Rose Bhanji

Imekuwa ni desturi kwa baadhi ya WanaCCM kwamba kila ninapotoa maoni yangu ya kukikosoa chama changu au serikali wamekuwa wananishambulia kuwa ni sababu ya kukosa ubunge wa Afrika Mashariki. Sina chuki ya kukosa ubunge na hii naisema kutoka moyoni. Siku zote nimekuwa mkweli kwamba pale panapotakiwa kukosoa sijasita kufanya hivo na pale panapotakiwa kupongeza sijasita kufanya hivo. Kwa vile ninanyanyaswa sana ni vizuri nilitolee ufafanuzi: Huo ubunge siyo kwamba nilikosa lakini ni kutokana na majungu, fitna na roho mbaya ya baadhi ya watu....vita niliyopigwa ni kubwa sana na Mungu tu ndo anajua. Ni kweli kwamba niliumia sana sana kwasababu sikujua nimemkosea nini Rais Magufuli mtu ambaye nilimpenda kwa moyo wangu wote. Isitoshe kazi yangu ya ubunge niliifanya kwa kujituma na kwa moyo wangu wote. Ulikuwa huniambii kitu pale lilipotajwa jina lake...nilifunga safari mpaka mikoani kumfanyia kampeni kwa pesa zangu mfukoni siyo kwamba anipe cheo, hapana ni kwasababu nilimwamini. Na Naomba niwaulize hivi JK angemkata jina Magufuli baada ya kushinda kura za maoni ndani ya chama angejiskiaje? Hakika angeumia lakini nina imani angemsamehe kama vile mimi nilivomsamehe. Hizi ni nafasi leo zipo na kesho hazipo. Ni sawa na kuja duniani na kesho tunaondoka. Naomba sana sana msininyanyase kwasababu mnaniumiza moyo wangu
Sio wew tu use kiongoz kunawengne, ukichukia chukia sana but jpm ndio alishaamua hvyo
 
Shy Rose, asilielie mitandaoni bali atulie maisha yaendelee. Na kwa style ya kumshambulia Mkiti ndio kabisa anaonesha vetting ilikuwa sahihi.
Namshauri akachukue busara kwa Mh. Maudline Castico ambaye aliwahi kufukuzwa CCM kuwa sio raia akiwa Mjumbe wa KK Taifa akafanya subira leo ni Waziri kwa Zanzibar.

Kimsingi, katika siasa majungu na fitna ni mambo ya kawaida hivyo pambana navyo uvishinde.
Kabisa siasa na majungu pipa na mfuniko
 
Nchi Ya Asali Na Maziwa
Nchi Iendelee Mbele
Standard Gauge Railway (SGR )
Stigler Gorge Kazi Inaendelea Tupate Megawatts 2000
 
Kweli mkuu makosa yote yanavumilika lakini hili la wasiojulikana linakatisha tamaa kabisa.

Unaumda kundi la kuua binadamu wenzako??
Kawkweli mkuu amani na utulivu vimepungua baada ya Magufuli kuingia madarakani, kabla yake matukio ya utekaji, upoteaji, kupiga risasi hadharani, watu kukimbia nchi yao wakiwindwa na wasio julikana vineshamiri baada ya Magufuli kuingia madarakani....utetezi wa serekali ni wa kipuuzi kabisa yahani wanajificha kwenye mapambano ya dhidi ya ufisadi ambayo kimsingi ni muhimu kama yatapiganwa pasipo ku compromise usalama.
 
Unasema amani na utulivu vimepungua halafu uko kwako una chart hahaha unajua maana ya amani na utuluvu kupungua? Huu wasaha wa kujadili na kuchati umeupata kama hakuna amani?
 
Back
Top Bottom