Shule za miaka ya 1980 na 1990 mwanzoni

Shule za miaka ya 1980 na 1990 mwanzoni

Nimekuwa nikizikumbuka shule za miaka ya 80 na 90 ambazo kila mzazi alitamani mwanae asome mojawapo kati ya hizo. Mimi binafsi nilifaulu std VII kwenda Mawenzi sec Moshi lakini mzee wangu alinihamishia Umbwe mapema sana, hiyo ilikuwa 1992. Najiuliza kipindi kile shule hizi zilikuwa na nini na kwa sasa hazisikiki tena?

Shule hizo ni Umbwe, Weruweru, Ashira, Usagara, Galanos, Pugu, Ilboru, azania, Jangwani, Mazengo, Msalato, Iringa Girls, Tosamaganga,, Loleza, Mbeya Sec, Mzumbe, Kibaha, Tanga Tech, Minaki, Nganza, Songea Boys/girls, old Moshi, nk...

Kilichozipoteza shule hizi nini?

mkuu umesahau sengerema
 
Wimbo wa shule tukiwa tumekakamaa ' shule yangu Mara nitakuenziiiii michezo tunacheza vizuri ". Acha kabisa wakuu enzi hizo. Madogo ya siku hizi utoz tu kichwan bure tu
 
Wimbo wa shule tukiwa tumekakamaa ' shule yangu Mara nitakuenziiiii michezo tunacheza vizuri ". Acha kabisa wakuu enzi hizo. Madogo ya siku hizi utoz tu kichwan bure tu

Mkuu sio mitoto tatizo serikali yenyewe ndy ya kulaumiwa kwa sababu watoto wao hawasomi hizo shule.Zamani mwanafunzi akifaulu wenzake walikuwa wanasema mwache anastahili kwenda hizo shule sio sasahivi imekuwa fashion kufauru
 
Nilipita NJOSS kamwe sitaisahau O-level yangu pale. Kushindana kupata div one. Elimu ilikuwa bora sana ila na ukiritimba ulisababisha baadhi ya watu wenye sifa kuliko vizazi kata kukosa nafasi.
 
naona umetaja nganza girlz umeacha NSUMBA boyz wakati hyo ni couple toka enzi za mkoloni...... alichokiunganisha mkoloni mbongo asikitenganishe!!!!!
 
Back
Top Bottom