Shy-Rose Bhanji Ajitetea

Shy-Rose Bhanji Ajitetea

Mimi Shy-Rose Bhanji, Mbunge wa Afrika Mashariki-Tanzania, ninapinga vikali na kwa nguvu zote shutuma zilizotolewa dhidi yangu kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.
Shutuma hizi hazina ukweli wowote na zinalenga, si kuniharibia, bali kuchafua sifa yangu na utendaji kazi wangu katika Bunge la Afrika Mashariki.
Lengo kuu la shutuma hizo ni kunivunja nguvu na ari ya kutetea maslahi ya nchi yangu na Watanzania wenzangu kwani daima nimekuwa kikwazo na mwiba kwenye ajenda zinazokiuka maslahi ya Tanzania.
Kwa mfano ardhi ya Tanzania kugawiwa kwa wana Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kinyume na Sera ya Tanzania. Nimekuwa miongoni mwa wabunge wa Tanzania tulio mbele katika kulipinga suala hilo. Sishangai likinijengea uadui.
Isitoshe, kwenye ajenda ya kumuondoa madarakani Spika wa EALA, Dk. Margaret Zizziwa, nilisimama kidete kwa kutounga mkono kwa sababu halikuwa na maslahi ya Tanzania na yalikuwa kinyume na malengo ya ushirikiano wa Jumuiya nzima.
Hoja ya kumuondoa Spika ilikuwa ni sehemu ya ‘mchezo mchafu’ ya ajenda ya siri ya kumweka kwenye nafasi hiyo mjumbe mwingine kwa maslahi ya wachache.
Jaribio hili la kumuondoka Spika lilifanywa na kushindikana mara tatu baada ya kukosa sahihi za kutosha kutoka Tanzania, ikiwamo ya kwangu.
Baada ya kampeni ya kumwondoa Spika kushindwa, wabunge kadhaa walikuwa wanasusia vikao vya Bunge wakati wameshachukua posho za vikao. Kwa mfano kikao kilichofanyika hivi karibuni hapa Dar es Salaam.
Malumbano ndio yamekuwa yakitawala na kuinyima Bunge akidi ya kuendelea na ajenda za mtangamano. Huu ni usaliti wa wazi kwa nchi zilizowachagua na kuwatuma katika Bunge la EALA.
Ukijaribu kuwaasa kwamba mwenendo huo si sahihi, unageuka kuwa adui.
Na sasa wameamua kunitukana na kuzusha tuhuma kadhaa kupitia mitandao ya kijamii ambako yote ni utunzi wa kisanii usiokuwa na chembe ya ukweli, uhalali wala ushahidi.
Wahenga walisema ‘akutukanaye hakuchagulii tusi’. Walete ushahidi wa tuhuma zote dhidi yangu.
Kwa mfano, shutuma kwamba nililewa pombe ndani ya ndege, kuvunja chupa, kufanya fujo na kufungwa pingu wakati wa safari ya Ubelgiji si kweli hata kidogo.
Kama hizi tuhuma ni za kweli, kwanini hazikupelekwa polisi, serikalini au vyombo vingine vya sheria baada tu ya tukio?
Ijewe wamesubiri wiki mbili baada ya madai hayo ya tukio la kutunga ndipo wajitokeze wakati wa kikao kinachoendelea mjini Kigali, Rwanda? Kwanini wasubiri kikao cha Kigali ndipo uzushi huu utolewe?
Tuhuma kwamba nimewatukana marais wa nchi tatu hazina mashiko isipokuwa kuhalalisha kampeni ya wale wanaonichafua na kuibua chuki kwa maraisi na raia katika nchi za Kenya, Rwanda na Burundi.
Ninayo heshima kubwa sana kwa marais wa nchi zote tano na raia wa nchi wanachama ambako mara zote nimepokewa na kuishi kwa amani na upendo katika nchi hizo. Naahidi kuedeleza heshima hii.
Hainiingii kichwani ni wapi nilipoteza heshima hii isipokuwa kwa wale wasionitakia mema ambao wamekusudia kufanikisha ajenda zao.
Shutuma zote dhidi yangu zimetengenezwa na watu ambao hatushabihiani katika hoja zetu na sishangai kwa hilo.

Mimi ni Mtanzania na ni Mbunge wa Tanzania. Hivyo nina wajibu wa kulinda na kutetea maslahi ya Watanzania ili kuleta mtangamano wenye uwiano sawa kwa nchi zote wanachama.

Ninaahidi nitaendelea kuwatumikia Watanzania kwa nguvu zangu zote na kutoa ushirikiano kwa wabunge wengine wa EALA kwa manufaa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Nimeyasema haya nikiamini kuwa: “Uongo ukiachwa usemwe mara nyingi unaweza kuaminiwa kuwa ni ukweli.”
Mungu ibariki Afrika MasharikiUmoja Wetu ni Nguzo Yetu

Hivi ni vigezo gani vilitumika kumuchagua shy rose kutuwakilisha katika eneo nyeti kama hilo? Jamani kama kuna mtu ana wasifu wa huyu mama naomba, kabla sijasema lolote juu yake
 
Kachelewa kukanusha, kwangu mie nimeamini kile kilichosemwa awali.

Yale maelezo ya awali yalikuwa na chembechembe za uwongo/maelezo yasiyoendana na uhalisia wa mambo ambayo yanapelekea story nzima kukosa uhalali. Kwa mfano, maelezo kwamba wabunge/abiria walimsihi rubani asitue Cairo kwa dharura (emergency landing) si tu ni uongo bali inaonyesha aliyetunga habari ile asivyokuwa makini. Hivi kweli rubani huwa anapokea ushauri kutoka kwa abiria wa ni nini cha kufanya? Ushauri kwamba rubani asifanye emergence landing unatolewa na abiria? kweli? Kwamba kuna abiria anafanya fujo kwenye ndege (anavunja chupa nk) na anahatarisha usalama wa abiria wengine pamoja na ndege yenyewe,na utaratibu unamwelekeza rubani kufanya emergence landing ili polisi wafanye kazi yao nk., lakini abiria wanamsihi rubani akiuke taratibu naye anawaelewa na safari inaendelea. Kweli? Haya ndio yale mambo ya kina Hashim Lundenga na Miss Tanzania na Passport na Vyeti vya Kuzaliwa vya kufoji huku akitarajia watu waelewe tu, pengine kwa kuwa amezoea sana kudanganya kiasi kwamba kwake kudanganya ni hali ya kawaida.
 
Mimi ni Mtanzania na ni Mbunge wa Tanzania. Hivyo nina wajibu wa kulinda na kutetea maslahi ya Watanzania ili kuleta mtangamano wenye uwiano sawa kwa nchi zote wanachama.

Ninaahidi nitaendelea kuwatumikia Watanzania kwa nguvu zangu zote na kutoa ushirikiano kwa wabunge wengine wa EALA kwa manufaa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Safi sana mama.....we chapa kazi. Hao wakuguse tu waone muungano huu utakavyokwisha in seconds!
 
Mimi huu utetezi sijasoma wote na pia hata ile habari sikuimaliza yote. Habari yenyewe kwa msomaji makini ukianza tu kuisoma unaona kabisa imekaa kimajungu majungu sana. Simtetei huyu Shy ila pia siwezi kumsulubisha kwa habari iliyokaa kimajungu majungu kama ile.
 
sidhani kama kuna mtu yeyote atafanya fujo kama ilivyo daiwa ndani ya ndege na asikamatwe na polisi mara tu anapofika iendako - kawaida pilot anawajulisha polisi mapema kuwa kuna mtu anafanya fujo na huwa wanamsubri mlangoni mara tu ndege inapotuwa hutiwa mbaroni na kufunguliwa mashataka ya kuharibu amani akiwa ndani ya ndege,. Hizi habari hazina ukweli

go go go go shyrose wewe ni shujaa unamkomesha kagame na vbaraka wake .....najua kagame anajua uhuru ni dhaifu na anaingilika kirais ndio maana anadai na kenya imetukanwa kilichopo apo ni kua kagame anataka kumuondoa huyu spka mganda aweke mnyaruanda au mkenya ili atekeleze maslahi ya rwanda na kenya ya kuja kupgania ardhi tanzania kwa kila mwananchi kupewa cash na nchi yake na kuja kulangua ardhi yetu wanataka spka wao ili achakachue akidi wadai bunge limeptsha ikfka kwa marais wawe na ndio ya wengi......watanzani jf imevamiwa na watus wa rwanda kuwen makini tumuunge m kono shyrose mti wenye matunda ndio unaopgwa mawe.......ukfanya fujo kwenye ndege uktua tu unawekwa ndan mbona shy hakuwekwa ndani wastudanganya hao watusi
 
Shyrose ni shujaa.....kagame anatapatapa mwsho tunamtoa ikulu ya kigali tme will tell
 
Kama alitiwa pingu kwenye ndege si tungesikia kwenye habari za kimataifa? African MP arrested in the sky!:sleepy:
 
Hii habari eti kwamba kafanya hivi mara hivi,, ni uongo mtupu, bali lengo kuu ni kumchafua tu huyu mbunge hodari. Nimefanya udukuzi, hakuna kitu kama hicho.
 
Umalaya ulimtongoza akakupa.acheni chuki Na majungu vijana . Hivi kunywa pombe Tanzania nzima anakunywa huyo dada peke yake?
..we umejuaje kama nilimtongoza akaninyima??..we unatetea majanga kwa kuwa hujui...si hatutaki kuwakilishwa na vihio na wahuni.....
 
Huyo Dada Sura Yake Tu Imekaa Kimatatizo Je Mnategemea Nini? Vitu Vingine Siyo Vya Kuvipotezea Muda! Nilikwisha Mdharau Siku Nyiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii..............ingi.

Kwani ukimdharau wewe ndio kinatokea nini eti?!!!. Figomarakanakipero.
 
Shy-rose anaonewa Katika hili, sidhani Kama ule uzushi ulikuwa ni kweli, Mti wenye Matunda ndio hupigwa mawe.
 
sidhani kama kuna mtu yeyote atafanya fujo kama ilivyo daiwa ndani ya ndege na asikamatwe na polisi mara tu anapofika iendako - kawaida pilot anawajulisha polisi mapema kuwa kuna mtu anafanya fujo na huwa wanamsubri mlangoni mara tu ndege inapotuwa hutiwa mbaroni na kufunguliwa mashataka ya kuharibu amani akiwa ndani ya ndege,. Hizi habari hazina ukweli
Huu ni uzushi tena uliokithiri hivi mtu afanye makosa makubwa kama haya atakaliwa kimya kiasi hicho, je hata picha tu kama kuna ukweli, jamani tubadilike tuache uzushi
 
Mimi Shy-Rose Bhanji, Mbunge wa Afrika Mashariki-Tanzania, ninapinga vikali na kwa nguvu zote shutuma zilizotolewa dhidi yangu kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.
Shutuma hizi hazina ukweli wowote na zinalenga, si kuniharibia, bali kuchafua sifa yangu na utendaji kazi wangu katika Bunge la Afrika Mashariki.
Lengo kuu la shutuma hizo ni kunivunja nguvu na ari ya kutetea maslahi ya nchi yangu na Watanzania wenzangu kwani daima nimekuwa kikwazo na mwiba kwenye ajenda zinazokiuka maslahi ya Tanzania.
Kwa mfano ardhi ya Tanzania kugawiwa kwa wana Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kinyume na Sera ya Tanzania. Nimekuwa miongoni mwa wabunge wa Tanzania tulio mbele katika kulipinga suala hilo. Sishangai likinijengea uadui.
Isitoshe, kwenye ajenda ya kumuondoa madarakani Spika wa EALA, Dk. Margaret Zizziwa, nilisimama kidete kwa kutounga mkono kwa sababu halikuwa na maslahi ya Tanzania na yalikuwa kinyume na malengo ya ushirikiano wa Jumuiya nzima.
Hoja ya kumuondoa Spika ilikuwa ni sehemu ya ‘mchezo mchafu’ ya ajenda ya siri ya kumweka kwenye nafasi hiyo mjumbe mwingine kwa maslahi ya wachache.
Jaribio hili la kumuondoka Spika lilifanywa na kushindikana mara tatu baada ya kukosa sahihi za kutosha kutoka Tanzania, ikiwamo ya kwangu.
Baada ya kampeni ya kumwondoa Spika kushindwa, wabunge kadhaa walikuwa wanasusia vikao vya Bunge wakati wameshachukua posho za vikao. Kwa mfano kikao kilichofanyika hivi karibuni hapa Dar es Salaam.
Malumbano ndio yamekuwa yakitawala na kuinyima Bunge akidi ya kuendelea na ajenda za mtangamano. Huu ni usaliti wa wazi kwa nchi zilizowachagua na kuwatuma katika Bunge la EALA.
Ukijaribu kuwaasa kwamba mwenendo huo si sahihi, unageuka kuwa adui.
Na sasa wameamua kunitukana na kuzusha tuhuma kadhaa kupitia mitandao ya kijamii ambako yote ni utunzi wa kisanii usiokuwa na chembe ya ukweli, uhalali wala ushahidi.
Wahenga walisema ‘akutukanaye hakuchagulii tusi’. Walete ushahidi wa tuhuma zote dhidi yangu.
Kwa mfano, shutuma kwamba nililewa pombe ndani ya ndege, kuvunja chupa, kufanya fujo na kufungwa pingu wakati wa safari ya Ubelgiji si kweli hata kidogo.
Kama hizi tuhuma ni za kweli, kwanini hazikupelekwa polisi, serikalini au vyombo vingine vya sheria baada tu ya tukio?
Ijewe wamesubiri wiki mbili baada ya madai hayo ya tukio la kutunga ndipo wajitokeze wakati wa kikao kinachoendelea mjini Kigali, Rwanda? Kwanini wasubiri kikao cha Kigali ndipo uzushi huu utolewe?
Tuhuma kwamba nimewatukana marais wa nchi tatu hazina mashiko isipokuwa kuhalalisha kampeni ya wale wanaonichafua na kuibua chuki kwa maraisi na raia katika nchi za Kenya, Rwanda na Burundi.
Ninayo heshima kubwa sana kwa marais wa nchi zote tano na raia wa nchi wanachama ambako mara zote nimepokewa na kuishi kwa amani na upendo katika nchi hizo. Naahidi kuedeleza heshima hii.
Hainiingii kichwani ni wapi nilipoteza heshima hii isipokuwa kwa wale wasionitakia mema ambao wamekusudia kufanikisha ajenda zao.
Shutuma zote dhidi yangu zimetengenezwa na watu ambao hatushabihiani katika hoja zetu na sishangai kwa hilo.

Mimi ni Mtanzania na ni Mbunge wa Tanzania. Hivyo nina wajibu wa kulinda na kutetea maslahi ya Watanzania ili kuleta mtangamano wenye uwiano sawa kwa nchi zote wanachama.

Ninaahidi nitaendelea kuwatumikia Watanzania kwa nguvu zangu zote na kutoa ushirikiano kwa wabunge wengine wa EALA kwa manufaa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Nimeyasema haya nikiamini kuwa: “Uongo ukiachwa usemwe mara nyingi unaweza kuaminiwa kuwa ni ukweli.”
Mungu ibariki Afrika MasharikiUmoja Wetu ni Nguzo Yetu

muda ni hakimu mzuri sana.

Sent from my HTC Desire 626GPLUS dual sim using JamiiForums mobile app
 
Huyu nae anataka kutumia turufu ya ''maslahi ya watanzania'' kuficha tabia yake mbovu iliyooza kama yai viza! Anajulikana na watu wa karibu yake kuwa ni mlevi na mgomvi na hali huwa mbaya sana anapolewa! Halafu anatumia ile ile mbinu mufilisi ya ma-ccm kusema ''lete ushahidi'' au ''wanataka kunichufua kwa sababu...''

Mimi sidhani km hoja ya msingi ni "ulevi" km ni tabia hakuanza baada ya kuchaguliwa ubunge...! Km ndivyo aliwezaje kuwa mbunge km ulisemalo lilikua ni tatizo!

Ukweli ni kwamba aliwezaje kusimama kidete dhidi ya hoja zenye maslahi ya nchi kwa udhati kiasi hicho?

Km hoja ni tabia aliyonayo ni lipi ki utendaji hakulifanya sawa? Au kwa kulinganishwa na wabunge wenzie ni wapi hakufaa?

Hoja ya ardhi ilikua kali na nyeti km alisimamia kwa usahihi ubovu wake ni nini?
 
Vema ni kujirekebisha kitabia tu jamii itakuona kama umesingiziwa au la.
SIKU ZOTE POMBE SIYO KITU RAFIKI KWA HESHIMA YA BINADAMU.
 
Wapo wasio lewa na hawana heshima, km kiongozi anaweza kumwambia commissioner wa polisi kwamba "hawezi kazi" au Waziri Mkuu anaruhusu "shisha" bado anaonekana anafaa.... kauli hizi angezitoa Shy ingekuaje?
 
Vema ni kujirekebisha kitabia tu jamii itakuona kama umesingiziwa au la.
SIKU ZOTE POMBE SIYO KITU RAFIKI KWA HESHIMA YA BINADAMU.
Shyrose na makongoro nani anayejulikana kwa ulevi?
 
Back
Top Bottom