Shy-Rose Bhanji Ajitetea

Shy-Rose Bhanji Ajitetea

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,464


Mimi Shy-Rose Bhanji, Mbunge wa Afrika Mashariki-Tanzania, ninapinga vikali na kwa nguvu zote shutuma zilizotolewa dhidi yangu kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.
Shutuma hizi hazina ukweli wowote na zinalenga, si kuniharibia, bali kuchafua sifa yangu na utendaji kazi wangu katika Bunge la Afrika Mashariki.
Lengo kuu la shutuma hizo ni kunivunja nguvu na ari ya kutetea maslahi ya nchi yangu na Watanzania wenzangu kwani daima nimekuwa kikwazo na mwiba kwenye ajenda zinazokiuka maslahi ya Tanzania.
Kwa mfano ardhi ya Tanzania kugawiwa kwa wana Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kinyume na Sera ya Tanzania. Nimekuwa miongoni mwa wabunge wa Tanzania tulio mbele katika kulipinga suala hilo. Sishangai likinijengea uadui.
Isitoshe, kwenye ajenda ya kumuondoa madarakani Spika wa EALA, Dk. Margaret Zizziwa, nilisimama kidete kwa kutounga mkono kwa sababu halikuwa na maslahi ya Tanzania na yalikuwa kinyume na malengo ya ushirikiano wa Jumuiya nzima.
Hoja ya kumuondoa Spika ilikuwa ni sehemu ya ‘mchezo mchafu’ ya ajenda ya siri ya kumweka kwenye nafasi hiyo mjumbe mwingine kwa maslahi ya wachache.
Jaribio hili la kumuondoka Spika lilifanywa na kushindikana mara tatu baada ya kukosa sahihi za kutosha kutoka Tanzania, ikiwamo ya kwangu.
Baada ya kampeni ya kumwondoa Spika kushindwa, wabunge kadhaa walikuwa wanasusia vikao vya Bunge wakati wameshachukua posho za vikao. Kwa mfano kikao kilichofanyika hivi karibuni hapa Dar es Salaam.
Malumbano ndio yamekuwa yakitawala na kuinyima Bunge akidi ya kuendelea na ajenda za mtangamano. Huu ni usaliti wa wazi kwa nchi zilizowachagua na kuwatuma katika Bunge la EALA.
Ukijaribu kuwaasa kwamba mwenendo huo si sahihi, unageuka kuwa adui.
Na sasa wameamua kunitukana na kuzusha tuhuma kadhaa kupitia mitandao ya kijamii ambako yote ni utunzi wa kisanii usiokuwa na chembe ya ukweli, uhalali wala ushahidi.
Wahenga walisema ‘akutukanaye hakuchagulii tusi’. Walete ushahidi wa tuhuma zote dhidi yangu.
Kwa mfano, shutuma kwamba nililewa pombe ndani ya ndege, kuvunja chupa, kufanya fujo na kufungwa pingu wakati wa safari ya Ubelgiji si kweli hata kidogo.
Kama hizi tuhuma ni za kweli, kwanini hazikupelekwa polisi, serikalini au vyombo vingine vya sheria baada tu ya tukio?
Ijewe wamesubiri wiki mbili baada ya madai hayo ya tukio la kutunga ndipo wajitokeze wakati wa kikao kinachoendelea mjini Kigali, Rwanda? Kwanini wasubiri kikao cha Kigali ndipo uzushi huu utolewe?
Tuhuma kwamba nimewatukana marais wa nchi tatu hazina mashiko isipokuwa kuhalalisha kampeni ya wale wanaonichafua na kuibua chuki kwa maraisi na raia katika nchi za Kenya, Rwanda na Burundi.
Ninayo heshima kubwa sana kwa marais wa nchi zote tano na raia wa nchi wanachama ambako mara zote nimepokewa na kuishi kwa amani na upendo katika nchi hizo. Naahidi kuedeleza heshima hii.
Hainiingii kichwani ni wapi nilipoteza heshima hii isipokuwa kwa wale wasionitakia mema ambao wamekusudia kufanikisha ajenda zao.
Shutuma zote dhidi yangu zimetengenezwa na watu ambao hatushabihiani katika hoja zetu na sishangai kwa hilo.

Mimi ni Mtanzania na ni Mbunge wa Tanzania. Hivyo nina wajibu wa kulinda na kutetea maslahi ya Watanzania ili kuleta mtangamano wenye uwiano sawa kwa nchi zote wanachama.

Ninaahidi nitaendelea kuwatumikia Watanzania kwa nguvu zangu zote na kutoa ushirikiano kwa wabunge wengine wa EALA kwa manufaa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Nimeyasema haya nikiamini kuwa: “Uongo ukiachwa usemwe mara nyingi unaweza kuaminiwa kuwa ni ukweli.”
Mungu ibariki Afrika MasharikiUmoja Wetu ni Nguzo Yetu




 

Attachments

Hapo ni blaha blaha tupu! Kwa nini aambiwe yeye tu na sio wabunge wengine wa tanzania?

Hiii inji bana ni shida mtu anaiwakilisha tanzania kimataifa anadanganya uma ana miaka 18ilhali ni kijeba halafu watu wazima kabisa na mvi juu wanakuja kumsafisha tena bila hata soni halafu aisee hapa ndipo napo washusha imani kabisa watu wa hovyo sana.
 
Huyu nae anataka kutumia turufu ya ''maslahi ya watanzania'' kuficha tabia yake mbovu iliyooza kama yai viza! Anajulikana na watu wa karibu yake kuwa ni mlevi na mgomvi na hali huwa mbaya sana anapolewa! Halafu anatumia ile ile mbinu mufilisi ya ma-ccm kusema ''lete ushahidi'' au ''wanataka kunichufua kwa sababu...''
 
Sawa mimi sina tatizo na maelezo yake ila hajajibu shutuma zile za jana, kwa mfano:

Ni kweli mlienda hiyo safari?

ulikuwa na nani katika msafara wenu huo?

Nini kilichojili wakati wa safari hiyo? mkiwa angani na baada ya kufika?
 
sosoliso Shy- Rose Wangu amejibu

Alishasema toka jana hizi zilikuwa ni pumba zilizokuwa na ajenda ya siri GAUTAMA.. Yule mtoa mada atakuwa ni part wa hii kampeni.. Ningependa sana kama Uongozi wa JF ungekuwa unawachukulia hatua kali wale wote ambao wanataka kuutumia mtandao huu kuwachafua wengine kwa uongo usio na mbele wala nyuma..
 
Last edited by a moderator:
Kuna mwendesha semina mmoja pale Mlimani City alikazana kuwaambia wanasemina wake "MNAPASWA KUWAZA NJE YA BOX".....Mmoja wa wanasemina alikerwa na kurudiwa rudiwa kwa kauli hiyo, akamuomba mseminishaji aeleze nini maana ya kuwa ndani ya box, nini maana ya kuwaza nje ya box na kwa namna gani mtu anawaza ndani au nje ya box...!! Bahati mbaya mseminishaji alishindwa kutoa ufafanuzi...kwa lugha nyepesi ailonekana kakariri msemo huo bila kuuelewa..macho_mdiliko ebu anzisha uzi mhususi utoe mhadhara juu usemi huo-KUWAZA NJE YA BOX
 
Sio kweli! Jaribu kuwaza nje ya box!

Mkuu mimi nimewaza nje ya boksi ndio maana nikaja na hitimisho hilo.Habari kwa nini iwepo muda huu kwa tukio lililotokea wiki 2 zilizopita na baada ya mkutano kufanyika Kigali.Aliyeleta uzi kuhusu huyu mama alisema habari ya huyu mama imebandikwa kwenye tovuti ya bunge lao, nimeangalia tovuti yao hakuna kitu kama hicho.
 
Kuna mwendesha semina mmoja pale Mlimani City alikazana kuwaambia wanasemina wake "MNAPASWA KUWAZA NJE YA BOX".....Mmoja wa wanasemina alikerwa na kurudiwa rudiwa kwa kauli hiyo, akamuomba mseminishaji aeleze nini maana ya kuwa ndani ya box, nini maana ya kuwaza nje ya box na kwa namna gani mtu anawaza ndani au nje ya box...!! Bahati mbaya mseminishaji alishindwa kutoa ufafanuzi...kwa lugha nyepesi ailonekana kakariri msemo huo bila kuuelewa..macho_mdiliko ebu anzisha uzi mhususi utoe mhadhara juu usemi huo-KUWAZA NJE YA BOX

Asante mkuu kwa kuliona hilo.
 
Huyu nae anataka kutumia turufu ya ''maslahi ya watanzania'' kuficha tabia yake mbovu iliyooza kama yai viza! Anajulikana na watu wa karibu yake kuwa ni mlevi na mgomvi na hali huwa mbaya sana anapolewa! Halafu anatumia ile ile mbinu mufilisi ya ma-ccm kusema ''lete ushahidi'' au ''wanataka kunichufua kwa sababu...''

Mi naona kama akijisikia kuitumia hiyo turufu atumie tu. Kwani kuna mwanasiasa gani hapa Tz anajali hayo maslahi ya watanzania hadi sasa? Tumeshakuwa shamba lisilokuwa na mwenyewe, kila anayepita anachuma kiasi chake, na ziada anakanyagakanyaga mradi watoto na wajukuu zetu waje wafe njaa!
 
sidhani kama kuna mtu yeyote atafanya fujo kama ilivyo daiwa ndani ya ndege na asikamatwe na polisi mara tu anapofika iendako - kawaida pilot anawajulisha polisi mapema kuwa kuna mtu anafanya fujo na huwa wanamsubri mlangoni mara tu ndege inapotuwa hutiwa mbaroni na kufunguliwa mashataka ya kuharibu amani akiwa ndani ya ndege,. Hizi habari hazina ukweli
 
Back
Top Bottom