Jamaa Fulani Mjuaji
Member
- Jul 25, 2020
- 65
- 125
Hii nimekuwa nikijiuliza sana, ukimsikiliza kiongozi yeyote hasa Mawaziri wa TAMISEMI wanajinasibu kuwa shule zote zimepokea pesa ya ukarabati na wanajinasibu kwa kudai kuwa hakuna shule ambayo haijapata pesa za kujenga madarasa mapya au kukarabati yaliyopo lakini kuna shule kongwe hazijawahi kuguswa kabisa zipo ukipita baadhi ya shule utawaonea huruma hasa sekondari za kata na shule za msingi za vijijini shule zina hali mbaya sana.
Madirisha kama milango na baadhi ya shule madarasa yameshikiriwa na nguzo za miti ili kuta zisianguke ila ni ajabu waziri wa tamisemi na watendaji wake wanasema wamejenga nchi nzima.
Mbaya zaidi ni kila ukijaribu kufuatilia kuwa hizi shule kwanini hazikarabatiwi ukiachana na watoto kukaa chini kwa sababu ya kukosa madawati ila tu hata kupiga sakafu angalau watoto wasikae kwenye mchanga na vumbi au kwenye mawe unaambiwa kuwa hili jambo liache kama lilivyo au wanasema utoe taarifa wewe kama nani.
Nitakuja na taarifa fupi ya research ilofanywa na taasisi fulani na ushahidi kuanzia mwakani maana kuna mahali shule madarasa mengi yamejaa vumbi na watoto wanakaa juu ya mawe na wadau walijaribu kupendekeza kuwa kwanini tusiombe kuitisha harambee ili waalikwe wadau mbalimbali ili wachangie shule angalau ipate mifuko hata 200 ya cement ili angalau vyumba vya madarasa vikarabatiwe.
Ila jambo la ajabu ni kwamba, unaambiwa mbunge au diwani wa eneo husika anakasirika ikionekana kuna mtu nje ya chama amepeleka hata mifuko ya cement bila yeye kuhusishwa na hata ukimhusisha kuwa tukualike kwenye harambee kuchangia ujenzi wa shule kalenda zinakua nyingi na kupiga chenga kwa sababu hawataki kuchangia maendeleo.
Kwa maana kwamba ili mdau yeyote akitaka kufanya jambo lazima wanasiasa hawa wahusike ili nao waonekane wako kwenye chain wapate fagio.
Mbunge yeye kaamua kukaa dar au dodoma ila mtu akianzisha alambee eneo lake kuchangia maendeleo hata kama ni ujenzi wa shule anaonekana adui wa mbunge anataka kupoka jimbo.
Kuna wadau wengi wako nje wanatamani kuchangia maendeleo ila yanakwama kwa sababu ili utoe pesa yako lazima ipitie kwa wanasiasa wapate kujioshea ili waonekane na wao wamehusika hata kama alishasahau kabisa eneo lake.
Kwa mtazamo wangu mambo kama haya yanavunja moyo wadau walio tayari kuchangia maendeleo na kuchelewesha maendeleo pengine kusingekua na huu ukiritimba maeneo mengi sana yangekua na maendeleo hasa kwenye haya maeneo ya shule za watoto zetu.
Kero yangu | mtazamo wangu | mjumbe hauwawi.