Shule zafungwa Ufaransa kwasababu ya Kunguni

Wazungu wanajua kudeka na kijidekeza, sina kumbukumbu km kuna shule ya bweni hizi za serikali hapa nchini kwetu ambayo haina kunguni. Kunguni wanauzi na niwasumbufu ila wanatoka kiwepesi mno ukiamua kupambana nao kiume. Haizidi cku mbili kuwaondosha ndani ya nyumba
Maji ya moto! jua Kali!!!
 
Waziri wa Elimu wa Ufaransa Gabriel Attal ametangaza kuwa nchi hiyo imelazimika kufunga shule saba zinazowapokea wanafunzi wapatao 1,500 baada ya kuvamiwa na kunguni.

Mapema wiki hii, mamlaka ya Paris ilitangaza kufungwa kwa shule mbili kwa sababu ya kunguni, moja huko Marseille na nyingine Villefranche-sur-Saone nje kidogo ya mji wa kusini mashariki wa Lyon.

Serikali ya Ufaransa imefanya msururu wa mikutano wiki hii kuchunguza idadi inayoongezeka ya visa vya kunguni, wakati nchi hiyo ikiandaa Kombe la Dunia la Rugby na ambayo itakuwa mwenyeji ya Michezo ya Olimpiki hapo mwakani.

Serikali mjini Paris imelazimika sasa kuingilia kati kupambana na kunguni hao. Ijumaa iliyopita, Waziri Mkuu wa Ufaransa Elisabeth Borne aliitisha kikao cha baraza la mawaziri kujadili namna ya kupambana na kunguni.

Takwimu za Shirika la Afya na Usalama wa Chakula nchini Ufaransa zinaonesha kuwa angalau nyumba moja kati ya kumi nchini humo ilikuwa na kunguni katika miaka michache iliyopita. Kuwatokomeza kunguni inagharimu pesa nyingi na wakati mwingine zoezi hilo hurudiwa mara kadhaa.

Kunguni wameripotiwa sehemu mbalimbali nchini Ufaransa kama kwenye treni za mwendo kasi katika mji mkuu Paris, na hata katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Charles De Gaulle.

Kunguni ni mdudu mdogo asiyeweza kuruka bali anayeweza kutembea haraka kutoka sehemu moja hadi nyingine au hata nchi hadi nchi, na imekuwa vigumu kumtokomeza kwa kutumia dawa za kuulia wadudu. Lakini pia, kunguni anaweza kuishi hata mwaka mzima bila kula.


DW Swahili
Walikataa mavazi yanayompendezesha mungu kwaa mwanamke kwa kutaka kuangalia mapaja. Sasa mungu anawapiga na kitu kizito kunguni kila mahala. M/mungu ni mkubwa sana
 
Back
Top Bottom