"Shule za vipaji maalum" inamanisha nini hasa?

"Shule za vipaji maalum" inamanisha nini hasa?

Mental talent ni za kina Isaac Newton..hawa hapa bongo ni wenye uwezo mkubwa wa kufaulu mitihani yao vizuri
Huenda ata bongo zingekuwepo ila system ya elimu yetu imebase kwenye ufaulu mitihani tu,kuwasoma hao kina Newton....
 
Hakuna shule kipaji (majengo kipaji haha) ni wanafunzi wanaopelekwa hapo ndio vipaji na mizani yake au SI unit kibongobongo ni outstanding performance
Sasa kama kipaji SI unit yake ni kufaulu, kwann hutaki niite shule yangu ya kata (ilinifaulisha) shule vipaji?
 
Sasa kama kipaji SI unit yake ni kufaulu, kwann hutaki niite shule yangu ya kata (ilinifaulisha) shule vipaji?
Km shule ndio imekufaulisha mngefaulu wote,sasa darasa lina wanafunzi 100 div 1 zipo 3!tuiite shule ya vipaji kweli?
 
Km shule ndio imekufaulisha mngefaulu wote,sasa darasa lina wanafunzi 100 div 1 zipo 3!tuiite shule ya vipaji kweli?
Una uhakika gani tulikua 100? Na una uhakika gani hatukupata div one? Je hizo shule zako unazoziita za vipaji maalum hawana div 4 na zero? Kama kufaulu ni kipaji, kwann basi uendelee kuziita shule za vipaji ilhali wana div zero na four?
 
Hawa akina newton ni moja ya wenye "vipaji maalum"...hii kukariri na kuiba mitihan si kipaji maalum.
Haha,I have been there br NO CHEATING ,ndio maana hawapati one wote nakuhakikishia wangepata treatment km za feza au marian 99% wangekuwa na one...mostly ni msuli ukiwa br
 
Una uhakika gani tulikua 100? Na una uhakika gani hatukupata div one? Je hizo shule zako unazoziita za vipaji maalum hawana div 4 na zero? Kama kufaulu ni kipaji, kwann basi uendelee kuziita shule za vipaji ilhali wana div zero na four?
Ili ufaulu ni LAZIMA usome kwa elimu ya bongo (labda km utaibia,na kuibia lazima uwe na kitu kichwani) sasa km husomi utafeli tu hakuna namna....ubaya zamani shule za gvt hawafwatilii sana ujitambue mwenyewe tu,usipojielewa UTAFELI TU
 
Hujajibu swali. Soma maswali uyajibu yote, kama huwezi kaa kimya.
 
Ni kuwatofautisha tu kutokana na marks zao ili kuwapa morali na wanafunzi wengine huku wapambane
 
Hujajibu swali. Soma maswali uyajibu yote, kama huwezi kaa kimya.
Matokeo sio siri kwa olevel gvt ni majanga,hakuna shule hata moja ya kata 50% wamepata one,labda sio TZ,na za kata almost zote ni olevel,sa sijui yako ipi?kwa wanaopata 4 na 0 special hawasomi,au kuumwa,panic etc na ni % ndogo
 
Hujajibu swali. Soma maswali uyajibu yote, kama huwezi kaa kimya.
Huo ni mfano tu,kwan mi najua ulisoma wapi na mlikuwa wangap?ila umesema shule ya kata na reality kwa bongo hakuna asiyejua matokeo,its a fact
 
Zile ni shule ambazo hua zinachukua wanafunzi wenye ufaulu wa juu..hakuna kingine zaidi ya hcho.
Kwa form one kila mkoa unapewa nafasi za wanafunzi kwenda kwenye hzo shule..kwa mfano unaweza ukawa na marks nyingi kwenye mkoa fulani kuliko mwanafunzi wa mkoa mwingine na bado usiende kama nafasi za mkoa wako zimeshachukuliwa na wengine..
Kwa form five mara nyingi wanaangalia ufaulu kwenye mchepuo wa mwanafunzi naoenda kusoma lakini mara nyingi wanachukua wenye dision one kuanzia ya 7-14 ikitegemeana na ufaulu wa mwaka husika, na mara nyingi cut point zinakua 3-4 kwa pcm yaan AAB na kwa pcb wanachukuaga mpaka 5 huku kigezo cha kupata one 7-13 au 14 kikizingatiwa..so unaweza ukawa umepata one ya 13 lakini kwa bahati mbaya ukawa na CCC Kwenye mchepuo wa pcb kwa mfano na unataka kusoma huo mchepuo basi automatically unajikuta umekosa nafasi kwenye hzo shule na mwenzako mwenye one ya 14 lakin kwenye pcb akawa na AAB akapata nafasi.
KWANINI HUWA WANAFAULU KWA WINGI KWENYE MITIHANI YA TAIFA
1.Aina ya wanafunzi wanaosoma kwenye hzo shule wanakua wanajengewa mazingira ya kusoma kwa ushindan mkubwa sana..kwa mfano ushindan wa
kua kwenye chumba fulani cha darasa kulingana na ufaulu wa mitihan ya ndani..
2.Aina ya mitihan ya ndani inayoandaliwa kwenye hzo shule inakua migumu kuliko hata NECTA..Hii inawafanya wanafunzi siku zote kusoma kwa bidii ili kufaulu..kwa mfano mitihani kama GAUGING Kwa wale wale waliosoma Mzumbe wanaweza eleza hii kitu inavyokimbizaga kwenye chumba cha mtihani
3.Mahusiano mazuri kati ya wanafunzi na walimu..hii inachangia sana wanafunzi kufaulu..mara nyingi kunakuaga hakuna adhabu zisizo za msingi zinazoweza mpotezea muda mwanafunzi..Enzi hzo nakumbuka kulikua hakuna adhabu kama fimbo kwa mwanafunz
4.Matokeo ya waliokutangulia mbele pia yanakua yanakupa hamasa ya kufaulu, Kwa mfano unafika form one tu unakuta kwenye notes board wadau waliomaliza form 4 wamepiga one za kutosha tu.
Walimu na vitu vingine vinakua kama shule zingine tu na kama usipojituma kufeli inaweza kuwa jambo rahisi zaidi.
 
Kipaji maalumu ndio Special school? Je shule zenye uhitaji maalum nazo ni special? Kila mwanafunzi ni special whether umesoma Nyamisati or Mzumbe,kufaulu mtihani kuna factors nyingi e.g mtihani umekuja angle yako,haujapanic,umepata feki,umenunua majibu etc
 
Back
Top Bottom