"Shule za vipaji maalum" inamanisha nini hasa?

"Shule za vipaji maalum" inamanisha nini hasa?

Kipaji ni uwezo wa kufanya jambo juu ya uwezo wa wengi. Wanafunzi wanaoenda kwenye hizi shule kama MZUMBE, ILBORU , TABORA BOYS, KIBAHA, MSALATO, TABORA GIRLS n.k wengi wao wana uwezo mkubwa (kipaji) ama wa kufikiri au kukariri.

Kuna jamaa yangu alisoma TABORA BOYS alikuwa na uwezo wa kufikiri na ku solve swali la hesabu hata kama hajawahi kujifunza topic husika. Atatumia njia yoyote kulitatua swali.Alikuwa hasomi sana.

Jamaa yangu mwingine alisoma MZUMBE, Alikuwa na uwezo wa kukariri REVIEWS ZOTE maswali na majibu, yakiisha anatafuta mengine kwenye S.CHAND, google na hata shule jirani, yaani ukimletea swali linalofanana na lile alilowahi kuliona hakosi. Ila ukimletea jipya kulipata ni vigumu, hasa kama hana concept yoyote. Mda mwingi alikuwa anasoma na kutafuta maswali mengi na kukariri.

A talented student can either be a GENIUS, INTELLIGENT or BOTH.
The end(kufaulu) justifies the means (kumeza/kukariri au kufikiri), ila vyote vina sehemu yake
 
Kipaji ni mtu sio shule,kwa muktadha wa shule za vipaji ni zinazochukua wenye ufaulu wa juu...so kwa mantik hiyo kunaweza kuwa na 'vipaji maalum' ata kwenye shule za kawaida ndioo maana sio wote waliosoma special olevel watasoma special advance,ni survival.for the fittest, tena sometimes hata 50% ya darasa itayomaintain kubaki special inaweza isifike
 
Kule vipaji hakuna hata kufundishwa sana, Tabora Boys mwalimu wa Geography aliondoka ulikuwa mwendo wa discussion na msuli tu

Hivi hata geog ni somo linalohitaji kufundishwa???? mimk masomo yanayohutaji kufunzwa ni Math na Phys tu
 
Malengo ya shule hizo yameharibiwa na serikali zilizokuwepo madarakani, mwisho wa siku yakabaki majina tu "shule za vipaji maalumu"...
Ni kweli kwa mfano school motto ya ilboru ni EDUCATION FOR SERVICE, uelimishwe uihudumie jamii kwa kuleta positive change sasa serikali haiweki mkazo huko badala yake mtu anakomalia kufaulu tu,na ugali wake....kibaha motto imebase zaidi kwa individual person 'STRUGGLE FOR SUCCESS' na ndo real what is going on,watu wanastruggle kweli kweli kwenye zinazoitwa special schools
 
Hivi mbali na kuangalia tu ufaulu wa wanafunzi kwenye mtihani wao waliofanya ni vipaji gani vingine vinavyoangaliwa kabla ya kumchagua mwanafunzi na kumpeleka kwenye hiyo shule ya "vipaji" maalumu? Maana bila ufaulu mzuri hata kama mwanafunzi anavyo vipaji vingine mfano kuimba, kupiga chombo/vyombo vya muziki, kukimbia, sarakasi n.k. hawezi kuchaguliwa kujiunga na shule hizo.

Badala ya kuitwa shule ya vipaji maalumu pengine zingeitwa shule kwa wenye ufaulu wa kipekee. Vinginevyo pasipo kuangalia ufaulu pekee yake wachukuliwe na wale wenye vipaji kama nilivyotaja hapo juu na kuwaweka pamoja ili kuleta maana halisi ya vipaji maalumu.

Nakumbuka wakati nachaguliwa kwenda kuanza form one Kibaha Secondary mwaka 2003 kutoka wilaya ya temeke tulikuwa wanafunzi wanne na iliandikwa "waliochaguliwa shule ya vipaji maalum kiakili" bold neno KIAKILI
 
Write your reply...uzi huu mwanzoni ulionekana wa kawaida na watu wakatoa majibu rahisi na kulazimisha ufungwe.Ila kwa unavyoendelea uzi huu umekaa kifalsafa hasa na unafikirisha.
 
Back
Top Bottom