Shy-Rose Bhanji Ajitetea

Shy-Rose Bhanji Ajitetea

Haya tumemsikia SRB sasa mleta uzi wa kwanza alete ushahidi wa taarifa yake ya awali,
atuwekee picha ya mtuhumiwa akiwa amefungwa pingu n.k.Kwenye ndege siku hizi hatuzimi simu tunatumia 'Flight mode'
si rahisi tukio kubwa kama hili kukosa walau picha moja,iwe ya mnato au ya video.
 
BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI KANDA YA TANZANIA (EALA-TZ)
_____________________________________________________



TAMKO LA PAMOJA LA WABUNGE WA TANZANIA WANAOWAKILISHA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI (EALA) JUU YA SAKATA LA KUTAKA KUMVUA MADARAKA SPIKA WA BUNGE HILO 0/06/2014

Sisi, Wabunge saba wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania (EALA-TZ), tunapenda kusisitiza msimamo wetu wa kutounga mkono jaribio la kutaka kumuondoa madarakani Spika wa EALA, Mh. Margaret Nantongo Zziwa.

Baada ya kutafakari kwa uangalifu na kwa umakini mkubwa kuhusu chanzo halisi cha hoja yenyewe ya kutaka kumuondoa Spika wa EALA madarakani, tuligundua mambo yafuatavyo:

1. Hoja hii haina maslahi ya Tanzania na iko kinyume na malengo ya ushirikiano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Tumebaini kuwa hoja yenyewe ni sehemu ya "mchezo mchafu" wa ajenda ya siri ya kujaribu kuweka mbele maslahi ya baadhi ya wanachama wachache wa jumuiya badala ya kuzingatia maslahi mapana ya EAC.

2. Tuhuma mbalimbali zilizotajwa dhidi ya Spika wa EALA kuhusu yeye kuonesha upendeleaji, ujeuri na mapungufu mengine ya uongozi zimegundulika kuwa hazina mashiko na wala mantiki .

3. Kitendo ambacho kimetushtua ni kuwa kumekuwa na majaribio kadhaa ya baadhi ya Wabunge wa EALA kutoka nje ya Tanzania na viongozi wa Sekretarieti ya EAC kutaka kulazimisha sahihi za baadhi ya Wabunge wa Tanzania zitumike kinyume na utaratibu kuunga mkongo Azimio tajwa (kitu ambacho tunakipinga kwa nguvu zote). Hii inadhihirisha kuwepo kwa ajenda ya siri katika sakata hilo dhidi ya maslahi ya Tanzania na jumuiya kwa ujumla.


4. Kufuatia malumbano yaliyoibuka katika kikao cha Bunge cha mwezi Machi huko Arusha, sisi Wabunge wa Tanzania tulipokea maoni na masikitiko mengi kutoka kwa wana Afrika Mashariki na viongozi kwa ujumla wakitusihi kumaliza tatizo hili kwa njia ya amani na utulivu, lakini jitihada zetu ziligonga ukuta. Hatua hii ilizidi kutudhihirisha kuwepo kwa ajenda ya siri.


Ikumbukwe kuwa azimio la kutaka kumuondoa Spika madarakani awali lilipangiwa kuwasilishwa katika kikao cha Bunge la EALA cha mwezi Machi 2014 huko Arusha lakini liligonga mwamba baada ya kuibuka mabishano ya kisheria, hali iliyopelekea kuahirishwa kwa kikao hicho.

Hoja hii ililetwa tena kwenye vikao vingine vya EALA, lakini baada ya kutafakari kwa makini kuhusu chanzo halisi cha mzozo huu, idadi kubwa ya Wabunge kutoka Tanzania (7 kati ya 9) waliamua kwa pamoja kuipinga hoja hii kwani imekosa mashiko na haizingatii maslahi ya Tanzania na maslahi mapana ya jumuiya kwa ujumla.

Aidha, wabunge watatu wa EALA kutoka Tanzania ambao awali waliunga mkono hoja hii waliamua baadae kuipinga kwa kutoa sahihi zao kwa hiari yao wenyewe na walimwandikia barua Katibu wa Bunge wa EALA kumueleza maamuzi yao kwa mujibu wa utaratibu mnamo tarehe 29 Mei 2014. Barua hizo za Wabunge wa Tanzania wa EALA kutoa sahihi zao kwenye hoja hiyo zilipokelewa rasmi na Katibu wa Bunge.

Wabunge hao wa EALA kutoka Tanzania walitumia haki zao za kikanuni kuondoa sahihi zao kama inavyoeleza katika kanuni ya 9 (2) ya Kanuni na Utaratibu wa Uendeshaji wa Bunge (Rules of Procedure of the Assembly) inayosema: "Azimio la kumuondoa Spika madarakani halina budi kuambatana na sahihi zisizopungua nne kutoka kila nchi mwanachama."

Hoja yenyewe ya kumuengua Spika wa EALA ni batili kisheria kwa kuwa haikuwasilishwa Bungeni ndani ya siku 7 tangu ilipopelekwa kwa Katibu wa Bunge na pia imekosa sahihi za kuungwa mkono na wabunge wanne kutoka kila nchi mwanachama wa EAC kama kanuni zinavyotamka.

Uamuzi wa Wabunge wa EALA kutoka Tanzania kuondoa sahihi zao kwenye hoja hiyo ni lazima uheshimiwe na kila mtu kwa kuwa wanatekeleza haki yao ya kidemokrasia.

Tunaomba uongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ngazi zote ikiwemo Sekretarieti ya jumuiya kuheshimu maamuzi ya Wabunge wa EALA kutoka Tanzania. Ikumbukwe kuwa hapo awali, wabunge wa 5 wa EALA kutoka Tanzania kati ya jumla ya wabunge wote 9 wa Tanzania walionesha kuunga mkono hoja hii. Baada ya kubaini kuwepo kwa “mchezo mchafu” na ajenda ya siri, Wabunge watatu wa EALA kutoka Tanzania waliondoa sahihi zao na hivyo basi kufanya idadi kubwa ya Wabunge kutoka Tanzania (7 kati ya 9) kuipinga hoja hii batili.

Wabunge wa EALA wameshapoteza muda mwingi, fedha na rasilimali nyingine mpaka sasa kwenye hoja hii isiyo na tija ya kujaribu kumng'oa madarakani Spika wa EALA. Sasa hatuna budi kuweka jitihada zetu kwenye kazi muhimu ya kutetea maslahi ya raia wapatao milioni 140 wa Afrika Mashariki.

Hatuwezi kuwahudumia raia wa Afrika Mashariki kwa kuweka mbele ajenda za siri na kujishughulisha kwenye siasa za malumbano. Wananchi wa Afrika Mashariki wanataka kuona faida halisi kutoka kwenye jumuiya yao. Tuna imani na Spika wa sasa wa Bunge la EALA kuwa ni kiongozi sahihi wa kuongoza Bunge hilo.

Tunaamini kuwa hakuna tija yoyote kwa Wabunge wa EALA kuendelea kupoteza fedha za walipa kodi wa Afrika Mashariki kwa kujadili hoja hii batili. Badala yake, Wabunge wa EALA wana kazi ngumu ya kusimamia maslahi ya wananchi wa jumuiya wanaotaka kupata elimu bora, maji safi na salama ya kunywa, uhakika wa chakula, afya bora, miundombinu ya kisasa na maendeleo ya kiuchumi -- siyo siasa za ulaghai.

Tunatoa wito pia kwa Wabunge wenzetu wa EALA kutoka nchi nyingine wanachama na kwa viongozi wa Sekreterieti ya EAC kutojihusisha na ajenda zozote za siri za kujaribu kumng'oa Spika wa sasa wa EALA aliyepo madarakani kisheria. Wananchi wa Afrika Mashariki wanastahili zaidi ya hayo.

Njia pekee ya kufikia maslahi yetu ya pamoja ni kwa kutumia ushirikiano, badala ya kuendekeza malumbano na siasa za chuki na kututenganisha. Sisi Wabunge saba bado tunasisitizia AMANI NA UTULIVU kwani bila ya hivyo hakuna maendeleo na ustawi wa jamii.



Tamko hili limetolewa Dar es Salaam tarehe 9 Juni 2014 na Wabunge wafuatao:


Mhe. Adam Kimbisa, Mwenyekiti wa Wabunge wa EALA wa Tanzania

Mhe. Shy-rose Bhanji, Katibu wa Wabunge wa EALA wa Tanzania

Mhe. Charles Makongoro Nyerere, Mbunge wa EALA

Mhe. Maryam Ussi, Mbunge wa EALA

Mhe. Bernard Murunya, Mbunge wa EALA

Mhe. Twaha Taslima, Mbunge wa EALA

Mhe. Angellah Kizigha, Mbunge wa EALA



________________________
Mwenyekiti, Wabunge wa EALA wa Tanzania



________________________
Katibu, Wabunge wa EALA wa Tanzania



________________________
Mwanasheria, Wabunge wa EALA wa Tanzania
 
Mkitaka kuwajua wanyarwanda kwa kuplot vitu ingieni jukwaa la kimataifa.Kama waliweza kumwambia Kikwete mhutu watashindwa kumtengenezea huyo mama.Huyu mama anawasumbua sana bungeni mule.

Kuwa na aibu boss...Nadhani unajaribu kutetea usichokijua.Hata kama amekulipa ufanye hivyo nadhani dhamila inakusuta. Shortly kumtetea Shyrose kwa hizi skendo zake ni sawa na kujaribu kuziba jua kwa kiganja cha mkono.Tanzania inaabishwa na wapuuzi wachache kama huyu.... Still mtu bila haya eti anajenga utetezi....Shame upon you na huyo mpuuzi wenu...
 
Yani mnamsulubisha Mtanzania mwenzenu bila hata kuwa na ushahidi wakati anaitetea Tanzania?!

Yaan sie tuna matatizo kila sehemu.. Imagine mtu analeta tuhuma hapa na hawa wanaojiita GT wanazipokea na kuziamini bila ya kutaka kujua upande wa pili.. Fikiria kuna member kaandika na ninamnukuu "Kachelewa kukanusha, kwangu mie nimeamini kile kilichosemwa awali"!.. Mwingine hata hamjui huyo anaetuhumiwa lakini kwa unafiki anatengeneza stori ya kuendelea kumuua anaetuhumiwa..! Ujinga tu..
 
Kuna mwendesha semina mmoja pale Mlimani City alikazana kuwaambia wanasemina wake "MNAPASWA KUWAZA NJE YA BOX".....Mmoja wa wanasemina alikerwa na kurudiwa rudiwa kwa kauli hiyo, akamuomba mseminishaji aeleze nini maana ya kuwa ndani ya box, nini maana ya kuwaza nje ya box na kwa namna gani mtu anawaza ndani au nje ya box...!! Bahati mbaya mseminishaji alishindwa kutoa ufafanuzi...kwa lugha nyepesi ailonekana kakariri msemo huo bila kuuelewa..macho_mdiliko ebu anzisha uzi mhususi utoe mhadhara juu usemi huo-KUWAZA NJE YA BOX
Labda uniambia una tatizo na lugha ya kiingereza, lakini mimi nafikiri kama hujui maana yake uki-google sekunde moja utakuwa umejua kila kitu. Wewe unafikiri mimi naandika kitu cha kukariri kama mlivyozoea kukariri kwenye shule za bongo?
Nenda hapa....
Thinking outside the box - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Dah!! Hii nchi ni kubwa kwa kweli.Si niliskia mahakama ilitengua ubunge wa wabunge wote toka nchi ya kusadikika akiwemo huyu anaebwabwaja hapa,kwani wamerudishwa lini??
 
hili bunge la EALA linatofauti gani na BMK la CCM lililohitimika hivi karibuni? THINK OUTSIDE THE BOX!
 


Mimi Shy-Rose Bhanji, Mbunge wa Afrika Mashariki-Tanzania, ninapinga vikali na kwa nguvu zote shutuma zilizotolewa dhidi yangu kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.
Shutuma hizi hazina ukweli wowote na zinalenga, si kuniharibia, bali kuchafua sifa yangu na utendaji kazi wangu katika Bunge la Afrika Mashariki.
Lengo kuu la shutuma hizo ni kunivunja nguvu na ari ya kutetea maslahi ya nchi yangu na Watanzania wenzangu kwani daima nimekuwa kikwazo na mwiba kwenye ajenda zinazokiuka maslahi ya Tanzania.
Kwa mfano ardhi ya Tanzania kugawiwa kwa wana Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kinyume na Sera ya Tanzania. Nimekuwa miongoni mwa wabunge wa Tanzania tulio mbele katika kulipinga suala hilo. Sishangai likinijengea uadui.
Isitoshe, kwenye ajenda ya kumuondoa madarakani Spika wa EALA, Dk. Margaret Zizziwa, nilisimama kidete kwa kutounga mkono kwa sababu halikuwa na maslahi ya Tanzania na yalikuwa kinyume na malengo ya ushirikiano wa Jumuiya nzima.
Hoja ya kumuondoa Spika ilikuwa ni sehemu ya ‘mchezo mchafu’ ya ajenda ya siri ya kumweka kwenye nafasi hiyo mjumbe mwingine kwa maslahi ya wachache.
Jaribio hili la kumuondoka Spika lilifanywa na kushindikana mara tatu baada ya kukosa sahihi za kutosha kutoka Tanzania, ikiwamo ya kwangu.
Baada ya kampeni ya kumwondoa Spika kushindwa, wabunge kadhaa walikuwa wanasusia vikao vya Bunge wakati wameshachukua posho za vikao. Kwa mfano kikao kilichofanyika hivi karibuni hapa Dar es Salaam.
Malumbano ndio yamekuwa yakitawala na kuinyima Bunge akidi ya kuendelea na ajenda za mtangamano. Huu ni usaliti wa wazi kwa nchi zilizowachagua na kuwatuma katika Bunge la EALA.
Ukijaribu kuwaasa kwamba mwenendo huo si sahihi, unageuka kuwa adui.
Na sasa wameamua kunitukana na kuzusha tuhuma kadhaa kupitia mitandao ya kijamii ambako yote ni utunzi wa kisanii usiokuwa na chembe ya ukweli, uhalali wala ushahidi.
Wahenga walisema ‘akutukanaye hakuchagulii tusi’. Walete ushahidi wa tuhuma zote dhidi yangu.
Kwa mfano, shutuma kwamba nililewa pombe ndani ya ndege, kuvunja chupa, kufanya fujo na kufungwa pingu wakati wa safari ya Ubelgiji si kweli hata kidogo.
Kama hizi tuhuma ni za kweli, kwanini hazikupelekwa polisi, serikalini au vyombo vingine vya sheria baada tu ya tukio?
Ijewe wamesubiri wiki mbili baada ya madai hayo ya tukio la kutunga ndipo wajitokeze wakati wa kikao kinachoendelea mjini Kigali, Rwanda? Kwanini wasubiri kikao cha Kigali ndipo uzushi huu utolewe?
Tuhuma kwamba nimewatukana marais wa nchi tatu hazina mashiko isipokuwa kuhalalisha kampeni ya wale wanaonichafua na kuibua chuki kwa maraisi na raia katika nchi za Kenya, Rwanda na Burundi.
Ninayo heshima kubwa sana kwa marais wa nchi zote tano na raia wa nchi wanachama ambako mara zote nimepokewa na kuishi kwa amani na upendo katika nchi hizo. Naahidi kuedeleza heshima hii.
Hainiingii kichwani ni wapi nilipoteza heshima hii isipokuwa kwa wale wasionitakia mema ambao wamekusudia kufanikisha ajenda zao.
Shutuma zote dhidi yangu zimetengenezwa na watu ambao hatushabihiani katika hoja zetu na sishangai kwa hilo.

Mimi ni Mtanzania na ni Mbunge wa Tanzania. Hivyo nina wajibu wa kulinda na kutetea maslahi ya Watanzania ili kuleta mtangamano wenye uwiano sawa kwa nchi zote wanachama.

Ninaahidi nitaendelea kuwatumikia Watanzania kwa nguvu zangu zote na kutoa ushirikiano kwa wabunge wengine wa EALA kwa manufaa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Nimeyasema haya nikiamini kuwa: “Uongo ukiachwa usemwe mara nyingi unaweza kuaminiwa kuwa ni ukweli.”
Mungu ibariki Afrika MasharikiUmoja Wetu ni Nguzo Yetu





huu utakuwa mpango wa komu na genge lake la chagadema tangu akose ubunge wa eac
 
Yani mnamsulubisha Mtanzania mwenzenu bila hata kuwa na ushahidi wakati anaitetea Tanzania?!

Huyo haitetei Tanzania ispokuwa anaiaibisha .... Siyo lazima uandike hapa.. Unaweza ukasoma tu na kubaki kimya. Kama unaona kaonewa nenda kampe pole....
 
sidhani kama kuna mtu yeyote atafanya fujo kama ilivyo daiwa ndani ya ndege na asikamatwe na polisi mara tu anapofika iendako - kawaida pilot anawajulisha polisi mapema kuwa kuna mtu anafanya fujo na huwa wanamsubri mlangoni mara tu ndege inapotuwa hutiwa mbaroni na kufunguliwa mashataka ya kuharibu amani akiwa ndani ya ndege,. Hizi habari hazina ukweli

Mkuu umeeleza vizuri. Isingewezekana kwa abiria uyafanye yote aliyoyaandika mleta tuhuma wa kwanza kumhusu mama Bhanji ukose kufikia mikononi mwa polisi mara ndege ikitua. Ulewe ndani ya ndege hadi uwekwe pingu na maafisa usalama ndani ya ndege,uvunje chupa ya pombe, uwatukane maraisi wote wa nchi za jumuiya na mamlaka husika zikuache tu huu ni uongo wa kumharibia sifa huyu mama. Nakubaliana na utetezi wake na wachangiaji muwe na lugha za staha kwa viongozi wetu hamuwezi kumwandika eti akilewa havai chupi. Hizo sio lugha za jukwaa hili na huna ushahidi wa hilo.
 
Huyo haitetei Tanzania ispokuwa anaiaibisha .... Siyo lazima uandike hapa.. Unaweza ukasoma tu na kubaki kimya. Kama unaona kaonewa nenda kampe pole....

angekuwa amezushiwa mbowe ungeshinda humu na mke wako mkimtetea
 
Mimi mwanachadema ninakuunga mkono shy rose kwa asilimia 100%. Wewe ni kamanda letu wa ukweli!
 
Kwanza bunge lenyewe halina tija...
 
Mambo ya wanasiasa wanajua wanasiasa. Hatahivyo, huwezi kuzusha mtiti ndani ya ndege halafu usikamatwe baada ya kutua.
 
Yaan sie tuna matatizo kila sehemu.. Imagine mtu analeta tuhuma hapa na hawa wanaojiita GT wanazipokea na kuziamini bila ya kutaka kujua upande wa pili.. Fikiria kuna member kaandika na ninamnukuu "Kachelewa kukanusha, kwangu mie nimeamini kile kilichosemwa awali"!.. Mwingine hata hamjui huyo anaetuhumiwa lakini kwa unafiki anatengeneza stori ya kuendelea kumuua anaetuhumiwa..! Ujinga tu..

Hizi siyo tuhuma.Huo ndo ukweli.Kaishachafuka hasafishiki hata kwa JIKI....
 
Back
Top Bottom