"Shule za vipaji maalum" inamanisha nini hasa?

"Shule za vipaji maalum" inamanisha nini hasa?

Nimebahatika kusoma Mzumbe. Aisee, kule kuna inteligent creatures. Swali ambalo mtu wa kawaida anaweza lisolve kwa wiki tatu, kipanga wa Mzumbe analisolve kwa dk 15. Kuna watu wana akili, acha tu.
Dakika 15 mbona nyingi sana mkuu Dakika sifuri
 
Zile ni shule ambazo hua zinachukua wanafunzi wenye ufaulu wa juu..hakuna kingine zaidi ya hcho.
Kwa form one kila mkoa unapewa nafasi za wanafunzi kwenda kwenye hzo shule..kwa mfano unaweza ukawa na marks nyingi kwenye mkoa fulani kuliko mwanafunzi wa mkoa mwingine na bado usiende kama nafasi za mkoa wako zimeshachukuliwa na wengine..
Kwa form five mara nyingi wanaangalia ufaulu kwenye mchepuo wa mwanafunzi naoenda kusoma lakini mara nyingi wanachukua wenye dision one kuanzia ya 7-14 ikitegemeana na ufaulu wa mwaka husika, na mara nyingi cut point zinakua 3-4 kwa pcm yaan AAB na kwa pcb wanachukuaga mpaka 5 huku kigezo cha kupata one 7-13 au 14 kikizingatiwa..so unaweza ukawa umepata one ya 13 lakini kwa bahati mbaya ukawa na CCC Kwenye mchepuo wa pcb kwa mfano na unataka kusoma huo mchepuo basi automatically unajikuta umekosa nafasi kwenye hzo shule na mwenzako mwenye one ya 14 lakin kwenye pcb akawa na AAB akapata nafasi.
KWANINI HUWA WANAFAULU KWA WINGI KWENYE MITIHANI YA TAIFA
1.Aina ya wanafunzi wanaosoma kwenye hzo shule wanakua wanajengewa mazingira ya kusoma kwa ushindan mkubwa sana..kwa mfano ushindan wa
kua kwenye chumba fulani cha darasa kulingana na ufaulu wa mitihan ya ndani..
2.Aina ya mitihan ya ndani inayoandaliwa kwenye hzo shule inakua migumu kuliko hata NECTA..Hii inawafanya wanafunzi siku zote kusoma kwa bidii ili kufaulu..kwa mfano mitihani kama GAUGING Kwa wale wale waliosoma Mzumbe wanaweza eleza hii kitu inavyokimbizaga kwenye chumba cha mtihani
3.Mahusiano mazuri kati ya wanafunzi na walimu..hii inachangia sana wanafunzi kufaulu..mara nyingi kunakuaga hakuna adhabu zisizo za msingi zinazoweza mpotezea muda mwanafunzi..Enzi hzo nakumbuka kulikua hakuna adhabu kama fimbo kwa mwanafunz
4.Matokeo ya waliokutangulia mbele pia yanakua yanakupa hamasa ya kufaulu, Kwa mfano unafika form one tu unakuta kwenye notes board wadau waliomaliza form 4 wamepiga one za kutosha tu.
Walimu na vitu vingine vinakua kama shule zingine tu na kama usipojituma kufeli inaweza kuwa jambo rahisi zaidi.
Well explanation mkuu
 
Malengo ya shule hizo yameharibiwa na serikali zilizokuwepo madarakani, mwisho wa siku yakabaki majina tu "shule za vipaji maalumu"...
 
Malengo ya uanzishwaji wa shule hizo yameharibiwa na serikali zilizokuwepo madarakani, mwisho wa siku yakabaki majina tu "shule za vipaji maalumu"...
 
Wkt ule tunafanya masomo ma3, best yangu alipata 127 akaenda Mzumbe, mi nikabaki shule ya wilaya yetu na 121 yangu! The end justifies the means.. Jamaa yangu alipofikia nikisema itakuwa namsimanga!
Waliosoma Zamani Kwa kweli ilikuwa shida jamaa alipata maksi 120 lakini hakuchaguliwa shule yeyote na ndiyo shule iliishia hapo.Ashukuriwe aliyebuni wazo la Kata school japokuwa utekelezaji wake unasuasua
 
Nimebahatika kusoma Mzumbe. Aisee, kule kuna inteligent creatures. Swali ambalo mtu wa kawaida anaweza lisolve kwa wiki tatu, kipanga wa Mzumbe analisolve kwa dk 15. Kuna watu wana akili, acha tu.
Fedha ni kipaji maalum au siyo kipaji maalum?
 
Kipaji ni uwezo wa kufanya jambo juu ya uwezo wa wengi. Wanafunzi wanaoenda kwenye hizi shule kama MZUMBE, ILBORU , TABORA BOYS, KIBAHA, MSALATO, TABORA GIRLS n.k wengi wao wana uwezo mkubwa (kipaji) ama wa kufikiri au kukariri.

Kuna jamaa yangu alisoma TABORA BOYS alikuwa na uwezo wa kufikiri na ku solve swali la hesabu hata kama hajawahi kujifunza topic husika. Atatumia njia yoyote kulitatua swali.Alikuwa hasomi sana.

Jamaa yangu mwingine alisoma MZUMBE, Alikuwa na uwezo wa kukariri REVIEWS ZOTE maswali na majibu, yakiisha anatafuta mengine kwenye S.CHAND, google na hata shule jirani, yaani ukimletea swali linalofanana na lile alilowahi kuliona hakosi. Ila ukimletea jipya kulipata ni vigumu, hasa kama hana concept yoyote. Mda mwingi alikuwa anasoma na kutafuta maswali mengi na kukariri.

A talented student can either be a GENIUS, INTELLIGENT or BOTH.
 
Kwa hiyo nikisoma shule ya kata na nikapata one nzuri shule yangu ya kata itakua shule ya vipaji maalum?
Kwa point zinazotumika hapa za Kata nazo zitakuwa za Vipaji maalum maana kuna vijana ni magenious licha ya mazingira magumu ya kujifunza lakini Huwa wananyoosha A kadhaaa
 
Wanaoingia kwenye shule za Vipaji maalum Huwa wote wanahitimu wakiwa na vipaji maalum?
 
Haha,I have been there br NO CHEATING ,ndio maana hawapati one wote nakuhakikishia wangepata treatment km za feza au marian 99% wangekuwa na one...mostly ni msuli ukiwa br
Sasa wanashindwaje kupata one ilihali wana vipaji maalum?
 
Matokeo sio siri kwa olevel gvt ni majanga,hakuna shule hata moja ya kata 50% wamepata one,labda sio TZ,na za kata almost zote ni olevel,sa sijui yako ipi?kwa wanaopata 4 na 0 special hawasomi,au kuumwa,panic etc na ni % ndogo
Hizo shule za Kata zingekuwa na mazingira kama ya hizo za Vipaji maalum nadhani nazo zingefaulisha sana
 
Wanaoingia kwenye shule za Vipaji maalum Huwa wote wanahitimu wakiwa na vipaji maalum?
Hiyo ndo changamotoo kubwaa hasa Kama MTU alieenda shule ya Kipaji maalumu kwa Kubebwaa aisee atapataa tabuu sanaaa.... Unamuua kisaikolojiaa mwanafunzi bora umpeleke kwenye level zakee...!! MTU anakata tamaa kabisa na kujiona hawezii maana kwanza wengi wanafunzi wa vipaji maalumu ndoto zao ni PCM NA PCB sasa ukija kujikutaa huna uwezo huoo ni nomaa Sanaaa lazima uathirikee kisaikolojiaa piaa utakataa tamaa Sana.. Na waalimu huwa wanafundisha Kama wanafundisha watu wanaojua kinachofundishwa hata Kama ndo siku ya Kwanzaa akiamini wanafunzi mtaenda kujisomea zaidiii... So sehemu kubwa ya elimu katika shule za vipaji ni KUJITAFUTIA mwanafunzi mwenyewee....
 
Zile ni shule ambazo hua zinachukua wanafunzi wenye ufaulu wa juu..hakuna kingine zaidi ya hcho.
Kwa form one kila mkoa unapewa nafasi za wanafunzi kwenda kwenye hzo shule..kwa mfano unaweza ukawa na marks nyingi kwenye mkoa fulani kuliko mwanafunzi wa mkoa mwingine na bado usiende kama nafasi za mkoa wako zimeshachukuliwa na wengine..
Kwa form five mara nyingi wanaangalia ufaulu kwenye mchepuo wa mwanafunzi naoenda kusoma lakini mara nyingi wanachukua wenye dision one kuanzia ya 7-14 ikitegemeana na ufaulu wa mwaka husika, na mara nyingi cut point zinakua 3-4 kwa pcm yaan AAB na kwa pcb wanachukuaga mpaka 5 huku kigezo cha kupata one 7-13 au 14 kikizingatiwa..so unaweza ukawa umepata one ya 13 lakini kwa bahati mbaya ukawa na CCC Kwenye mchepuo wa pcb kwa mfano na unataka kusoma huo mchepuo basi automatically unajikuta umekosa nafasi kwenye hzo shule na mwenzako mwenye one ya 14 lakin kwenye pcb akawa na AAB akapata nafasi.
KWANINI HUWA WANAFAULU KWA WINGI KWENYE MITIHANI YA TAIFA
1.Aina ya wanafunzi wanaosoma kwenye hzo shule wanakua wanajengewa mazingira ya kusoma kwa ushindan mkubwa sana..kwa mfano ushindan wa
kua kwenye chumba fulani cha darasa kulingana na ufaulu wa mitihan ya ndani..
2.Aina ya mitihan ya ndani inayoandaliwa kwenye hzo shule inakua migumu kuliko hata NECTA..Hii inawafanya wanafunzi siku zote kusoma kwa bidii ili kufaulu..kwa mfano mitihani kama GAUGING Kwa wale wale waliosoma Mzumbe wanaweza eleza hii kitu inavyokimbizaga kwenye chumba cha mtihani
3.Mahusiano mazuri kati ya wanafunzi na walimu..hii inachangia sana wanafunzi kufaulu..mara nyingi kunakuaga hakuna adhabu zisizo za msingi zinazoweza mpotezea muda mwanafunzi..Enzi hzo nakumbuka kulikua hakuna adhabu kama fimbo kwa mwanafunz
4.Matokeo ya waliokutangulia mbele pia yanakua yanakupa hamasa ya kufaulu, Kwa mfano unafika form one tu unakuta kwenye notes board wadau waliomaliza form 4 wamepiga one za kutosha tu.
Walimu na vitu vingine vinakua kama shule zingine tu na kama usipojituma kufeli inaweza kuwa jambo rahisi zaidi.
Exactly!na wengi malengo yao kwa olevel ni kuwa TO au kupata one ya single digit (7_9),mtu mwenye malengo makubwa hata akiteleza bado atafanya vizuri tu
 
Back
Top Bottom